Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Wakuu kwema..

Mambo ya online business kuna page Instagram wanauza iPhone, nikachati na muuzaji anauza simu used kutoka UK nilitaka iPhone 7+ wao wanauza 450,000 nikawaomba wakanipunguzia mpka 430,000 ijumaa ya tarehe 22 nikawatumia pesa kwa tigo pesa wakala ...

Mwenyewe anadai duka lipo Zanzibar simu ukisha order inakuja na boat ya mchana kwa maelezo yake.... Nilivotuma hiyo pesa aka confirm kwamba kapokea akiniahidi kwamba atanipa mamba ya mtu anaefanya delivery huku Dar ndo maongezi yakaishia hapo...

Kila nkimwambia anitumie hiyo namba kimya na kaniblock jamani naombeni msaada nataka niende police je kuna utaratibu gani huko kwa kesi za kutapeliwa mtandaoni....?? Naombeni muongozo karibuni
Unazingua wewe
 
Pole sana mkuu, hawa matapeli wanafanya biashara ya mtandao kutokuaminika na kuwaharibia wale waaminifu katika biashara hizo. Nimewahi tuma pesa kwa mtu yupo Zanzibar Tsh.mil.2 kasoro kabla ya kupokea mzigo na kesho yake mzigo niliupokea kama nilivyokuwa nimeagiza.

Sema kinachowaponza wengi ni kupenda kitonga, kitu cha mil. 1 unakuta kinauzwa bwelele..Hujiulizi huyu ananunua wapi kwa bei hii na anapataje faida?
 
Nafikiria kufungua darasa kuhusu hawa wauzaji wanaosema wapo zanzibar kwann wasije dar kwa maana wateja wao wengi ni wa dar .km kuna mtu alikuwa anauza mackbook alaf iringa yupo kupatana.com alaf kalipia premier ukifungua tu kupatana matangazo yao yanakaa juuu eti mackbook laki 3 mwizi huyu

Kisa kiliwai nitokea kwa wauzaji wa tv online kwa bei rahisi kutoka znz

Niliona tangazo kupatana nikampigia simu jamaaa akasema duka lake lipo magomeni jitini znz tv nchi 42 smart 450000 akaniambia usafiri kuja dar ni elfu 30 na tv unalipia nusu ukipokea mzigo una malizia basi nikamwambia fresh nakuja mwenyewe znz akaniambia alafu nicheki kwa bahati nzuri nina wanangu kibao jion nikapanda meli hadi zenjibar nikalala kwa msela wangu asubuhi tukazunguka madukani kutafuta tv basi kufika magomeni jitini nikabidi nimtafute yule mwamba aliesema yuko jitini nikampigia simu kapokea nikamuuliza duka lako liko wapi akasema nishakuambia magomen jitin basi nikamwambia mimi nipo jitini hapa jamaaa kastuka sanaaaaa kakata simu hapo hapo kaniblock na tukawa tumeishia hapo sasa nikaanza kuingia kila duka na kuwaelezea wauzaji wa tv wakawa wanasema watu wanalizwa sanaaaaaaa na hao matapeli wa mtandaoni lkn kwann wajinga hawaishi tanzania ???? Unamtumiaji mtu hela hata ofisi yake huijui ni ipi tubadilike wizi upo na corona pia ipo

Angalizo kwa wale waizi wasione km ndio wamepata kwa kuwadhulumu watu ipo siku na wao watadhulumiwa vile vile haki ya mtu haipotei unachokifanya sasa kwa watu utakuja kufanyiwa pia vivyo hivyo chunga sana matendo yako

Nawatakieni corona njema.
 
Hahaaaaaa umepigwa mchana kweupe. Hao wanauza mpaka mckbook kwa laki 5. Yan mackook ya 3m wanauza chin ya 1m. Na wanakuambua tuma nusu nusu unamaliza ukipokea mzigo. Hata kwa akili yako timamu huoni kunaupigaji apo. Nenda police mtamkamata tu uyo.
 
Binafsi mtu akiniambia lazima nitume hela ndo mambo mengine yaendelee napotezea. I prefer 'PAY ON DELIVERY ' type of business. Na mpaka sasa hivi sijawahi kutapeliwa kwenye manunuzi ya online. Nauona mzigo, naridhika ndo nalipia.
 
Pole mkuu, Mimi nilitapeliwa 15000 na wale w unganishwa vifurushi kwa bei poa,nikatuma hela akakubali mwisho was siku nikala block hadi Leo huwezi nishawishi kununua mtandaon,labda official page km kikuu,n.k
 
I phone 7plus kwa 450k umewahi ona wapi hyo bei mzee? Hata kama imetumika nje. Ndo ujifunze uache kupenda vya RAHISI kuwa makini next time Mjuba
Kwangu mimk tatizo sio bei.
Tatizo ni kutuma hela kwa mzimu.
Angefanya background check kidogo.
 
Taja hiyo page nikusaidie kushaghulikia niwepesi. Nakuhakikishia kuwapata.

IMG_4545.jpg
 
Online service unaanzaje kutuma Pesa Kwanza bidhaa haujaiona last time nilikutana na Mtu mtandaoni anauza Flat screen bei chee na akadai yupo karikoo Mtaa Fulani, na anafanya delivery nikamwambia pesa ipo na nikamuagiza na vitu vingine akamtuma Mtu akiwa na risiti na guarantee card za hizo bidhaa, Tukakutana G/mboto Tukatest kama vinapiga kazi vizuri akakubali kwenda na Kunifungia vifaa vyote...

Sasa bro seriously kabisa anaanzaje kutuma Pesa Kwa Mtu ambaye hata humjui, duka lake haulijui.. hata Polisi watakushangaa umeingiaje King kizembe hivyo......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kwema..

Mambo ya online business kuna page Instagram wanauza iPhone, nikachati na muuzaji anauza simu used kutoka UK nilitaka iPhone 7+ wao wanauza 450,000 nikawaomba wakanipunguzia mpka 430,000 ijumaa ya tarehe 22 nikawatumia pesa kwa tigo pesa wakala ...

Mwenyewe anadai duka lipo Zanzibar simu ukisha order inakuja na boat ya mchana kwa maelezo yake.... Nilivotuma hiyo pesa aka confirm kwamba kapokea akiniahidi kwamba atanipa mamba ya mtu anaefanya delivery huku Dar ndo maongezi yakaishia hapo...

Kila nkimwambia anitumie hiyo namba kimya na kaniblock jamani naombeni msaada nataka niende police je kuna utaratibu gani huko kwa kesi za kutapeliwa mtandaoni....?? Naombeni muongozo karibuni
Imeisha hyo

Mloge tu
 
Ntumia 20,000 nikusaidie
 
Back
Top Bottom