Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

Unatumaje hela kwa mtu usiyemfahamu?

Hapo ndugu hauji ibiwa teeena!!!
 
Unatumaje pesa kabla ya kupata bidhaa?
Watanzania tutajifunza lini?
 
Yupo mwingine, anajifanya yupo Kenya, Simu zake anauza bei chini sana.
Ukimuuliza unapataje bidhaa, eti utume pesa, ala yeye akutumie kwenye mabasi.

Na bado watu wanaingia kwenye mtego wa namna hiyo, unatuma hela bila dhamana yeyote ya unaemtumia hela, tunatamani vizuri, ila tahadhari juu ya ulinzi wa pesa yako unahitajika kabla ya kulipia bidhaa hata dukani.
Ni vizuri unaponunua kagua mali ujilidhishe na ubora, kabla ya kulipia bidhaa, ukisha lipa ukagundua udhifu wa bidhaa uliyopewa ni ngumu kwa mfanya biashara kukurejeshea fedha zako. Tuzipe dhamani fedha zetu.
 
screenshot hiyo page tuletee hapa, tutairipoti insta mpaka ifungiwe, tuta comment mpaka insta wenyewe waifunge.

Huyo kasharipotiwa na kufungiwa na cjui anahonga nn hadi insta wanamfungulia na page yake anaipromote sponsors[emoji23] daily ana add new followers
IMG_4545.jpg
 
hivi mnashindwa hata kutaja hizo instagram pages zilizowatapeli , nyie jamaa niaje kwani
 
Mkuu kweli yaani ukatuma hela hivi hivi mtandaoni? Dah kuna watu so innocent yaani unamuamini mtu kirahisi rahisi hivi
 
Khaaaaa
Pole mkuu, Yaaani ukishaona Mtu anauza bidhaa hasa electronics Anadai ana Duka na ni nje ya Dar halafu haanzi kwa kutaja exact location Anajinadi kusema popote tunakutumia, Anza kutumia akili yako vizurii....

Wanatumia trick ya nje ya dar hasa zanzibar maana wanajua Ni ngumu kuifuata,
Na anajua wateja wengi wapo Dar, au Ana ndugu Dar, hivyo akikuambia yupo Dar ni simple tuu utahitaji kumuona au kutuma mtu.

Huyo ni tapeli, hauzi simu na Asilimia kubwa yupo Dar...

Ila vitu vingine ni kujiongeza tuu, sasa kweli mtu anakuambia Anauza simu, yupo Manyara, Tabora, Iringa(kupatana wamejaa hawa) Ukiangalia Mazingira ni bonge ya Duka, Bei nayo hata ya China haioni ndani....

Khaaa sasa kweli kweli kwelii mtanzania mwenzangu Duka la Simu bei chee tena iphones na Macbook za maana likose kote kwa kukaa likae Mara na sumbawanga?????

Halafu pia hii habari ya mjini ya sasa ya free delivery ndio inawaumiza watu..
Ni nzuri ila kiafrica wengi wana mlengo wao mwingine..

Na binafsi hata kama hamna utapeli, sio mpenzi wa biashara za free delivery hasa zile ambazo zinahitaji ukaguzi, bora hizi za kimataifa za kuagiza nje, ila bongo uaminifu bado sana

Raha ya biashara uone bidhaa, ukague, ulidhike, ulipe uchukue..

Sio ulipe uletewe, ulazimike kuchukua,
Ukienda dukani waweza ukutane na option nyingi quality tofauti tofauti uamue mwenyewe ya kuchukua.
well said

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom