Wakuu kuna mtindo wa hawa watu wanaotangaza biashara zao za vifaa vya electronics kutoka Zanzibar, wanaandika kwa Dar ni free delivery na bara wanatuma, kuweni makini na hawa watu ni matapeli.
Wamefungua page zao Instagram na zipo SPONSORED.kama hawa jamaa hapo chini.
MKIANGALIA PAGE NYINGI INSTAGRAM ZIMEANZA NA JINA LA MTU/KITU ALAFU LINAFUATA NENO ELECTRONICS ASILIMIA 99 YA HAO NI MATAPELI,wachache sana kukuta ni wakweli
Kwa mfano unakuta wanajiita
Musa electronics
hemedstore electronics,
tz.electronics,
muzamiru_electronics
mwimbwe electronics,
bm_electronics_tz
Na kadhalika
Hawa ni matapeli,wameshatapeli watu wengi sana.na wanakuwekea screenshot kujionesha walikua wanawasiliana na mteja alie mkoani akiwajibu tayari kapokea mzigo kumbe usanii tu, ukiangalia hata sehemu za comments kwenye page zao za Instagram wamezibock ili kuficha baadhi ya comments za watu wanaowaambia nyie ni matapeli.
Tunaomba serikali na jeshi la polisi liwafuatilie hawa watu wa aina hii na waanze na huyu maana wanaharibu sifa ya watu wengine walio serious wanaotangaza biashara zao kupitia mitandao kama Instagram.wao wanajisajili instagram wanapiga picha za vifaa mbalimbali vya electronics kumbe hawana duka wala nini. Wanaweka namba za simu kuwa trace na kuwakamata ni jambo jepesi tu,ili wasiendelee kuwarubuni watu.wanakuambia lipia mzigo nusu wakutumie mzigo,ukilipa tu wakipokea pesa hawapatikaniki tena.msiwaamini,
Watu waaminifu duniani siku hizi hakuna
Kutambua kua ni matapeli angalia page ya huyu anaye jiita Abdala mohamed Omary, hapo juu,page yake hio hio baada ya muda anabadilisha jina sasa anajiita Abdala ally Mangia,kama ilivyo page yake hio hio hapo chini kushoto,Anabadilisha jina mara kwa mara.
Na anaweka updates ya picha za vifaa vya electronics.kumbe ni tapeli
Hapo chini tena kulia amebadilisha tena jina ni tapeli huyo huyo wa hapo juu,kwa page yake ya Instagram hio hio,hapa chini kabadili picha pamoja na namba za simu, anajiita Ibrahim Chilagula kumbe ni tapeli yule yule.
Ana badili namba za simu na picha akiona ameshajulikana,ila inabidi ashughulikiwe huu ujinga ukomeshwe
Kuweni makini wakuu