Narubongo
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 2,768
- 2,753
harusi ni jambo la kifamilia mimi sitaki kabisa mambo yakuwekana mbele kama padri anaongoza ibada. Kuna rafiki yangu alifunga ndoa mwezi uliopita, aliweka milioni 5 hakuna mchango wa mtu. Tulitoa order hotel moja matata waandae chakula chenye thamani ya sh 20,000 kwa kila mtu, vinywaji tulipiga bajeti ya bia 10 kwa kila mtu yani 25,000 (kumbuka wengine hawanywi pombe gharama inashuka) jumla max 45,000 kwa kila mtu. Waalikwa 30 upande wa bibi na 30 baba.. 45,000*60=2,700,000 iliyobaki ilitumika kwenye mavazi na vitu vingine vidogo vidogo. Sehemu ya shughuli hotel waliandaa kwa gharama zao cause ni order kubwa.. watu walikula wakasaza, wakatambaa tulikesha mpaka majogoo..Hivi kwanini mtu upange shughuli yako binafsi kwa kutegemea pesa za wengine? Halafu hao wengine wasipokupa pesa unastressika... kwanini usifanye unachokiweza?
Mimi hizi mambo nilishazikataaga zamani sana yaani