Kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu anayekuzidi umri sana ni hatari

Kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu anayekuzidi umri sana ni hatari

waterproof

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2020
Posts
388
Reaction score
352
Kuwa katika mahusiano na mwanaume mtu mzima na tajiri ni hatari sana, kwa sababu hiyo ina maana unaweza kuwa na madaraka kidogo juu ya mahusiano. Kwa kukosekana kwa usawa wa madaraka, unaweza ukakosa kuwa na udhibiti wa kufanya maamuzi yako mwenyewe. Mahusiano, katika hali yake ya ubora, ni kuwa na usawa na kuheshimiana.

Katika karne hii ya 21 ya utandawazi wa kiuchumi mawasiliano,miundo mbinu imekua kawaida sana kwa Dada zetu kujali maslahi has a kwenye suala la mahusiano

Hapo namaanisha wasichana wengi kwa karne hii wanapenda wawe katika mahusiano na wanaume wenye uwezo wa kifedha kwasababu ya kutaka kutimiza majukumu yao ya kujikimu

Enzi za babu zetu wasichana walikua wakichagua nani wa kwanza nae maisha na kutafita wsnacho kipata lahashaa hawakua wajinga au mbumbumbu Bali walijielewa kwasababu iliwafanya wawe na sauti na kuheshimiwa katika maamuzi aijajua sababu ilikua ni kabla ya utandawazi au; likua ni tamaduni

Leo hii wasichana hutamani kua katika mahusiano na MTU ambae amejitosheleza kila kitu so dhambi wala kosa Bali hawato weza kuwa na sauti yeyote kwenye Mali alizozikuta na kuhisi ana nyanyaswa na hvyo kupelekea mahusiano meng kuvunjika na ndiko tunakoipata kauli ya "WANAUME WOTE NI MBWA"😂. Ndio madada zetu wamezoea kutuita hvyo yakiwazidia

Kwenye maisha ya ndoa jamani kikubwa kupata MTU mnae sikilizana mambo yote yatakua mepesi kwenu.kumtanguliza mungu kutawafanya muwe na furaha ya milele ndicho nnachomuomba mungu kila siku na naamini mkewangu mama wa familia Yangu ayatoka humuhumu JF naamini katika hilo bado naendelea kusisitiza natafuta mke maana Mungu amenionesha yupo humu JF ajitokeze mapema ili watoto wasichelewe kuanza shule😂😂

Haya ni mawazo Yangu naomba kuwasilisha.
 
Huo umri utategemea na jinsia, kama ni me kuwa mkubwa sio issue ila kama ke ndo ana umri mkubwa hilo ni tatizo
Kwanini kwa ke akiwa mkubwa ni tatizo na kwa me so tatizo huku tukisema binadamu wrote ni sawa?
 
Binafsi napenda mwanaume anizidi umri but not more than 10 years
Pia asiwe na umri mdogo kuliko mimi au asiwe sawa na mimi.
Kibaiolojia mwanamke anawahi kukua kuliko mwanaume.

Lakini huwa wanasema umri ni namba tu!
Kinachomata ni upendo na maelewano.
 
nyie wanaume ambao mnaoa wanawake waliowazidi umri shauli yetu itafika mnaenda kwenye sherehe alafu kuna mda MC atasema wenye ndoa waje mbele alafu mtaanza kukimbiana,, msijali kuna jamaa alikuwa amelopoka hapa nikawa namkoti maneno yake
 
Kwanini kwa ke akiwa mkubwa ni tatizo na kwa me so tatizo huku tukisema binadamu wrote ni sawa?
Sababu mwanamke anazeeka mapema, menopause anafika akiwa na 45, imagine kijana wa miaka 30 anaoa mwanamke wa miaka 45 ambaye hajazaa na lengo la ndoa ni kujenga familia.

Familia itajengwa kwa couple hiyo kweli?
 
Binafsi napenda mwanaume anizidi umri but not more than 10 years
Pia asiwe na umri mdogo kuliko mimi au asiwe sawa na mimi.
Kibaiolojia mwanamke anawahi kukua kuliko mwanaume.

Lakini huwa wanasema umri ni namba tu!
Kinachomata ni upendo na maelewano.
Maana hakuna palipo andikwa au kuwekwa sheria kwambi watu kwenye umri sawa ndo waoane but n maelewano tu
 
Sababu mwanamke anazeeka mapema, menopause anafika akiwa na 45, imagine kijana wa miaka 30 anaoa mwanamke wa miaka 45 ambaye hajazaa na lengo la ndoa ni kujenga familia.

Familia itajengwa kwa couple hiyo kweli?
Shida yetu wanadamu hatuna imani hata punje ya haradani..kwangu Mimi naamin hakuna lishindikanalo kwa mungu
 
nyie wanaume ambao mnaoa wanawake waliowazidi umri shauli yetu itafika mnaenda kwenye sherehe alafu kuna mda MC atasema wenye ndoa waje mbele alafu mtaanza kukimbiana,, msijali kuna jamaa alikuwa amelopoka hapa nikawa namkoti maneno yake
Endelea kuquote na kuona aibu kwenye couple inayoleta maendeleo
 
nachoona zamani mabinti wengi waliolewa na wazee au watu waliowazidi umri kuliko hata sasa hivi na pia walikuwa wana maamuzi madogo sana kuhusu ndoa zao.
Sio wore ndugu ni baadhi
 
Back
Top Bottom