Kuwa na mpenzi "mtoto" inahitaji ujasiri sana

Kuwa na mpenzi "mtoto" inahitaji ujasiri sana

Meridah Tough

Senior Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
136
Reaction score
365
Wakubwa habari zenu?

Leo naleta mada hapa ila kiukweli nina amani na furaha tele ingawa jana nimepigwa kibuti.

Huyu jamaa kwa kweli haeleweki. Yeye mwenyewe pia hajielewi anataka nin katika haya maisha. Ni kijana wa miaka 31, ameajiriwa na amepanga chumba kimoja. Tumefahamiana naye muda mrefu sasa.

Tulipofahamiana, mwenzangu alikuwa akiniheshimu. Na bila kujisifia kiukweli mimi naweza kuwa na mapungufu mengi kama binadamu yeyote lakini kwa kuwa mtiifu, kutohangaika na wanaume na kuwa na mapenzi ya kweli, kiukweli hilo kombe linanihusu.

Sasa sielewi kama mwenzangu amenizoea sana yani sijui. Lakini nilianza kugundua mwenzangu ana vitabia vya kufanya mawasiliano ma ex zake hadi usiku. Jambo ambalo binafsi lilinikera sana. Nilipojaribu kuongea naye, kiukweli alikubali kuwa anachat na mtu ambaye wanalong distance relationship, mwanafunzi wa chuo, 21 years na wamekutana mara mbili toka wafahamiane.

I was very shocked ila nilimbana kuwa achague mtu mmoja abaki naye ili tusiendelee kuumizana. To my suprise, alidai kuwa yeye hana mpango wa kumuacha hata mmoja including me na hataki mwanamke wa kumwambia aache tabia za kuchat na wanawake wengine na yule mwanafunzi ananijua kwa kusikia toka kwake na wala hana tatizo na hilo.

Kwa kweli jambo hili lilinifikirisha sana. Kipindi hiki wakati watu wanahangaika kufanya kila aina ya miradi kuendana sawa na maisha, mwenzangu yuko busy anawaza wanafunzi. Mwanafunzi ambaye anamjibu "Hiyo pesa unatuma au hutumi?" Yeye mwenyewe mshahara haumtoshi hata inanilazimu wakati mwingine kucover expenses ndogondogo.

Conclusion yetu wala haikuwa kwa kugombana wala kupeana maneno machafu, aliniweka wazi kuwa mimi ni muhimu kwake lakini hawezi kuacha kuchat na watoto wake so kama nitavumilia hilo nibaki naye. Kwa kweli, hata kwa kupretend, siwezi baki na mwanaume wa aina hii ambaye anaonyesha dharau kipindi hiki cha mwanzo. Mwanaume ambaye hajui nini anataka katika maisha yake. Niliomba ni bora niondoke katika maisha yake abaki na amani ya kuendelea kuchat.

Kama akijisikia kuoa huyo binti kwa kweli kwangu its real okey sababu siwezi kugombania mwanaume.
 
Dooh ani mtu anakuambia kabisa anacheat na hakuachi wewe wala mchepuko

Mapenzi bwana bora Mtu akucheat kwa Siri na ukimdaka aoneshe kujitetea kuliko huyo anaekubali Namna hio. Mapenzi yenu yatakua hayana Maana Sasa hapo

Bongo kufikia Open relationship kama US Bado sana, Ninae rafiki yangu mzungu(ke) yeye yup kwny Open marriage na jamaa ake yan fresh mtu anamichepuko alaf hakuna noma anadunda nae and everybody knows
 
Huyu alikuwa anaficha. Lakini hawezi kunidanganya hata kidogo. Kwa hiyo nilimbana na ushahidi kabisa hata akaweka wazi hili swala. Na anajua hawezi kuniambia tu "Am sorry sitafanya tena," sababu nitahitaji kuona baadhi ya vitendo kuthibitisha. Kwa hiyo nafuu yake ni kusema ukweli tu.
 
Sidhani kama utamuacha umeshapenda hapo,kuleta uzi hapa ni kutafuta nafuu ya moyo na kuambiwa ni kawaida kwa mwanaume kucheat

Ila bibie fikiria huna hata ndoa ushaanza cover expenses ndogo ndogo je mkiingia huko ndoan si utagharamia hadi hao wanafunzi bila kufahamu au kwa kufahamu ili mradi unabembeleza penzi
 
Hahahaaa hata hili nililifikiria ndio maana nikaamua kuondoka.

Wanasema maisha ni kupanga na kuchagua. Suala la kuondoka sikulifanyia maamuzi kwa mara moja. Nilikaa nikafikiria. Mwisho wangu na yeye ni upi? Nini nahitaji katika maisha yangu? Mimi nataka maisha ya kujiheshimu. Haijalishi kama nipo na mume ama sipo naye. Ila kuwa na mwanaume wa hivi ina maana kuwa maisha ninayoyataka hapo hakuna.

Yeye bado hajui afanye nini. Akipata pesa ni starehe tu. Mara kadhaa hata nimechukua simu yake ila nilichoambulia hata huyo mwanamke mwingine anahangaika na kulalamika sana. Mwanaume anatumia pesa katika starehe inafika kipindi anagombana na mwanafunzi kisha elfu 20 yaani yule mwanafunzi ampe hiyo 20.

So kuleta hapa kuna wengine watajifunza. Wanapitia changamoto za aina hii ila wanalazimisha kubaki katika mahusiano haya. Wakipitia humu na kuona hata comment zenu, akili zinawafunguka. Mimi nimemchukulia kuwa ni mtoto, akili yake haijakomaa.
 
Back
Top Bottom