Kuwa na watoto wengi, kuna faida ama ni hasara?

Kuwa na watoto wengi, kuna faida ama ni hasara?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wazazi wengi tunatofautiana katika kuwa na idadi ya watoto; wapo wanaopenda kuwa na watoto wengi na pia wapo wanaopenda kuwa na watoto wachache.

Kwa jamii yetu ya kiafrika kwa walio wengi, mtoto anakuwa yuko tayari kujitegemea kwa mahitaji yake mwenyewe pale anapofikia miaka 30 na kuendelea; kwa hiyo atakuwa chini ya uangalizi wa mzazi kwa miaka yote 30.

Tuje kimahesabu

Makadirio
  • Mtoto kwa siku anatumia 10,000
  • Mwaka una siku 365
  • Atakaa kwa wazazi, miaka 30
  • Idadi ya watoto 5
Gharama zao kwa miaka 30 ni = 10,000 x 365 x 30 x 5
= 547,500,000/=
Inamaana wazazi watatumia kiasi hiki cha fedha (547,500,000/=) kuwakuza hao watoto mpaka wajitegemee, huku wazazi wakimiliki nyumba ya milioni 20

Bado hujaweka mavazi, ada za shule n.k

Kwa mantiki hiyo; Je, kuwa na watoto wengi ni 'Asset' ama ni 'liability'?
 
Hili ndilo jibu sahihi na ni hitimisho la hii hoja, kila mmoja abaki na kile anachoona yeye ni sahihi kwake ..
Vipi kuhusu garama za malezi; kwa sababu mlo mmoja debe la mahindi linaweza kuisha
 
Afrika tunaishi kwa imani kuwa Mungu akileta mtoto, huleta na sahani yake..

Unaweza kuzaa mmoja na akakupasua kichwa kumtunza, unaweza ukawazaa kumi na ukashangaa unawamudu vyema tu.
Nakubaliana na wewe, ndio maana tunakuwa na changamoto nyingi
 
Kuwa na watoto wengi ni bora kama uwezo wa kuwatunza upo, mwanaume ana uwezo wa kuwa na watoto hata 100 katika umri wa maisha yake ila awe na wake wengi

Ukiwa na mashamba 10 ya heka tano tano unaweza tengeneza estate na na wewe ukawa mzee wa boma( ha ha ha......)
 
😂😂😂
 
Back
Top Bottom