Kuwa na watoto wengi, kuna faida ama ni hasara?

Kuwa na watoto wengi, kuna faida ama ni hasara?

Kila mwaka madarasa mapya yanajengwa, na hayo yaliyopo bado watoto wanarundikana Kama mbuzi, huku ajira ngumu na kupelekea graduates kuwa wengi mtaani.

Hizi kampeni za kusema ni maamuzi ya mtu mwenyewe kuamua kuwa na namba fulani ya watoto hazipo sawa, ndo zinapelekea mabinti wengi wadogo kuwa na watoto wengi majumbani kwa wazazi wao.

Watanzania tunazaliana mno, na hii ni hatari kwa taifa letu hivyo Basi lazima tujitathimini.
we jamaa tz tunazaliana Sana? Waaache watu wazae nchi kubwa hii Kinacho matter ni population density tz tuna 40/ km square ambayo ni bado ndogo sana
 
Kuna wengine wana watoto wengi na hawawatunzi. Kila mtoto anatumiwa na mama mtu
 
Afrika tunaishi kwa imani kuwa Mungu akileta mtoto, huleta na sahani yake..

Unaweza kuzaa mmoja na akakupasua kichwa kumtunza, unaweza ukawazaa kumi na ukashangaa unawamudu vyema tu.
Ubarikiwe na Bwana Yesu Mnazareti.
 
Chakushangaza kwenye haya maisha ni kwamba Elfu ukiwa peke yako kwa siku ukiwa peke yako unakula unamaliza yote na inakutosha vizuri,pia ukiacha Elfu kumi hiyo hiyo kwa familia ya watu watano inawatosha vizuri pia kwahiyo kupanga ni kuchagua
 
Wazazi wengi tunatofautiana katika kuwa na idadi ya watoto; wapo wanaopenda kuwa na watoto wengi na pia wapo wanaopenda kuwa na watoto wachache.

Kwa jamii yetu ya kiafrika kwa walio wengi, mtoto anakuwa yuko tayari kujitegemea kwa mahitaji yake mwenyewe pale anapofikia miaka 30 na kuendelea; kwa hiyo atakuwa chini ya uangalizi wa mzazi kwa miaka yote 30.

Tuje kimahesabu

Makadirio
  • Mtoto kwa siku anatumia 10,000
  • Mwaka una siku 365
  • Atakaa kwa wazazi, miaka 30
  • Idadi ya watoto 5
Gharama zao kwa miaka 30 ni = 10,000 x 365 x 30 x 5
= 547,500,000/=
Inamaana wazazi watatumia kiasi hiki cha fedha (547,500,000/=) kuwakuza hao watoto mpaka wajitegemee, huku wazazi wakimiliki nyumba ya milioni 20

Bado hujaweka mavazi, ada za shule n.k

Kwa mantiki hiyo; Je, kuwa na watoto wengi ni 'Asset' ama ni 'liability'?
Mkuu kwenu mmezaliwa watoto wangap?
 
Kuwa na watoto watatu , hafu unafika miaka 55, unakuta wote wamepatwa na majanga, kupanga ni kuchagua muhimu kuchagua jibu sahihi.
 
Back
Top Bottom