Kuwa wapenzi wa muda mrefu na hadi kufunga ndoa ni kitu kinavutia sana

Ni kweli. Kama siyo type yako ni bure na itakuwa ni kama kujitesa. Ukutane na hawa mwanamke wa uswazi, kila weekend ni sherehe, kwenda kwao ndiyo usiseme, mashoga ndiyo washauri wake wakuu na wewe kidume ni msomi, mwenye mambo ya kisomi halafu utegemee ndoa idumu?
 
Mimi nimeona makosa mawili katika haya maelezo yako kuhusu kuchelewa kufunga ndoa na huyo mpenzi wako wa muda mrefu sasa kama ulivyoeleza hapo kwa kirefu.

Moja;
Ilikuwa ni lazima upewe sababu ya kuendelea kuisubiri hiyo ndoa na ukubaliane na hiyo sababu, siyo tu kusubiri kwa sababu anazozijua peke yake.

Hivyo, kwa kuwa ndoa ni yenu nyote wawili, basi sababu za kuchelewa au kuwahi kwaKe ni lazima ziwe za pamoja.

Mbili;
Nadhani vyuo vyetu vina tatizo, kama mhitimu wa chuo kama wewe kuwa na mpangilio huu wa uandishi naliona tatizo kwenye elimu uliyopitia.

Sio rahisi, mhitimu wa daraja kama lako kuandika taarifa yote hiyo ndefu kwa aya moja tu. Na isiyo na nukta wala mkato. Kwa hakika kama taifa, tuimarishe elimu yetu.

Ova
 
Kuna msela anapiga kampanga akimaliza mastaz amuoe😀😀😀

Omba sana mkuu, maisha ni Vita.
 
Punctuation.
 
Kuna ukweli hapa, me mke wangu tulianza kudeti 2003 wakati huo nipo form 2, tukaja kuoana 2013. Now tuna miaka 10 ya ndoa lkn miaka 20 ya mahusiano. Anasemaga ananijua kama kanizaa yeye [emoji3]
Nyie ndio pure talented in love
 
Asipokusikiliza jua wewe n plan B
 
Wazinzi ndo wanafurahia mahusiano yao ya muda mrefu wakati wazazi wetu waliozeshwa bila ata ya kujuana na mpaka wamezikana

Kukaa kwenye mahusiano mda mrefu ni kutengeneza njia za Uzinzi tu hakuna kingine na mwisho wa siku maumivu yake kuliko ya kumchuna ngozi mbuzi akiwa hai
 
Hongera mkuu,wengine tulipenda sana lakini ilishindikana,hakuna kitu kizuri kama kuanza na kumaliza pamoja,na hakuna kitu kinaumiza kama kuachana na mtu uliyempenda,kuja kupata mwingine umpende kama mwanzo ni vigumu sana japo inatokea lakini kwa uchache sana.

[emoji22][emoji22]
 
Mkuu, huyo ninayemuongelea hapa tuliachana pia. Nakiri niliumia, nilipitia wakati mgumu kumpata kama yeye, mwisho nikakubali kushindwa nikarudi kwake.

Ever since, maisha yamerudi kuwa na maana tena.
Kila mtu ana mtu wake, ukishampata baki nae kwa gharama yoyote.
 
Kuna ukweli hapa, me mke wangu tulianza kudeti 2003 wakati huo nipo form 2, tukaja kuoana 2013. Now tuna miaka 10 ya ndoa lkn miaka 20 ya mahusiano. Anasemaga ananijua kama kanizaa yeye [emoji3]
hahah
 
Sisi tusiokua na bahati ya mapenzi cjui tuna comment wap!!! Hata hivyo ngoja nipunguze stress

KATAA NDOA NI LAANA, NDOA NI USENGE MTUPU.... just joking
 
Sema wameanza kuzini miak 9 nyuma ,usitamani kuwa kama Flani kila Mtu ana ukurasa wake ,one yote yatafichuliwa
 

Muda ni namba tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…