Kuwapa watoto majina ya kigeni Kizungu/Kiarabu ndio usasa au kutojitambua?

Kweli mkuu huku tunataka kiswahili kikuwe huku tunaita watoto majina ya kizungu kama ni vikatuni mbona viko Vingi vya kiswahili bora angemwita hata kirikuu, madenge,....ila kuna padri mmoja alikataa kubatiza watoto majina yakizungu hadi ujue maana ya jina halisi tena liwe la kiswahili au la kilugha kiukweli hata majina tumewazidi hadi wenye Nayo/wazungu
 
Haha
 
Recently nimekutana na mtu anasajili namba ya simu kwa kitambulisho cha NIN kwa jina ka Bandika Bandua Balele
 
Hata kama ningekuwa na mbuzi nisingemuita madenge/kirikuu.
 
Waafrika tulishavurugwa kitambo,ila hili sio jambo la kwanza, Hayati Dikteta Mobutu Sese Seko Kuku Ngwendu wa Zabanga alipiga marufuku majina ya kigeni ndani ya Nchi yake ya Zaire

Ndio tukawapata akina Kabasele ya Mpanya
 
Majini yanajua jina ? Du kweli waafrika bado tupo gizani.
Majini yana macho na akili ya kibinadamu !!!!!
 
mi katika vitu nilivyokataa mapema ni hili la kuita watoto majina ya kizungu. nilipata uzoefu nilivyotengeneza viatu vyangu vikakamatwa kisa jina langu la kizungu pale hongkong wakasema ni kopi vikataifishwa.
 
Naunga mkono hoja... Maaana hata uislam umesema tuwape watoto wetu majina mazuri... Ila haujasema tuwape ya kiarabu pekee imesema majina mazur tuh.. Afu kingine kila mzazi apangiwi jina we ukiwa na wanao waite utakavyo c hatutokupinga.... Ila majina ya kizaramo mabaya aisee mara sikujua,chausiku,shida,mwakatobe .....kwa hio sometimes ya kizungu na kiarabu ni bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…