Kuwapa watoto majina ya kigeni Kizungu/Kiarabu ndio usasa au kutojitambua?

Izi bando mzitumie vizuri na uzi za kijinga zisiekwe. Kila mtu ana choice yake na sababu ya kupatiwa mtoto wake jina husika. Haijaalishi km ni kiswahili, kiluga, kizungu, kiarabu wala la lugha yoyote. Kuna choice moja na reason mbili. Ww unajisumbua kuhamaki buree ulitaka aitwe nani? Si uzae wako alaf ndo uhamaki akipewa Jina hutaki!!!
 
Labda nikuulize swali mkuu..nini maana ya jina ambangile

Ambangile ni jina la Kinyaki (kimila) ambalo maana yake mimi siijui kwa kuwa si Mnyaki, ila lina maana.

Ngoja tumsikie Gwappo Mwakatobe.

Na hiyo ndo haswaaa hoja yangu, kwamba majina yaliyopo mazuri ni ya kilugha na si ya Kiswahili.

Kwa kiswahili utaambulia VIELEZI na majina ya vitu, ndiyo maana wengi wanaangukia humo au yale ya Kiebrania kina Samweli sijui Yohana wakidhani ni ya Kiswahili.
 
Mkuu mbona Povu???
Mwanao umemwita Lulu nini
Ahahaha hapana mkuu,Mimi sina mtoto bado lakini nimekumaind vile umetaja majina mabaya matupu wakati majina mazuri yapo kibao Tu

By the way Nina ndugu mtoto wa babaangu mdogo anaitwa si_kitu sijui Mzee aliwaza nn kumpa mtt wa kike jina la hovyo vile
 

Kama unataka haki ya kila mtu kuita jina analotaka, mbona hutambui haki ya mwezio kuanzisha UZI anavyotaka..!!
 
Naitwa Mapito mzee wangu anaitwa mzee Mwanza Jee kuna kauzungu. Hapoooo
 
Lakn mkuu hata hayo majina so called ya Dini ukichimba maana yake unakuja kuambiwa ni kielezi au kihisishi(Mimi siyo mtaalamu wa Kiswahili ) mfano jina Jacob au John au Mohamed au ashura ukigoogle maana ya jina ndy tunarudi huku huku Kwa kina Lulu na furaha Tu mkuu..hii imekaaje
 
Forest hill ni jina la kinyakyusa?

Toa kwanza kibanzi cha kwenye jicho lako
 

Lulu ni madini, lina maana gani?

Ashura ni jina la mtu lenye maana 1, 2, 3... (kama zipo)...

Furaha ni hisia, wabongo kwa 'uzungu' wanaita Happyness (ingawa sijawahi kusikia mzungu mwenye jina hilo) [emoji23][emoji23][emoji23].

Bado nasisitiza HAKUNA majina ya WATU yenye asili ya KISWAHILI.

Hatuna namna, tuendelee kukwapua majina ya VITU tu, enhee!!
 
Ukweli hayo majina ya kigeni yametokana na tamaduni za huko yalikotoka hayajatoka peponi au mbinguni. Haya ya asili yetu yanaonekana ya kishetani.
 
Tuanzie hapa,kama ni me kwanini umetahiriwa,ukiumwa kwanini unaenda hospitali,ukitaka kusafiri kwanini unapanda ndege,ukitoka kuoga kwanini unavaa nguo?hayo yote umeiga wazungu sio asili yetu,tuendelee tu mkuu na maisha,tukubali kuwa tulitawaliwa nao na sasa tunaishi kama wao,tukubali tu yaishe...
 
🤣🤣Wacha Tu tukubaliane ktk kutokukubaliana..binafsi nikija kujaaliwa kupata mtoto nitapendekeza jina la Kiswahili ingawa unasema hakuna jina la Kiswahili🤣🤣potelea mbali..Ila sioni tatizo lolote kumpa mtoto jina lolote liwe la kizungu kiarabu nk,so tupo pamoja mkuu🙏
 

Pamoja mkuu.[emoji847]

Kwa kumalizia tu niseme, Sato Hiroshi ni jina la Kijapani.[emoji1493][emoji1493][emoji1493]
 
Pamoja mkuu.[emoji847]

Kwa kumalizia tu niseme, Sato Hiroshi ni jina la Kijapani.[emoji1493][emoji1493][emoji1493]
Ahahahah yah ni jina la kijapan kweli
Lina historia kdogo ktk harakati zangu

Kipindi nipo skuli nilikuwa mpenzi sn wa muvi,siku moja nikakutana na muvi Kali sn starring allitwa Satoh Hiroshi,jamaa nilitokea kumkubali sn Hadi kwenye madaftari nikaandika Hilo jina badala ya jina langu halisi(utoto Raha Sana ),na wenzangu wakaanza kulizoea Hilo jina

Pia ndy ukawa mwanzo wa kujifundisha martial art..Kwa hiyo jamaa alini inspire sn ndy maana Hadi huku nimekuja na id ya Hilo jina..ni hivyo yani
 
Punguza jazba
 

Ungeorodhesha baadhi ya hayo majina ya kikwetu ili watu waanze kuwapa watoto wao, vinginevyo ni vigumu kuwapa majina ambayo hayafahamiki watoto!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…