Kuwapiga wanawake hivi sio sawa hata kama ni wezi

Kuwapiga wanawake hivi sio sawa hata kama ni wezi

Hao wapumbavu ningewasukuma ndani ,hii clip kama ni current imfikie mama yetu,,kama ni ya tendo limefanyika Ndani TZ Territorial area ....

Kwa kosa gani?. Kwenye sheria hatuendi hivyo. Tunaangalia msabababishaji wa tukio. Hao vibaka wasingeenda happy dukani nani angewapiga?. Unaongea kana kwamba wamevamiwa kwao wakati wao ndio wamevamia dukani kwa mtu.
 
Kwa kosa gani?. Kwenye sheria hatuendi hivyo. Tunaangalia msabababishaji wa tukio. Hao vibaka wasingeenda happy dukani nani angewapiga?. Unaongea kana kwamba wamevamiwa kwao wakati wao ndio wamevamia dukani kwa mtu.
Unajua nyie watanzania wengi ndo mnaofugaga matatizo. Ooh tumsamehe, ooh ni mmama hao ndo wanaofukuzisha wamama wenzao kazi, mtu kila siku dukani vitu vinapungua unaambiwa wewe ndo unaiba dukani kumbe mpumbavu mmoja tu.
 
Mwizi ni mwizi haijalishi ni mtu wa aina gani kinachoangaliwa pale ni kile kitendo anachokifanya, sasa basi mtu anapofanya kitendo cha wizi halafu mkamkamata na kutokana labda yeye ni mmamama kama hao hapo mkasema mumsamehe nakuhakikishia asilimia kubwa ataendelea kufanya huo wizi wake kwengine. Huko sasa ataenda kuibia wahuni wamuue,

Halafu mwizi hapigwagwi bakora tena mikononi, h jamaa naona kabisa walizingatia kigezo cha huruma . Swhemu nyngne wangepigwa mawe na marungu wakitoka hapo wanakaa hospita miezi mitatu hawarudii tena unakua umewaokoa.
 
Ila Wanaume wanahuruma sana. Hii video imesambaa maeneo mengi kila nikisoma comment naona wanaume badala ya kushabikia hicho kipigo wameumia ingawa hao wanawake ni wezi ila nimeona wanaume wengi hilo hawajapay attention sana wamelipa uzito swala la kwann hao wanawake wamesulubiwa kama sio wanawake.

Nikajifunza kitu kuhusu mioyo ya wanaume kwa wanaume. Aiseee wanaume tubarikiwe na mwanamke yoyote anayedharau, kuchukia, au kumuongelea vibaya mwanaume yoyote MUNGU anamuona na atampa adhabu yake. Wanaume wanastaili mauwa mengi sana popote walipo.
 
Duh mbaya sana aisee. Halafu sijui kabila gani hawa majamaa wana sound warugaruga.
Wanaonekana ni watu wa pande za ziwa Victoria kule. Maana wale maeneo ya akina mura kule huwa hawanaga simile kwenye kutoa dozi mwanamke anakung'utwa kama si tatizo vile.
 
Wenye pesa wengi hasa wafanyabiashara ni watu wasio na elimu na wametokea maisha magumu sana sana

mpaka biashara zao zinafika hapo wamepitia mengi,kaloga,kafanya kila fekeche analolijua la hatari afike hapo

mtu mmoja unaenda iba duka la mtu kama huyo Uta safa ze konsekwenses, nenda kaibie wasomi huko walio ktk

biashara kama kina vunja bei,and make sure unaiba eneo vunja bei yupo ili ukidakwa Huruma ipite,ila ukiiba kwa vijana

wa vunjabei wakakudaka wao,wakati washakatwa mihahara yao sana na bosi kwa kuambiwa wao ndio wezi

asee hamna rangi utaacha ona,Ki ufupi kuchukua sheria mkononi kuna wakati inabidi tu,Ni makosa lakini nakuhakikishia

hata wewe unaesema sheria isichukuliwe mkononi ni kwa vile hili unaliona jepesi,ila yapo mambo ukifanyiwa Hutokaa ukumbuke polisi,kanisa,imamu,Mungu,wala MALAIKA wake Utatoa adhabu ya kufa mtu kwa muhusika.

Ki ufupi,hebu kila mtu acheze kwenye line yake usimkanyage mwenzio Tusipangiane adhabu za kuwapa wanaotujeruhi hisia na miili yetu na mali zetu,Tusipangiane kabisa.

Nasemaga mimi ukiingia 18 zangu tena nmekudaka uwe mwizi,uwe adui yangu kwa namna yyte ile bana weee bana weeee,simpigi hata kiduchu ila atakufa kwa KIU na NJAA yani ndio kitu pekee naweza mpa mtu ataeingia 18 zangu.
 
Dah hii imenikumbusha tukio moja la mdada wa mjini hawa masista duu hawa ukimuona hivi huwezi dhania kuwa ana matukio ya wizi.

Huyo dada mishe zake ilikuwa ni kuwarubuni bodaboda kwa kuwachukua kama mteja wa kawaida halafu kuna chimbo anawapeleka huko nje ya mji wanachezea kabali wananyang'anywa pikipiki zao na vibaka wanaokuwa wamejibanza huko vichakani.

Sasa kwasababu ni mchezo wake. Kuna kijana nadhani alimshika sura kuna bodaboda mwenzao aliuwawa na kuporwa pikipiki yake ilikuwa ni mpya kabisa.

Jamaa aliwajulisha wenzake na ndipo ukawekwa mtego. Wa kumfuatilia na wakabaini kuwa ni mshiriki wa haya matukio.

Dah aiseee aliamshiwa shughuli na akakiri kuwa ni kweli amefanya hayo matukio. Dah walichomfanya lile tukio hadi leo bado linani haunt kichwani.

Mdada alikuwa anapigwa mateke, magumi, makofi, vimbo kama mwanaume. Akadondoka chini wadau wakaanza mponda na mawe. Wakamchakaza hakupona. Alifia pale pale.

Dah nikasema jamani huyu si mngembeba anakula vibao viwili vitatu halafu mnaenda nae huko geto mkaishi nae kama mwezi hivi chini ya ulinzi mkali na apate chakula vizuri na kupewa mazingira ya usafi vizuri, ila atoe gemu kwa wana kiroho safi kama msamaha wake.

Then ndio apelekwe polisi.

Dah ila ni ngumu sana kutazama mwanamke anapigwa huwa kuna roho inakataa kabisa na kuruhusu hilo litokee wanaume tunahuruma sana na hawa viumbe. Ila hata wao mwizi anapokuwa anapigwa wengi huwa wanalia na kupiga makelele na kuhimiza mwizi asiendelee kupigwa sababu hawawezi vumilia kuona mtu anafanyiwa mateso.

Ugomvi wa mwanaume na mwanamke huwa unamalizwa kitandani.
 
Basi wewe ni mbaya kuliko hao wezi. Wewe ni katili kabisa.
Naam! Nitaendelea kuwa katili mpaka wajitafutie njia sahihi ya kujipatia kipato, hatukuiba tulivyo navyo, tulivitafuta kwa jasho!

Niliwekwa kati na wezi miaka fulani, mmoja wao alikuwa mwanamke, walikuwa na mapanga na bisibisi, walishawahi kuruka pia ukuta wakaiba kila kitu kwenye gari wakaniachia nusu gari, walishawahi kuiba dukani kwangu wakasafisha walivyoweza kusafisha! Worse enough ni pale walipomkata kata dada yangu panga, sina huruma na mwizi, jinsia yeyote
 
Naam! Nitaendelea kuwa katili mpaka wajitafutie njia sahihi ya kujipatia kipato, hatukuiba tulivyo navyo, tulivitafuta kwa jasho!

Niliwekwa kati na wezi miaka fulani, mmoja wao alikuwa mwanamke, walikuwa na mapanga na bisibisi, walishawahi kuruka pia ukuta wakaiba kila kitu kwenye gari wakaniachia nusu gari, walishawahi kuiba dukani kwangu wakasafisha walivyoweza kusafisha! Worse enough ni pale walipomkata kata dada yangu panga, sina huruma na mwizi, jinsia yeyote
I know. Wewe huwachukii kuliko mimi. Mwizi akikupatia kwenye anga zake anakuumiza vibaya sana na hata kukuua. Mimi nilichosema ni kutumia nguvu inayolingana na jinsi mwizi alivyokujia na anavyo-behave baada ya kumuweka kwenye ulinzi. Unaweza kumpa bakora ndiyo hasa ukizingatia kuwa polisi hawachukulii serious lakini siyo upige kama unaua. Hao kina mama kipigo walichopata hakiendani na haya niliyoelezea.
 
Kwanza hapo kuwaonea huruma kwa kuwa ni wanawake ingekuwa walioiba ni wa kiume hapo yangekuwa mengine
 
Waume zao wawapage pesa sio kutembeza miili mikubwa madukani kwa watu kumbe majizi
Wee unadhani walivyonaswa hapo hiyo ni siku yao ya kwanza?

Ukute wana maduka yao, wanakusanya wanaenda kuuzia madukani kwao.

Hapo mwanaume hauwezi jua lolote kuhusu uozo huo.

Unaagwa vizuri tu kuwa wanaenda mjini kununua vifaa na wala haombwi hela, ni michezo yao ya kila siku wanajifanya wajasiria mali.
 
Hata kuwapiga picha/video wakikiri kuwa wameiba ni adhabu tosha pia na sio kuwapiga kiasi kile si sawa
 
Back
Top Bottom