Kuwapiga wanawake hivi sio sawa hata kama ni wezi

Acha zako. Wanaume nao je?. Mwizi ni mwizi tu. Kuchukua sheria mkononi ndio hatakiwi tena kwa wote. Wanawake hivi sasa ni manunda kweli
 
ndio maana nikasema Real man sijamaaniaha wote,sikushangai kwa maana unaonekana sio mmojawapo so endelea kuwala stiki bt if you are Real Man you will Never do that
Wacha weeeeee, real men unamaanisha nini?
 
Sio wanawake tuu. Hata wanaume kupigwa hivyo si sawa
Tuschukue sheria mkononi
Tatizo wakuu mnaangalia upande mmoja tu wa shilingi.

Hamjadili sababu iliyopelekea kuudhi umma!

Wizi pia ni tabia ya kukemea bila ya kumumunya maneno.

Tunatakiwa kwanza kwa pamoja tuikemee tabia chafu ya wizi na udokozi maana inarudisha nyuma maendeleo ya watu.

Haijalishi jinsia ya mwizi, wizi kwa ujumla haufai.
 
Mwizi hana ubavu wa kufungua kesi ya malalamiko wala madai ya fidia baada ya kupondwa na kadamnasi yenye hasira.

Hapo anataka yaishe, ajikung'ute vumbi aondoke huku akificha sura kukwepa kutambuliwa na wanaomjua.

Tunachokikosea sana kujaji mtu kwa sura na jinsia, hilo ni kosa tunafanya.

Ukipata msala wa kusafishwa na dizaini ya hao wanawake, hauwezi tena kuwahurumia ama kutoa wazo la kuwakinga!

Hao ni vibaka kama vibaka wengine.
 
Na mwenye duka anafungua kesi ya wizi na upotev wa mali na uharibifu..fidia b10...
ishu inakuja kwenye vidhibiti ulivyomshika navyo huyo mwizi viko wapi..?? hapo wao wenyewe wameshaharibu mazingira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…