Kuwapiga wanawake hivi sio sawa hata kama ni wezi

Kwa hiyo kuwapiga ndio adhabu yake, hawakuwa tishio hao wangeweza kabisa kuwashika na kuita polisi, tuache kuishi kama wanyama
Mkuu wezi sio watu wazuri hata kidogo ukiwapeleka polisi wanatolewa dhamana wanatoka then wanaendelea kuiba tena wengine wakitoka wanawatafuta waliowapeleka polisi wanaweza kukuua, dawa ya mwizi ni kipigo tu ila sisupport kuuwawa
 
Sio wanawake tuu. Hata wanaume kupigwa hivyo si sawa
Tuschukue sheria mkononi
Unaamka asubuh unakuta nyavyu ichana mwizi kapita cm ya suruali yako ulo8 Jana uliotundika ktk msumari.
 
Mtu wa hivyo mkuu unaachana naye hajui maumivu watu wanaopitia, jamaa alibiwa vitu ndani pamoja na document za ofisi aliweka kwenye begi wakadhani ni pesa, alikaa ndani mwaka mzima ofisi ikajua anawachezea game halafu huyo mtu akutane na mwizi kwamba amwambie hongera
 
Kuna upigaji mwingine siyo mtu unampiga kichwani akifariki inakuaje, hiyo si adhabu, kingine wanao mpiga ni watoto wanao weza kuita mama.......
Wizi sio mzuri ila sijapenda hao kupigwa style hiyo.
 
Hata mimi imenikwanza sana, mwanaume inakuwaje unampiga hivyo mwanamke............hata hapa nimebishana na wife nikamweleza ni bora hata wangetafuta wanawake wenzao ndo wawaadhibu au wawasute, naturally haijakaa vyema.
Angefanikiwa kuiba,aliyeibiwa ingekuaje ?
Hapo swala sio mwanamke bali ni mwizi.
Kama unaona huyo mwanamke hakupaswa kupigwa namna hiyo basi hata mwanaume asingepaswa kupigwa namna .
 
Mwizi ni mwizi tu haijalishi kama ni mwanamke au mwanaume. Kama unaweza kuwa na muda wa kumdadisi mwizi mwanamke kwa nini usipate muda kama huo wa kumpakata mwizi mwanaume na kumdadisi mazingira yaliyopelekea kujiingiza kwenye wizi? Issue kubwa au tatizo hapa ni mtu au watu kujichukulia sheria mkononi. Sympathy zingine tunazoonyeshwa na baadhi ya wachangiaji ni zile za "mitandaoni" tu lakini pindi ukiibiwa utabadilisha kauli.
 
Hao wapumbavu ningewasukuma ndani ,hii clip kama ni current imfikie mama yetu,,kama ni ya tendo limefanyika Ndani TZ Territorial area ....
 
Nimeshindwa kuangalia video yote aisee!
Daah😭😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…