MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ninaandika huu uzi nikiwa na hasira iliyochanganyikana na huzuni kwa huu mmomonyoko wa maadili unaozidi kuota mizizi. Jamii kwa sasa iko bize kushabikia mambo ya kipuuzi huku ikiachana na agenda muhimu za kitaifa. Picha na video chafu zimekuwa na thamani kuliko mambo mengi yenye tija mitandaoni.
Jana ilikuwa na habari iliyovuma sana kuhusu Mama Wema na Luludiva kwa habari ya video zao chafu. Ila leo ghafla habari inayoenea ni Nandy na Billnas kupeana mimba kabla ya ndoa na kuutangazia umma kupitia mitandao ya kijamii. Wamasambaza picha zao za kimahaba huku Nandy akiwa tumbo wazi.
Walichokifanya hakikubaliki kwa mila na desturi zetu pia hata kiimani ya kikristo. Hakuna kabila wala dhehebu la kikristo linaloruhusu kupeana mimba kabla ya ndoa. Pia hakuna kabila wala kanisa linaloruhusu kusambaza picha za mama mjamzito akiwa tumbo wazi. Walichofanya ni kinyume kabisa na maadili ya kimila na kikanisa. Wote wanaowasifia pia wanafanya upuuzi. Binafsi NASUBIRI KUONA KANISA LITAKALOWAFUNGISHA HIYO NDOA WATU HAWA WAWILI inaosemekana wanapendana sana.