Kuwasifia Nandy & Billnas kupeana mimba nje ya ndoa ni ukosefu wa maadili

Kuwasifia Nandy & Billnas kupeana mimba nje ya ndoa ni ukosefu wa maadili

Ndugu Kiranga nyie ndo wale mnaotetea ushoga kwamba ni uhuru binafsi. Kama kungekuwa hakuna kuongelea mambo ambayo hayako sawa kwenye jamii basi kusingekuwa na haja ya mahakama wala polisi. Kwa mfano wewe Kiranga itokee hata muujiza umepata mamilioni ya hela kisha nenda kaweke kwenye akaunti yako uone kama hutatafutwa utolee maelezo hata kama ni zako. Acha kutetea upuuzi kwa hicho kiingereza chako cha juhudi binafsi.
Ushoga ni uhuru binafsi, na wewe si mahakama wala polisi.

Mfano wako wa mimi kuweka hela zangu kwenye akaunti yangu, wewe hiuna haki ya kuniingilia, kuna sheria na watu wenye mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Watanzania wengi mnapenda kuingilia mambo ya binafsi ya watu wasiowajua, wasiowajali wala kuwaelea.

Ni aina fulani ya frustrations za maisha.

Mnapenda ku control maisha ya watu.

Tatizo hao watu hata hawawajui.
 
Wazee wazima tunajadili mimba za vijana wadogo wakati dada zetu nao washazalishwa huko majumbani mwetu!
 
Some people want to control other people.

All this virtue signaling is just a mean to that end.

Whether they know it, or not.

Issue ni, kimsingi Billnas anaambiwa "Kwa nini unaishi maisha yako kwa uhuru wako na raha zako? Mimi sipendi kukuona unafurahi hivyo, nataka kuku control uishi ninavyotaka mimi, probably kimasikini kama mimi, kwa woga wa kuogopa jamii kama mimi"

Poor, unsuccessful, fearful, unfree people hate it when they see rich, successful, daring, free people living their best lives without a care for some bullshit societal rules.

They unfree hate that.They want to stop that at any cost. they want to control other people's lives.

Deep down, this is the problem.
 
Mambo yao waachie wenyewe, yasikuumize kichwa...
 
Huoni watu wanasifia DC Kubeba mimba bila kuwa na ndoa. Hovyo kabisa kizazi hiki
 
Pole sana Mkuu na ujitulize usije pata kiharusi bure maana siku hizi hiyo ndio fasheni na ndio dunia ilipofikia kwa sasa. Nakumbuka zamani kwa dini yetu huko kwetu Mashikolombwinde Mchungaji hafungi ndoa ya mwanamke mjamzito.
 
Achana na maisha ya watu wewe pambana na yako, kwani wao ni wa kwanza??!!!
 
Ninaandika huu uzi nikiwa na hasira iliyochanganyikana na huzuni kwa huu mmomonyoko wa maadili unaozidi kuota mizizi. Jamii kwa sasa iko bize kushabikia mambo ya kipuuzi huku ikiachana na agenda muhimu za kitaifa. Picha na video chafu zimekuwa na thamani kuliko mambo mengi yenye tija mitandaoni.

Jana ilikuwa na habari iliyovuma sana kuhusu Mama Wema na Luludiva kwa habari ya video zao chafu. Ila leo ghafla habari inayoenea ni Nandy na Billnas kupeana mimba kabla ya ndoa na kuutangazia umma kupitia mitandao ya kijamii. Wamasambaza picha zao za kimahaba huku Nandy akiwa tumbo wazi.

Walichokifanya hakikubaliki kwa mila na desturi zetu pia hata kiimani ya kikristo. Hakuna kabila wala dhehebu la kikristo linaloruhusu kupeana mimba kabla ya ndoa. Pia hakuna kabila wala kanisa linaloruhusu kusambaza picha za mama mjamzito akiwa tumbo wazi. Walichofanya ni kinyume kabisa na maadili ya kimila na kikanisa. Wote wanaowasifia pia wanafanya upuuzi. Binafsi NASUBIRI KUONA KANISA LITAKALOWAFUNGISHA HIYO NDOA WATU HAWA WAWILI inaosemekana wanapendana sana.
Acha wivu, wangapi wana mimba kabla ya ndoa dunia hii?
 
As gentleman uliekamilika Kiakili/kifikra, huwezi kufanya huu nnaoweza kuuita utoto+upuuzi kama mwanaume Kamili utangaze mkeo kuwa mjamzito!? Hakuna hongera kwa mjamzito! Bali kwa kujifungua salama!
 
Ninaandika huu uzi nikiwa na hasira iliyochanganyikana na huzuni kwa huu mmomonyoko wa maadili unaozidi kuota mizizi. Jamii kwa sasa iko bize kushabikia mambo ya kipuuzi huku ikiachana na agenda muhimu za kitaifa. Picha na video chafu zimekuwa na thamani kuliko mambo mengi yenye tija mitandaoni.

Jana ilikuwa na habari iliyovuma sana kuhusu Mama Wema na Luludiva kwa habari ya video zao chafu. Ila leo ghafla habari inayoenea ni Nandy na Billnas kupeana mimba kabla ya ndoa na kuutangazia umma kupitia mitandao ya kijamii. Wamasambaza picha zao za kimahaba huku Nandy akiwa tumbo wazi.

Walichokifanya hakikubaliki kwa mila na desturi zetu pia hata kiimani ya kikristo. Hakuna kabila wala dhehebu la kikristo linaloruhusu kupeana mimba kabla ya ndoa. Pia hakuna kabila wala kanisa linaloruhusu kusambaza picha za mama mjamzito akiwa tumbo wazi. Walichofanya ni kinyume kabisa na maadili ya kimila na kikanisa. Wote wanaowasifia pia wanafanya upuuzi. Binafsi NASUBIRI KUONA KANISA LITAKALOWAFUNGISHA HIYO NDOA WATU HAWA WAWILI inaosemekana wanapendana sana.
Ndoa sio kwenda Kanisani au Msikitini, mkishatambulishwa kwa ndugu wa pande zote mbili na kulipiwa mahari hiyo tayari ni ndoa.
 
Acha kupanic na vitu vya kawaida, "Ndoa hufungwa na MUNGU binadamu Ni mashahidi tu" hizi Taratibu za kibinadamu tu namna ya kujifurahisha tu! Co-creation= GOD+father+Mother , mtoto anazaliwa kwa uwezo wa MUNGU tu!, That's why we don't say street children lather homeless kids, kwasababu mitaa haitungishi mimba.
 
Back
Top Bottom