Kuwe na adhabuya kifungo kwa wazazi / walezi wanaoficha ndani watoto walemavu, ni ukiukaji wa haki za mtoto

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kuna kipindi niliwahi kuwa mtaa moja na familia flani, wengi tulijua kwamba wapo watatu tu ni mpaka siku ya msiba wa mtoto mlemavu ndio tukajua kuwa kulikuwa na mtoto wa ziada, ni jambo lililonishangaza sana.

Na chanzo kikuu bila kupepesa macho huwa ni kwamba wazazi wanaona aibu kwenye jamii kuhofia kusemwa vibaya, hizo sababu zingine kwamba ni kwajili ya usalama wa mtoto ni kivuli tu cha kujifichia.

wapo wazazi wanaothubutu kuwafungulia watoto kwanini wengine wafungie ?

adhabu iwepo ya kifungo ama faini ya milioni 5
 
Hapa Waziri wetu mpendwa Gwajima angesema kitu.
 
Akifungwa utamlea wewe huyo mtoto
 
Isitolewe tu adhabu, watu waelimishwe, Mambo kama haya ni ukosefu wa elimu, ulemavu sio dhambi,hakuna anayeomba kuzaliwa mremavu!
Tekinolojia sasa hv imeweka miumdombinu, mtoto, kiziwi, kipofu,bubu, mremavu wa viungo, anasoma vzr tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…