Kuyafikia mafanikio ya ufugaji kwa kuku wa broiler

Kuyafikia mafanikio ya ufugaji kwa kuku wa broiler

Mimi naomba kujua,
1. unatreat maji ya kuywa au unawapa tu kutoka kwenye bomba/ na kama untreat unatumia dawa gani?
Virid
2. Nimevutiwa kujua pia formula yako ya chakula unayochanganya hadi kuku wanenepe kufikia 1.5kgs ndani ya siku 28 ninajua kwa watu wengi huishia 1kg
Hii ni Siri hawez kukupa
 
Mtaalamu, hvv bila madawa broilers hawafugiki?
Mtaani huku watu hawali kwa kigezo kuwa n kuku wanasemekena wanakuzwa kwa madawa....yaan kuku mwanzo mwisho ni kulishwa hayo ma OTC n.k
Kuhusu dawa hapa wengi hawana uelewa kutokana na kulishwa rumors mfano kuna kuwakinga na magonjwa hasa wiki mbili za mwanzo baada ya hapo dawa unayoweza toa ni ya coccidiosis na vitamini angalau mara mbili kwa wiki ila cha kuzingatia hapa wiki moja kabla ya kwenda sokoni ni kuwapa maji tu ambayo hayana dawa basi
 
Mimi naomba kujua,
1. unatreat maji ya kuywa au unawapa tu kutoka kwenye bomba/ na kama untreat unatumia dawa gani?
2. Nimevutiwa kujua pia formula yako ya chakula unayochanganya hadi kuku wanenepe kufikia 1.5kgs ndani ya siku 28 ninajua kwa watu wengi huishia 1kg
1. Maji ya kuku ni vyema yatulie kidogo ata siku moja mbele kwan yako na chlorine na uwa inaevaporate na kipindi ambacho utumii dawa ni vyema kama waterguard ipo unaweza kuwa unatibu vimelea hasa wa typhoid na cholera.
2 . Kuhusu chakula bado naendelea na trial lakin matokeo ni mazuri na uwa naselect kuku nawatenga naendelea kuwaangalia kwa ukaribu zaidi na mpaka sasa formula nayotumia ni kuwa na mchanganyiko wa vyakula mfano mashudu,mtama,damu ,pumba n.k ambayo natengeneza kilo 332 na kupeletize hicho chakula alafu naweka na portion ya hizi mifuko ya grower ili kubalance kiwango cha protein . Nafanya hivi kwani chakula lazima ukipime maabara na kwa bongo maabara zipo chache sana lakin in field uwezi kusubili inabidi ujiongeze kwa udadisi zaid.
 
Nimekuwa katika industry ya kilimo na ufugaji na nimejifunza mengi kwani kuna changamoto nyingi kuanzia unapoweka kuku bandani siku ya kwanza hadi unawatoa.

Kila wiki katika ufugaji inakuja na changamoto yake , umakini hasa unaitajika siku za mwanzo ukianza vibaya utaona kila rangi na unaweza kulitelekeza banda kwa uzembe , mfano kwa mkoa niliopo kuku uanza kutoka siku ya 25 kufikia siku ya 30 kama soko limekaa vizuri wanakuwa wameisha bandani na hapa ndo trick ya ulishaji wa chakula ilipo ili kufikia uzito mzuri wa kilo 1.8 hadi 2 inapogonga siku ya 28.

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuwa watu wanatumia bidhaa zisizo faa kunenepesha kuku hao jambo ambalo kwa upande wangu sina uhakika nalo kwani mm na uzoefu wangu nimekuwa nikitumia chakula cha makampuni na portion ya kuchanganya mwenyewe kwa formula ambazo naendelea kuziboresha kila batch na matokeo ni mazuri sana . Pchani ni kuku wa siku 28.
Karibuni wadau tushare madini hasa ya ghalama hasa inayogharimu kila kuku mpaka kumtoa ,madawa na mbinu za kuyafikia masoko
View attachment 3654566
Ongera bana, dah,hawa kuku wameharibu ndoto yangu mwaka huuu hatari sana. Nimerudi kuwa kapuku wakati nilishapiga hatua sana.
 
Nguvu kazi, mabanda, Dactar (constant) pia uziweke hata hivyo gharama ya 6K per kuku ni kubwa ujitahidi kupunguza
Nakupata kiongozi , unaweza kushare pia jinsi unavyocut cost kuwa chini ya hiyo bei ya elfu 6 kwa siku 28 tunaweza kupata mwanga zaidi kwani cost kubwa hapa ni chakula hasa . Mfano cost za mkaa kwenye brooding anayefuga kuku 300 na mwingine 500 cost ni sawa
 
Virid ni dawa ya kutibu maji
V-rid ni dawa ambayo unatumia kutibu maji, vyombo, kupulizia bandani na kwenye maji ya kukanyagia unapokuwa unaingia bandani ili kutowaletea kuku magonjwa walio bandani.

Pia mm uwa natumia JIK kama nimemaliza kuwatoa kuku na ndani ya mda mfupi kama siku nne ninaingiza wengine hapa muhimu kujua JIK usiitumie kuku wakiwa bandani kwani ina makali ila ndani ya siku moja inakuwa imeshafanya kazi yake na kuacha banda likiwa salama , hapa unaweza pulizia v rid kama kukamilishia na dozi inaongezeka au kupungua kulingana na matumizi.
 
Kuhusu dawa hapa wengi hawana uelewa kutokana na kulishwa rumors mfano kuna kuwakinga na magonjwa hasa wiki mbili za mwanzo baada ya hapo dawa unayoweza toa ni ya coccidiosis na vitamini angalau mara mbili kwa wiki ila cha kuzingatia hapa wiki moja kabla ya kwenda sokoni ni kuwapa maji tu ambayo hayana dawa basi
Ooh....sawa sawa🙏🏼🙏🏼....jibu linekaa njema sana. Matumiz ya Antibiotics ( kwa kuku bila kujali wanaumwa ama la n hatari sana.
 
Ongera bana, dah,hawa kuku wameharibu ndoto yangu mwaka huuu hatari sana. Nimerudi kuwa kapuku wakati nilishapiga hatua sana.
Pole sana kiongozi unaweza share nasi hapa pengine tukapata funzo na solution ilikuwaje ukaanguka na tukajifunza zaidi. Maana ufugaji na kilimo ni sayansi inayobadilika kila kukicha
 
Ooh....sawa sawa🙏🏼🙏🏼....jibu linekaa njema sana. Matumiz ya Antibiotics ( kwa kuku bila kujali wanaumwa ama la n hatari sana.
Ni kweli kuna wengine wamevamia ufugaji wanadiliki kutumia hadi dawa za binadamu mm kila batch lazima niache kuku wa matumizi ya nyumbani maana mfugaji kama uwezi kula unachofuga hiyo ni dhambi kubwa sana
 
1. Maji ya kuku ni vyema yatulie kidogo ata siku moja mbele kwan yako na chlorine na uwa inaevaporate na kipindi ambacho utumii dawa ni vyema kama waterguard ipo unaweza kuwa unatibu vimelea hasa wa typhoid na cholera.
2 . Kuhusu chakula bado naendelea na trial lakin matokeo ni mazuri na uwa naselect kuku nawatenga naendelea kuwaangalia kwa ukaribu zaidi na mpaka sasa formula nayotumia ni kuwa na mchanganyiko wa vyakula mfano mashudu,mtama,damu ,pumba n.k ambayo natengeneza kilo 332 na kupeletize hicho chakula alafu naweka na portion ya hizi mifuko ya grower ili kubalance kiwango cha protein . Nafanya hivi kwani chakula lazima ukipime maabara na kwa bongo maabara zipo chache sana lakin in field uwezi kusubili inabidi ujiongeze kwa udadisi zaid.
Tujikite kwenye chakula mtaalamu, tusaidie mdadavuo kwa KG. Yaan jama n pumba kg XX, mashudu kg XX n.k utakua umetusaidia sana.
 
V-rid ni dawa ambayo unatumia kutibu maji, vyombo, kupulizia bandani na kwenye maji ya kukanyagia unapokuwa unaingia bandani ili kutowaletea kuku magonjwa walio bandani.

Pia mm uwa natumia JIK kama nimemaliza kuwatoa kuku na ndani ya mda mfupi kama siku nne ninaingiza wengine hapa muhimu kujua JIK usiitumie kuku wakiwa bandani kwani ina makali ila ndani ya siku moja inakuwa imeshafanya kazi yake na kuacha banda likiwa salama , hapa unaweza pulizia v rid kama kukamilishia na dozi inaongezeka au kupungua kulingana na matumizi.
Ok asante,
Je maji ya kunjwa unawapa tu kutoka bombani? au kuna dawa unaweka kabla ya kuwapa wanywe?
 
Ok asante,
Je maji ya kunjwa unawapa tu kutoka bombani? au kuna dawa unaweka kabla ya kuwapa wanywe?
Maji ya kunywa uwa ya leo mfano yanatumika kesho au keshokutwa nafanya hivi kuepusha muingiliano wa chroline na dawa ya kuku inayopelekea kupunguza ile ufanisi wa dawa au chanjo .
Mfano mwingine kama siku ya chanjo hata kama nina vaccine stabilizer au maziwa ya unga lazima maji niyachemshe ili chanjo iweze kufanya kazi yake vizuri. Maana mistake kidogo lazima ikutoe mchezoni
 
Mchanganuo wa chakula ambacho hadi sasa performance yake imefanya vizuri lakini bado naendelea na trial kwa chotara kilifanya vizuri zaidi siku ya 50 tayari kuku wanakuwa wamechukuliwa wote .
Pumba kilo 300
Mashudu kilo 100
Damu kilo 25
Unga wa sangara kilo 30
Mifupa kilo 5
Chokaa kilo 20
Dcp 3 kilo
Broiler premix kilo 4
Chumvi kilo 2
Lysine 0.5 kilo
Methionine 0.5 kilo
Toxic binder 0.5
Mtama kilo 32
Kwaiyo utachanganya na wakiweke kwenye pellet na kama utakuwa unalisha kuku chotara au kienyeji utaongeza kilo 126 za grower na upande wa broiler utakuwa unatoa mchanganyiko huo wa juu asilimia 20% mfano kuku 300 wa broiler kuanzia siku ya 20 unawapa kilo 30 kwa siku ambayo ni gramu 100 kwa kuku mmoja inamaana mchanganhiko wa pale juu utakuwa kilo 6 na grower kilo 24 na mara nyingi uwa naanza zoezi ili siku ya 18 .
Turudi nyuma kidogo inapofika siku ya 13 kuku inabidi umuanzishie kidogo kidogo mfano starter 75% na grower 25% siku inayofata 50% starter na grower 50% siku inayofata tena 25% starter na 75% grower unaenda hadi siku ya 21 ndo unawapa full growers hii itasaidia kama kuna kuku walio chini ya uzito wa kilo 1.2 nao wapande haraka wawe uniform
 
Back
Top Bottom