Jerry Farms
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 344
- 350
Sawa sawa🙏🏼🙏🏼Mchanganuo wa chakula ambacho hadi sasa performance yake imefanya vizuri lakini bado naendelea na trial kwa chotara kilifanya vizuri zaidi siku ya 50 tayari kuku wanakuwa wamechukuliwa wote .
Pumba kilo 300
Mashudu kilo 100
Damu kilo 25
Unga wa sangara kilo 30
Mifupa kilo 5
Chokaa kilo 20
Dcp 3 kilo
Broiler premix kilo 4
Chumvi kilo 2
Lysine 0.5 kilo
Methionine 0.5 kilo
Toxic binder 0.5
Mtama kilo 32
Kwaiyo utachanganya na wakiweke kwenye pellet na kama utakuwa unalisha kuku chotara au kienyeji utaongeza kilo 126 za grower na upande wa broiler utakuwa unatoa mchanganyiko huo wa juu asilimia 20% mfano kuku 300 wa broiler kuanzia siku ya 20 unawapa kilo 30 kwa siku ambayo ni gramu 100 kwa kuku mmoja inamaana mchanganhiko wa pale juu utakuwa kilo 6 na grower kilo 24 na mara nyingi uwa naanza zoezi ili siku ya 18 .
Turudi nyuma kidogo inapofika siku ya 13 kuku inabidi umuanzishie kidogo kidogo mfano starter 75% na grower 25% siku inayofata 50% starter na grower 50% siku inayofata tena 25% starter na 75% grower unaenda hadi siku ya 21 ndo unawapa full growers hii itasaidia kama kuna kuku walio chini ya uzito wa kilo 1.2 nao wapande haraka wawe uniform