Kuyafikia mafanikio ya ufugaji kwa kuku wa broiler

Lakini pia sijaona antibiotic ( mfano astrisul , fluban ,tylodox na respacare , )vitamini na probiotic, anticoccidiosis
 
Tujuze uzuri wao zaidi kiongozi kwa uzoefu wako
Sijawahi fuga kibiashara ila wanahimili sanaa maginjwa pia soko lake ni zuri kukiko wa kisasa sahizi kijijini kuku wa ten humpati nikuanzia 15,17 kuendelea mjini ndo bei imechangamka hatari tetea 20 mpk 23
 
Lakini pia sijaona antibiotic ( mfano astrisul , fluban ,tylodox na respacare , )vitamini na probiotic, anticoccidiosis
Ndio,hatujaweka gharama za antibiotic na madawa maana kwa wengine magonjwa yanaweza yakaingia na kwa wengine yasiingie,hiyo ni gharama bila madawa,ujenzi,maji na mishahara
 
Sijawahi fuga kibiashara ila wanahimili sanaa maginjwa pia soko lake ni zuri kukiko wa kisasa sahizi kijijini kuku wa ten humpati nikuanzia 15,17 kuendelea mjini ndo bei imechangamka hatari tetea 20 mpk 23
Ni kweli kabisa bei yake ni nzuri sana unaweza ongeza kama una eneo la kufugia ukaanza ufugaji wa kibiasha
 
Pia ni vyema walaji wa nyama hasa ya kuku iwe kienyeji, chotara au broiler kinachofanya kuku aweze kufikia uzito kwa mda mwafaka ni kuhakikisha chakula wanapewa kwa wakati muafaka na cha kuwatosha kila wiki na kuhakikisha unawapima kwenye mnzani kufuga kwa makisio hakuwezi kuleta ufanisi .
 
Baada ya mpambano mkali wa mauzo kuku wetu batch ya pisi 500 umekamilika kwa kubreak even ya kiasi cha shillingi 680, 000 baada ya kuondoa cost zote.
Changamoto
1. Kuku wameenda hadi siku ya 35 ndo wameisha wote
2. Kuku ni wengi sana mtaan kutokana na hali ya hewa kuwa rafiki kwani gharama ni ndogo sana
3. Hali ya soko pia kuwa na mdololo kidogo mnunuzi akilaza kuku maana yake anatakiwa kesho asije hadi kuku waishe.
4. Kukabiliana na wezi hasa wale vijana wa ndoo wanaopenda kunyonyolea hapo bandani uwa baadhi yao wana tabia ya kutaka wanyonyoe kuku alafu ndo uje kuhesabu kuku wengine ubakizwa kwenye maji ambao uwa faida yao last batch kwenye kuku 500 vifo vilikuwa vinne ila mwisho kuku 15 awakuonekana hivyo hasara ikala kwangu. Baada ya kubaini na kubanwa mchezo wamenunua mara moja tu na hawakuludi tena .
N.B kiujumla ufugaji wa kuku kila siku unakuja na changamoto zake ambapo kama ukiwa hauko makini utajikuta unabaki na mabanda na mtaji kupotea kabisa
 
Wakuu nina mpango wa kuanzisha mradi wa kuku 10000 wa mayai pamoja na nyama Dsm.Naomba mtu mwenye uzoefu wa kutosha katika ufugaji tuwasiliane anisaidie kujifunza zaidi au kama yuko interested tuangalie namna tunaweza kufanya kazi pamoja.
 
Wakuu nina mpango wa kuanzisha mradi wa kuku 10000 wa mayai pamoja na nyama Dsm.Naomba mtu mwenye uzoefu wa kutosha katika ufugaji tuwasiliane anisaidie kujifunza zaidi au kama yuko interested tuangalie namna tunaweza kufanya kazi pamoja.
Kwa uzoefu kidogo nilionao kwa kuku 1000 wa mayai nilitumia ml 11 had mwezi wa sita ambapo uzalishaji ukiwa vizuri kuanzia asilimia 80 wanakuwa na uwezo wa kujilisha wenyewe , hapo ndo unaweza pata picha na hapo banda nilikuwa nalo na baadhi ya vyombo
 
Kumaanisha 6M inatosha kufuga kuku 500 kufikia hatua ya Kutaga?
 
Kumaanisha 6M inatosha kufuga kuku 500 kufikia hatua ya Kutaga?
Yeah unafika kulingana na mkoa uliopo na kufanya trick ifuatayo kununua mahindi ya mwaka mzima , mashudu, hivi vingine uwa bei haibadiliki sana hapo utakuwa umewini kujua ilo ni rahisi kujua mfano kwa siku kuanzia miezi 5 kuku watakula kilo 65 hivyo utaangalia kwenye mchanganyiko wa formula mahindi ni kiasi gani multply kwa mda hadi kufikia bei zitakapokuwa chini kawaida kuanzia mwezi wa 5 hadi wa saba mahindi bei uwa chini
 
Unyama sana Boss,

Je ni kweli kuna utofauti kwenye uzalishaji kati ya Chakula cha Kununua na kutengeneza mwenyewe kupitia Formula?
 
Unyama sana Boss,

Je ni kweli kuna utofauti kwenye uzalishaji kati ya Chakula cha Kununua na kutengeneza mwenyewe kupitia Formula?
Ukipata mzoefu ambaye anafanya kazi ya ufugaji na akakuelekeza vyema kutengeneza chakula , faida utaiona sana maana unaweza kuta ghalama inasimama kwenye shilingi 700 kwa kilo wakati cha dukani inafika 1500 hivyo unaokoa pakubwa sana pia katika ufugaji wa kuku wa mayai mapato yakiwa 100% means asilimia 65 ni cost za vyakula na mengineyo na 35 % ndo revenue kama iko tofauti wanaweza nisahihisha wadau
 
Habari samahani, Mimi ni mfugajii lakini shidaa yangu IPO Kwa hao chotara maana nmejaribu kufuga mara kaza, lakini hakuna output yoyote maana kuku wanakufaa balaa juzi nimetoka kuteketeza kuku 300 wa wiki tanoo sijajuwa shidaa ni nn?Samahani unaweza nisaidia unatumia mbinu Gani ama mfumo wako wa ulishaji na utunzaji mpaka wanatoka👏🏿🙏🏿Natanguliza shukran..
 
Pole sana kiongozi , kwanza nijuze hao kuku unawatoa kampuni zip ? Mbili Unafuata mtiririko wa chanjo ? Tatu magojwa kama typhoid,coccidiosis unatibu kwa wakati ? Nn unazingatia biosecurity kama kupulizia dawa kabla ya kuweka vifaranga bandani, kuzuia wanyama kama panya bandani na kuweka dawa ya kukanyaga kabla ya kuingia eneo walipo kuku kila mara?
 
Mm nachukua interchick, chanjo Nina wapa, maana unakuta hata mwanzoni wiki kama ya pili shida inaanzaa, yaan unakuta hata Hawa kuku ninawaogopaa kabisa na pia kuhusu magonjwaa mm ninafuatilia lakin unakuta hawaponi kabisa yaan, nakuhusu biosecurity natumia D4VERT na kingine changamoto ni kwenye swaLa la chakulaa, maana natumia gharamaa nyingi kwenye kununua chakula cha dukani natamani kuchanganya mwenyw ila formula sahihi ndo kikwazo kikubwaa, samahani kama unaformula sahihi naomba unisaidie kiongozi na pia mfumo wako wa chanjo unawapaje mkuu🙏🏿.Natumai kuanzia upyaa
 

Hawa ni tanbro walikuwa na wiki sita hapa jambo la muhimu ni kuanza mapema hasa wiki ya kwanza wapate sulpha drug + dawa za mafua, wiki ya pili hasa siku ya 9 had 14 uwe umewapa dawa za coccidioss , kuhusu chakula kuna formula nimeandika huko page za nyuma rudi ukaisome na ndo uwa natumia kufikia siku 50 kuku uwa wengi wana uzito wa kilo mbili kaiangalie kwanza angalia na cost zake kwa mahala ulipo kisha kama kuna ambacjo ujaelewa unaweza niandikia inbox
 
Kuku hasa wiki ya tano moja ya changamoto kubwa ni ugonjwa wa typhoid hasa ndo unaweza wamaliza kuku wengi nitakuonyesha dawa ambazo uwa natumia hasa bandan kwa kuku wa broiler na chotara
 

Natumia dawa hii kwa ajili ya typhoid na cholera


Hizo ni kwa ajili ya mafua ina uwa naweka separate kila chombo katika siku nne hadi tano za mwanzo naludia tena wiki ya pili mwishon bas na uwa situmii tena dawa za mafua hadi kuku wanaondoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…