Kuyafunua yaliyofunikwa: Historia ya kweli ya Uyahudi na Wayahudi

Kuyafunua yaliyofunikwa: Historia ya kweli ya Uyahudi na Wayahudi

Inaonekana hauko makini na nilichokiandika, suala baba wa Musa nimeshaligusia humu ndani, soma utaona.

Kuhusu jina la mama yake Musa silijui.

Ama kuuliza suala la Musa alifikaje Misri, unaonyesha ni kwa namna gani humjui Musa.

Musa ni mzaliwa wa Misri, na amekulia katika nyumba ya Firauni.

Pili, ongeza umakini hakuna aliyesema Musa hana uhusiano na Wana wa Israeli, bali tumesema ya kuwa Uyahudi hauna uhusiano na ukoo wa Wana wa Israeli zaidi ya kuchukua jina mdogo wake nabii Yusuf aliyeitwa Yaahudha.

Muandishi wa vitabu vitano mimi simjui, kama unamjua tuambie humu na sisi tumjue.
Nonsense.
Kaa na upumbavu wako, and one thing i know for sure is hakuna unapata na hutakuja kupata chochote zaidi ya depression ukufe ukiwa umelala.
 
Nonsense.
Kaa na upumbavu wako, and one thing i know for sure is hakuna unapata na hutakuja kupata chochote zaidi ya depression ukufe ukiwa umelala.
Nacheka sana, ukahisi tuko maskani nini tunapiga soga mzee ?

Hapa tunaandika elimu kijana.

Nipo ....
 
Nacheka sana, ukahisi tuko maskani nini tunapiga soga mzee ?

Hapa tunaandika elimu kijana.

Nipo ....
Abdoool elimu yako haijawahi isaidia chochote dunia na haitokuja kutokea ikaisaidia.

Biblia inasema hivi imani bila matendo ni mfu! Yani wenzio huko wanakufa wanawahi mabikira 72 wewe upo humu JF unahangaika kutuongosha ahahaha hayo ni matumizi mabaya ya muda hata kama ndiyo kazi yako ni ufala.

Hakuna unachopata hapa narudia HAKUNA unajifurahisha tu mwisho wa siku ule ulale Mr Zurri.
Dunia haiko hivyo unavyodhani unakaza sana akili yako kuaminisha watu ufala pole
 
Poa.

Nipo....
 
Sehemu ya tatu

Kuondoka kwa wana wa Israeli katika ardhi ya Misri ni kwa amri ya Mola wao muumba. Pindi Musa alipofunuliwa na kuambiwa ondoke na watu wake, wakiwemo jeshi lake. Hii ilikuwa usiku.

Wayahudi wanasema katika kitabu chao ya kuwa Wana wa Israeli waliishi katika ardhi ya Misri kwa takribani miaka 430,kadhalika husemwa idadi ya walio ondoka katika ardhi ya misri walikuwa milioni,lakini hili halina ushahidi. Ukiondoa watoto na wanawake, na ukiondowa idadi ya ukoo wa Lawi, wanaume walikuwa 1,600.Kwa ujumla wake idadi yao ilikuwa ni ndogo, kama alivyothibitisha hili Firauni mwenyewe, kwa kusema "...inakuwaje watu wachache hawa watusumbue sisi tulio wengi".

Yale yaliyowakuta Wana wa Israeli baada ya kuondoka katika ardhi ya Misri

Yaliwatokea au kuwakuta mambo mengi sana Wana wa Israeli baada ya kuondoka kwao katika ardhi ya Misri, miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo :

1.Ombi lao kwa Musa awatafutie Mungu wa Sanamu mbali na Mola wao aliye waumba.

Hili lilitokea baada ya wao kufika katika ardhi nyingine wakitokea Misri, huko ugenini wakawakuta watu wanao abudu masanamu, na wao wakamuomba Musa awafanyie Mungu kama wa wenyeji wao wanao abudu. Ombi hili Musa aliwakatalia na kuwaambia, "....vipi mnataka niwafanyie Mungu kinyume na Mola wetu muumba ?"

Hapana shaka kabisa ombi hili toka kwa Wana wa Israeli lilikuwa baya sana.
 
UTANGULIZI
Masiku yamepita huku nikitamani sana kuandika chochote kuhusu Uyahudi na Wayahudi. Kuandika kuhusu chimbuko lao, kuandika kuhusu uhusiano wao na wana wa Israeli,kuandika kuhusu itikadi zao, kuandika kuhusu madai yao kwa nabii wa Mola muumba Musa mwana wa Imraan mwana wa Quhaata mwana wa Lawi mwana wa Yaqoub mwana wa Is'haak mwana wa Ibrahiim.

Lakini kalamu zimeshanyanyuka na wino umeshakauka na historia iliandikwa kitambo sana na wakubwa zetu kwa ubora, wakubwa zetu kwa maarifa na wakubwa zetu kwa umri, na nachokifanya mimi ni kurejea kwao na wala sitaandika jipya ambalo wao hawakuliandika,yaani kwa ufupi sitazua.

Maneno nitakayo yahudhurisha kwenu katika mfululizo wa anuani hii "KUYAFUNUA YALIYO FUNIKWA" ni natija au zao la utafiti wangu wa muda mrefu juu ya historia ya watu hawa. Lakini marejeo yangu hasa hasa yamemili katika vitabu viwili, ambavyo nitavitaja mwishoni mwa mada hii, yaani nikiwa nahitimisha somo hili.

Nini maana ya Uyahudi?
Katika kudurusu tamko hili la "Uyahudi" nitapita katika mapito mawili tofauti, pito la kilugha na pito la kiistilahi.

Maana ya Uyahudi kilugha
Wametofautiana wanazuoni juu ya tamko hili, wapo wanaosema tamko hili limetokana na lugha ya kiarabu katika tamko "al Huud" lenye maana ya toba (kutubia) na kurejea katika utiifu (kutokana na maovu aliyo yafanya mtu).

Wengine wakakataa na kusema hakika tamko hili si lenye asili ya Kiarabu, bali limetokana na mmoja wa watu kutoka katika ukoo (uzao) wa wana wa Israeli naye si mwingine bali ni "YAHUUDHA" (Huyu tutamuelezea kwa undani huko mbeleni) au tamko "Uyahuud/Yahuud" limetokana na ile dola iliyo anzishwa kusini mwa nchi ya Palestina baada kupita nabii Suleyman na hii ndiyo kauli yenye nguvu.

Maana ya Uyahudi kiistilahi
Uyahudi kiistilahi maana yake ni wale watu wanao dai ya kuwa wana mfata nabii Musa.

Sehemu ya pili post #28

Sehemu ya tatu post #113

Wenye tafsiri sahihi ya neno Uyahudi ni Waisrael

Tafsiri nyinginezo ikiwemo hii yakwako ni Uongo Wenye lengo la kujifariji

Musilamu hawezi Kuwa Myahudi hata Siku moja labda aamue kubadili Dini yake
 
Safi kabisa, je kila myahudi ni wa ukoo wa Israeli ?

JIBU: Ndio kila MYAHUDI ni sehemu ya Muendelezo wa Uzao wa YAKOBO(ISRAEL), na hii ni kwasababu Mtoto Mmoja wapo wa YAKOBO Aliitwa YUDA na Hii ni kwa Mujibu wa TALMUD na BIBLIA......Ila Wayahudi wa Dunia ya Leo inawezekana wasiwe 100% kinasaba kutokana na Muingiliano wa watu wa mataifa mengine walipotawanyika.

Je kuna sehemu yoyote inayo sema ya kuwa Musa alitumwa kwa Wayahudi au Musa alitumwa kwa Wana Wa Israeli ?

JIBU: MUSA hakutumwa kwa WAYAHUDI PEKEE, Bali Alitumwa kwa WANA WA ISRAELI wote na WAYAHUDI Wakiwepo Pale Utumwani Misri....Mkuu huwezi Tenganisha WAYAHUDI na WANA WA ISRAELI Maana Wote ni Sehemu ya UZAO wa YAKOBO.

Bila shaka haya umeyatoa katika Biblia na si katika vitabu vya Wayahudi, sasa ni kipi kinachokujulisha haya yanawakusudia Wayahudi na si Wana wa Israeli ?

JIBU: WAYAHUDI Wanatumia vitabu Viwili Boss
-Cha kwanza BIBLIA YA KIEBRANIA( Wakristo wanaiita AGANO LA KALE)
-Cha pili ni TALMUD

Ugonjwa wako Mkubwa Boss Unafikili WAYAHUDI ni TOFAUTI na WANA WA ISRAELI kitu ambacho si sahihi kama nlivoeleza hapo awali.
Hapa

Myahudi ni Mwana wa Israeli na sio kila Muisraeli ni Myahudi
Kumbuka kaka Reubeni, simeoni, lawi, zabuloni,isakari, Dani, Gadi,Asheri, Naftali, Yusufu, Benyamini,

Yuda .....Myahudi...au Yahudi ...ndie aliyebarikiwa sana kuliko ndugu zake wote

Kwahiyo sio kila Muisraeli ni Yahudi au Myahudi ila kila Yahudi ni Muisraeli kwa kuwa anatoka katika chimboku la Mzee Yakubu
 
Inaonekana hauko makini na nilichokiandika, suala baba wa Musa nimeshaligusia humu ndani, soma utaona.

Kuhusu jina la mama yake Musa silijui.

Ama kuuliza suala la Musa alifikaje Misri, unaonyesha ni kwa namna gani humjui Musa.

Musa ni mzaliwa wa Misri, na amekulia katika nyumba ya Firauni.

Pili, ongeza umakini hakuna aliyesema Musa hana uhusiano na Wana wa Israeli, bali tumesema ya kuwa Uyahudi hauna uhusiano na ukoo wa Wana wa Israeli zaidi ya kuchukua jina mdogo wake nabii Yusuf aliyeitwa Yaahudha.

Muandishi wa vitabu vitano mimi simjui, kama unamjua tuambie humu na sisi tumjue.
Masahihisho

Yuda ni mtoto wa nne wakuzaliwa kwa mzee Yakubu au Israel na Yusufu ni mtoto wa kumi na moja wakuzaliwa kwa Mzee Israel

Nakatika kutoa mibaraka ya Mwisho

Mzee Israel alimbariki sana Yuda kuliko ndugu zake wote

Mfano mtoto wa kwanza wa Mzee Israel Reubeni alilaaniwa na Baba yake kwa sababu alitembea na mke mmoja wapo wa Baba yake sio mama zao ambao walikuwa mtu na Dada yake
Hapa kumbuka wale mama zao walizaa mmoja watoto wanne ambao ni Reubeni ,simeoni, lawi ,na Yuda na mdogo mtu akazaa wawili tuu Yusufu na Benjamini

Waliobaki sita walizaliwa na wajakazi wao hao Mama zao ambao wapo sita nao

....simeoni na lawi walilaaniwa na Baba yao kwasababu wao walimua mtu wamataifa ambaye alikuwa mtoto wa mfalme alimbaka Dada yao wao walikuwa wapiganaji wazuri sana

...Yuda yeye alibarikiwa na aliambiwa fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda
Ni hapa sasa unapokuja kuona mibaraka ya Yuda kutoka kwa Mzee wao Israel ilikuwa mikubwa sana na ndio maana yeye Yuda aliwameza wengine mpaka leo
 
Hapa

Myahudi ni Mwana wa Israeli na sio kila Muisraeli ni Myahudi
Kumbuka kaka Reubeni, simeoni, lawi, zabuloni,isakari, Dani, Gadi,Asheri, Naftali, Yusufu, Benyamini,

Yuda .....Myahudi...au Yahudi ...ndie aliyebarikiwa sana kuliko ndugu zake wote

Kwahiyo sio kila Muisraeli ni Yahudi au Myahudi ila kila Yahudi ni Muisraeli kwa kuwa anatoka katika chimboku la Mzee Yakubu
Aliyebarikiwa sana ni nabii Yusuf na hakuna mwingine zaidi yake.
 
Mzee Israel alimbariki sana Yuda kuliko ndugu zake wote
Hiki ni kosa la kiitikadi hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kumbariki mwannadamu mwingine, usahihi ni kuwa wanadamu tunaweza kuwapenda sana wafu fulani kuzidi wengine.

Aliyependea sana na mzee Yaqoub ni nabii Yusuf mpaka ndugu zake wakawa wanamuonea wivu na hafimaye wakamfanyia vitimbi vya kumtumbiza kisimani.
 
Aliyebarikiwa sana ni nabii Yusuf na hakuna mwingine zaidi yake.
Hiyo niyakwako mimi kwenye kusoma kwangu Yuda ndio mtoto wa nne wa uzao wa Mzee Wetu Yakubu au Israel na alipokuwa na atoa mibaraka ya mwisho ukisoma utagundua Yuda alibarikiwa sana kuliko wote na Mzee wake
 
Hiki ni kosa la kiitikadi hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kumbariki mwannadamu mwingine, usahihi ni kuwa wanadamu tunaweza kuwapenda sana wafu fulani kuzidi wengine.

Aliyependea sana na mzee Yaqoub ni nabii Yusuf mpaka ndugu zake wakawa wanamuonea wivu na hafimaye wakamfanyia vitimbi vya kumtumbiza kisimani.
Acha kujifanya wewe unajua zaidi kuliko wengine

Yusufu ndio mtoto kipenzi wa Mzee Yakubu ila kwenye mibaraka alipewa mikubwa sana Yuda
 
Back
Top Bottom