Kuzaa mapema ni kujiongezea majukumu yasiyokuwa ya lazima

Kuzaa mapema ni kujiongezea majukumu yasiyokuwa ya lazima

Wewe unamjua mtoto mkubwa wa P funk unamjua mtoto wa lowasa, unamjua mtoto wa amani karume yule shangazi, unamjua mtoto Gardner, unamjua mtoto mkubwa wa ruge, unamjua mtoto mkubwa wa dudu baya wewe kuza before 26 kuna raha yake😬lakini sishauri
Inategemea familia yako, kama pangu pakavu at least 40+, tengeneza maisha kwanza, lakini kama kwenu wako vizuri at least 30+ wa kiume maana una support nyuma yako, wa kike at least 25+
 
Kila jambo na wakati wake, lkn tunatakiwa kufanya maamuz sahihi kwa wakati uliyo sahihi.

Zaid sana kila jambo lina hasara na faida zake, unachotakiwa kufanya ni kupima katika mizani je hasara na faida kipi kimezidi! Kisha ufanye uamuzi uliyo sahihi.
 
40+ mtoto yuppo form one wewe upo 60+ 😀 hizo nguvu za kutafuta ada unatolea wapi? Hapo bado chuo, apate kazi nk. Pata watoto ukiwa bado kijana na una nguvu za kupambania familia yako
 
Unakuta kijana amezaa akiwa na umri mdogo, na kuanza kubeba majukumu mazito ndani ya umri mdogo, ata maisha anakuwa hajayafurahia.

Mbaya zaidi anazaa watoto wengi, inayopelekea katika maisha yake yote ya ujanani mpaka uzeeni anaishi kwa kuteseka, kwa kugharamia familia kwenye mahitaji na elimu.

Ukitaka kushuhudia hili, mtazame mwenzako au ata jirani yako hapo mtaani, hawana furaha kabisa, wote wanawaza mwezi januari watavukaje.

Ile ya kusema kila mtoto anakuja na bahati yake hiyo haipo siku hizi, we zaa angalau ukiwa na miaka 40+, ndio maana wenzetu nje wanazaa watoto 2 au 1.​
Kuzaa mapema wala sio shida , kikubwa uwe umejipanga namna ya kuhudumia hao watoto basi...izo raha za dunia sio lazima ziwe anasa tu, ata watoto wana raha yake, kuchelewa kuzaa nikujibebesha majukumu muda wa kupumzika, mfano unapata mtoto wakwanza una miaka 40 inamaana mpaka uyo mtoto anafika mda wa kawaida wa kujiajiri au kujiajiriwa wewe ushamaliza muda wa utumishi mahala ulipo ajiriwa, yani umeshafikisha 60+ unaishi kwa pension kama hukuwa na shughuli nyingine sasa wafikirie hao wanaofata baada ya huyo wakwanza uliomzaa na 40+ utajikuta muda wa kupunguza majukumu na kula matunda ya wanao wewe bado unahaangaika na ada za shule na majukumu mengine. Kama sio sababu za kiafya zaa mapema watoto wanakuja na ridhiki zao na unaweza ukaenjoy anasa zako wakiwepo na kuwakuza wote ukiwapa mahitaji yao muhimu na kikubwa zaidi utashuhudia na wajukuu zako ukijaliwa umri mrefu.
 
Uzae kwa fujo kwa masirahi ya nani??? Unanufaika nini?? Zaa watu ambao unaweza kumudu mahitaji yao na kuwamonitor makuzi yao, malezi yao, afya yao, elimu, talent n.k. Africa tunafanya mambo ya Msingi kimasihara sana
Neno kipato kwenye comment yangu umeliona ndugu yangu, au umetishwa kuzaa kwa fujo. Nimezingatia kipato, na kuzaa pia. Aliye na kipato na amewasomesha wote, na kumiliki mali ya kutosha, unampangiaje kuzaa. Umaskini wako isiwe zuio kwa wenye mali na lundo la watoto. Maskini asizae na tajiri azae. Uzazi wa mpango, vita, magonjwa ya kutengenezwa ni mkakati wa kupunguza idadi ya watu duniani na Africa hasa.
 
Kwa mwanaume angalau 35 hapo amezaa hasa Kwa mazingira ya Africa na mwanamke 25 awe amezaa na akifika 30 awe kamalizana na issue za kuzaa .

Kuhusu Maisha ni kujipanga zaidi unaweza usiwe hata na mtoto Ila bado ukashindwa kutoboa kabisa .


Ila yote haya uchumi ndo utaamua zaidi .
 
Back
Top Bottom