Mnaongea mambo hamjui! Kuzaa napo ni ku invest! Hakuna binadamu anafanya kitu bila faida. Hata ukiwa na fedha kiasi gani, bila kuwa na mtu wa kukusimamia hususan pale ambapo huna uwezo wa kimwili au akili, utapata shida sana kutokana na utapeli wetu wa Africa. Hivyo kuwa na mtu wa damu yako hasa wakati wa shida na mateso ni muhimu. Mtu baki ni mtu baki.
Tunazaa na kuwatunza ili watufae baadaye. Si kuzaa kwa ajili ya umma.
Aidha sisi tulivyokuwa Watoto, wazazi wetu waliuza assets zao ili tukaende shule. Baada ya kumaliza masomo, sisi ndiyo tulibadilisha maisha yao ya dhiki. Tukawajengea hadi maghorofa Vijijini. Siku hizi vijiji vingi vimekuwa na maendeleo kutokana na watoto waliorudi kulipa Fadhila kwa wazazi wao.