Kuzaliwa na kifo ndiyo ukweli pekee katika maisha! Mengine yote afanyayo binadamu katika maisha yake ni maigizo

Kuzaliwa na kifo ndiyo ukweli pekee katika maisha! Mengine yote afanyayo binadamu katika maisha yake ni maigizo

Hiyo ya Yesu inaweza kuwa ni maigizo extreme kuliko scenario zote ulizozielezea hapo.

Imagine eti huyo ndio alikuwa mtoto pendwa wa Mungu, still akatumwa aje kupigwa kipigo cha aibu mpaka kifo.

Guys tuelewane, huyo ni mtoto pendwa hakuna kama yeye lakini cheki kilichomkuta.

Na hapo hakuwa na dhambi.

Je hiyo inatupa tahadhari gani kwa sisi watoto wengine ambao sio pendwa kama alivyokuwa Yesu?

Plus na haya masharti aliyotuwekea ya mfumo wa tuishi na kuita dhambi kila kitu ambacho kitakuwa ni kinyume na maagizo yake, hivi hamuoni kwamba sometimes ipo haja ya kuzikwa na fire extinguisher ili kupambana na ile kitu ya huko jehanam?
Kwani wewe ukipanda mbegu shambani huwa huipendi kuila! Si unapanda ili iote izae nyingi?
Mungu alimleta mwanae afanyike kuwa mbegu za kuzaa wema kwa wanadamu!
Alikuja kuigiza maisha kama mwanadamu ili apitie machungu yote! Na pale aliposhinda aliwatangazia wote wanaomwamini yeye nao watashinda!
 
Kwani wewe ukipanda mbegu shambani huwa huipendi kuila! Si unapanda ili iote izae nyingi?
Mungu alimleta mwanae afanyike kuwa mbegu za kuzaa wema kwa wanadamu!
Alikuja kuigiza maisha kama mwanadamu ili apitie machungu yote! Na pale aliposhinda aliwatangazia wote wanaomwamini yeye nao watashinda!
Kwa hiyo stori za Mungu na Yesu unaziona real?
 
Ni kama kutoa haja tumboni ndugu ..ndiyo maana mtu anaweza zaa hata mara 10! Lakini haweza kiumbe hikohiko mara 10, lazima azae tofauti maana hiko kinachozaliwa ndicho halisi! Lakini mzaaji anaigiza tu
Igizo si unaweza rudia hata mara mia?
 
Hata ukiyakubali haibadilishi unachoigiza ni kama ndege tu walivyo kutwa wanazurula jioni wanarudi kwenye viota! Hata wewe binadamu ndivyo ulivyo huna ramani ya kudumu upo unaigiza tu kuishi kadri ya mazingira ulipo

Kwa hiyo hata wewe unavyoandika hapa unafanya masihala au unaigiza tu??
 
Kwenye haya maigizo nahisi mimi ni kanumba kwenye scene ya umaskini, maana naipatia mnoo
 
Inategemea igizo lako liko upande gan: likiwa kwenye utajiri hata ukiuza mawe yananunuliwa;

Zingatia hata Yesu alikuja duniani kuigiza kama mwanadam ili kupitia machungu ya kuishi kama binadam na kushinda majaribu
Wewe pengine una tatizo la kisaikolojia. Maisha yamekupiga badala ya kupigana, unatafuta njia za kijiliwaza.
 
Vitu pekee ambavyo ni ukweli ni viwili tu kwa mwanadam (kuzaliwa na kufa)
Maisha mengine yote ya mwanadamu ni maigizo!

Chochote afanyacho binadam huwa ni kama scene tu havina ukweli wowote kiuhalisia!

Kwa mfano: Ukiangalia watoto wanavyochezea makopo au wanavyoigiza kibaba baba au kimamamama au chochote ambacho hakina nadharia yoyote zaidi ya kusadikika na kufikirika!

Ndivyo ilivyo hata kwa wakubwa chochote ufanyacho hakina uhalisia wowote bali ni vitu vya kufikirika tu na kusukuma siku ziende.
  • Wengi wanaigiza kuishi kama wanandoa lakini kiuhalisia ni maadui wa baadae (maigizo)
  • Wengi wanaigiza matajiri leo lakini ni masikini wa baadae (maigizo)
  • Wengi wanaigiza maskini leo lakini baadae ni matajiri (maigizo)
  • Wapo walioteuliwa vitengo ili waje kutenguliwa baadae (maigizo)
  • Wapo walioshiba jana lakini wameamka na njaa kali mno (maigizo)
Kila afanyacho binadamu ni maigizo! Inategemea umepangwa kucheza Scene gani katika igizo lako la maisha!

Chochote ufanyacho katika maisha ya binadamu ni Maigizo tu kwahiyo msiwe siliazi sana kwenye hayo maisha yenu maana hata ukikaza haibadili chochote kwenye maigizo yako!
Mzee amka ukatafute hela acha kuota. Yaan Elon musk anaigiza? Hauko serious aisee.
 
Maigizo pia haya
 

Attachments

  • 6d9e2b3003b1454e87b29692ca63fa4a.jpg
    6d9e2b3003b1454e87b29692ca63fa4a.jpg
    39.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom