Huruma ya Mungu haipimiki maana ni kubwa sana LAKINI hasira ya Mungu haizuiwi na mwanadamu awaye yeyote.
Mungu huwapa wanadamu nafasi ya kujirudi, na kurudia utu wao. Viongozi wa CCM walipewa nafasi hiyo, lakini hawakubadilika kwa lolote. Wakatenda kwa ukaidi, dhuluma, uonevu na upendeleo.
Mungu ameendelea kutoa nafasi kwa hawa walevi wa madaraka. Lakini kiburi kikiendelea, Tanzania inaweza kuendelea kuongozwa na Makamu wa Rais kila baada ya uchaguzi.
Enendeni katika haki. Msipendelee wala kuonea hata mkamfanya Mungu wa haki akwa kinyume chenu.
Watu walimwomba sana Mungu wakati wa awamu ya 5. Maombi yalikuwa ya aina mbalimbali, lakini mengine ilikuwa ya kumwomba Mungu awaondolee mtawala mbaya. Kwa namna gani, hakuna aliyefikiria, maombi ilikuwa kuwaondolea mtawala mbaya. Maombi yao, kwa wakati ufaao, Mungu akatekeleza, tena kwa namna ambayo wengi hawakutarajia. Lakini ni nani mwenye kuhoji hekima ya Mungu?
Watu wa Mungu, wakati wakimshukuru Mungu kwakusikiliza sala zao, japo Mungu kawajibu maombi yao kwa mkono wenye nguvu, wa kuogofya, wasichoke kuendelea kumwomba awainulie kiongozi mwenye hekima, kiongozi mwenye upendo, kiongozi msikivu tena asiye na upendeleo, na pale kiongozi akikengeuka kwa kiburi na jeuri, awanusuru watu wake kwa kumwondoa kwa namna yoyote iwayo.