Kuna mambo unaweza kuhukumu kutokana na rekodi ya mtu, kuna mambo unaweza kusema huyu hapa sitegemei aheshimu katiba na demokrasia, kwa sababu kashasema anataka kuua upinzani by 2020.
Hapo una ushahidi wa maneno ya huyo mtu, ukimhukumu unamhukumu kwa fact.
Halafu kuna mambo ya kumhukumu mtu kwa paranoia tu, mtu kashasema mara kadhaa hataongeza muda, unakuwa na inferiority complex tu kuona ataongeza muda.
Kwa sasa, based on facts, kumhukumu Magufuli kwenye hili la kuongeza muda ni paranoia tu.
Na wapinzani wanaoshikia bango hili wanajionesha hawajakoma kisiasa kuchambua mbivu ni zipi na mbichi ni zipi.
Wewe Magufuli ana makosa kedekede ambayo kashayafanya, watu wote wenye akili na wanaoheshimu mantiki wanajua, hayana mjadala.
Unayaacha yote hayo, unaenda kuwa obsessed na makosa ambayo hajayafanya bado?