Nadhani hapa hata watu wa sheria haswa upande huu wa mpira, watusaidie kua mtu ameingia mkataba wa miaka 3, mwanzon kulingana thamani yake na performance yake alikua analipwa kiasi fulani ambacho si kikubwa, sasa kiwango kimepanda labda baada ya mwaka mmoja na nusu, kwaio kwenye mkataba umebaki mwaka na nusu umalizike, je mkataba hauwezi kuboreshwa kulingana na thamani ya klabu inavyopanda pamoja na kiwango cha mchezaji? Je ni sawa kusubiri hadi mwezi ndio uanze kujadili mkataba wake? Je hio si inatoa fursa hata kwa timu pinzani kutumia fursa hio kumchukua? Je klabu kama inasubiri hadi mwezi unabaki ina nia kweli ya kumtumia ?
Tshaba hana desturi ya kujiona mkubwa zaidi ya klabu, hana desturi ya ujeuri, mpira ni pesa na ni biashara kubwa sana kwa sasa na wachezaji wanapata pesa nyingi angalia ulaya huko, anachofanya ni sawa, kwenda kule ambapo anaona pesa wanayoitoa inaendana na thamani yake na kiwango chake, jasho lake, commitment yake kwa timu, simba tulikua na nafas kubwa na muda wa kutosha kumuongezea mkataba na kuuboresha kwaio viongozi wasianze kumrushia mawe na kumtuhumu kua anataka kuizidi klabu kitu ambacho sio sawa.