Wewe sio shabiki bali ni mpenzi wa Yanga, na mimi kama mpenzi wa Simba kwakweli tumesikitshwa kua Tshaba analipwa kamilioni tu kwa mwezi, dah, yani tume betray his love and trust kwa timu anayoipenda na aliyojitolea kuichezea kwa moyo wote, kwakweli aende tu panapomstahili aisee.
Swali fikirishi, ina mana sisi wachezaji watanzania kwenye timu zetu hizi tunadharaulika kiasi hiki, kwamba hatuna hadhi ya kulipwa zaidi ya m15 kwa mwezi sababu tu ni wazawa?
Pia aishi manula naona ameshasoma upepo naye dau lililokuja ni kubwa, na madau yalivyoanza kuja kwa kasi ndio viongozi kuanza kuhaha kuitisha mikutano na wachezaji kujadili mikataba mipya.
Tujifunze hata kwa wenzetu, wachezaji muhimu mikataba unakuta imebakiza mwaka au hata miaka 2, mabosi wameanza kujadili upya mkataba wa mchezaji husika, huku kwetu mchezaji muhimu anabakisha mwezi ndio mnaanza kukimbiakimbia.