Kwa aliyoyasema Rais Samia kuhusu ATCL, ni vyema Mkurugenzi akajiuzulu mapema kabla hajatumbuliwa

Inasikitisha mno!
 
ATCL hawamiliki ndege na hawahusiki na ununuzi wa ndege. ATCL ni kama wasimamizi wa biashara ya usafiri wa anga kwa niaba ya serikali. Mmiliki wa ndege za ATCL ni Tanzania Government Flight Agency (TGFA). Na taratibu za manunuzi zinaanzia wizarani kwa sababu pesa ya ununuzi haijazalishwa kutoka kwenye biashara zaidi ya bajeti kuu ya seriali. Sasa huyo Mkurugenzi wa ATCL anahusikaje hapo????
 
Hakika rais wetu anatakiwa asaidiwe pakubwa na kwa haraka, ikiwemo kumwombea Mungu ampe ujasiri, akili na hekima itokayo juu. Kakwama na kuishia kulalamika na kutukana: "...stupid..., ...pumbavu..."!

Nani ataogopa kuendelea kuiba na kula fedha za umma kwa kulalamikiwa na kutukanwa tu bila kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria?!
 
Nchi yetu bhana utadhani tunaigiza tunasubiri ripoti kila mwaka na sijui kama zinafanyiwa kazi na kwa nini iwe report kwa nini kusiwepo na kitengo cha kuzuia hayo madudu? Kama Hawks Team SA na kwingineko ina maana tunabariki wizi ili tuotolee ripoti..
 
Mama asiishie halo, mbona taasisi nyingi wanafanya upuuzi na hachukui hatua, mtanzania bila kumkazia atavuna mabua, watu wanachezea Kodi na mother ka mute, akiamua kukanyaga mafuta asichague.
 
a

anayenunua ni nani? maana ATCL wao wanazikodi tu, hakuna haja ya kujiuzulu
Nadhani mtoa mada hamjui mmiliki wa ndege... ATCL anakodi ....kuna ile team ya wanasheria wa hii mikataba ndio wamemgutusha bi tozo. Ungeniambia Mwigulu na katibu mkuu wake, au wale wa Ujenzi mawasiliano na uchukuzi ningekuelewa
 
Sijawahi kumsikia mama S akitukana hivyo embu tuone kama matusi yake yanaambatana na vitendo.

Mama Samia, alichukia sana sanaaa, kiukweli inaudhi mnoo mnoo, yaani watu wanaiba sanaa, Mkurugenzi ATCL lazima aondoke, pia Mkurugenzi TGFA lazima aondoke, kumbuka hizi ndege zikitaka kununuliwa TGFA lazima abariki maombi ya ATCL, hivyo wakurugenzi wote wawili lazima waondoke haraka na kuachia ngazi zao, yaani wajifukuzishe kazi wao wenyewe au Mh. Rais awafukuze kwa barua haraka sana kwa kuwatengua kwa barua haraka ya Ikulu.

Mh. Rais kachukia sana, naamini kati ya leo au ugeni huu wa Makamu wa Rais wa Marekani ukipita, atachagua wakurugenzi wapya ATCL na TGFA, ndio maana Mh. Rais alisema watupishe, naamini ni watu wengi kidogo, hadi ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali nayo inahusika kabisa. Ngoja tuone siku chache zijazo
 
Nani analipa hizo ukute wakala wa ndege sio ATCL
 
Mwache adhani uraisi ni kama kunyonyesha mtoto.AJIKAZE AAMUE.
Kwa ulichokiandika ni kama vile hukunyonya vizuri au huna shukrani kwa aliyekunyonyesha. Kwa taarifa yako binadamu anatengenezwa ktk siku 1,000. Chakula kikuu kwa miezi sita ni ziwa tamu la mama. #Ufikirie kabla ya kuandika. Uwe na heshima basi.🙏🙏🙏
 
Manunuzi na uendeshaji unafanywa chini ya Waziri/KM na board inamaana hao wote wanabaki kufanya nini?
 

Inaonekana kama ili uongoze hii nchi kwa mafanikio ni lazima uwaone watendaji wote wa serikali kama Ng'ombe au Punda. Uwapeleke peleke mpaka waombe kuacha kazi.

Kila mtu anayepata nafasi kidogo anataka kuiba.
Ndio kazi aliyokuwa amejipa Magufuli kunyoosha vichwa ngumu wote Serikalini. Matokeo yake alijijengea maadui ambao mpaka leo hawataki kusikia jina lake. Tutamkumbuka kama Rais pekee "Jiwe" asiyetishwa na kutishika.
 
Atcl haitoweza kukaa na kupata faida kirahisi kwanza inahitaji serikali iinyanyue ndio ianza kupata faida.

Airlines nyingi duniani zimeanguka lakini serikali ina take covers sababu ya impact ya nchi kuwa na airline.
 
Stupid na pumbavu sio tusi!.
P
Ni tabia za watu, mkuu hivi chama chenu kina nia thabiti ya kumkomboa masikini toka kwenye lindi la umaaikini? Mnamuwekea TOZO huku mnaiba billions, na nilivyoona mama kashindwa kumtaja kwa jina muhusika hata mmoja nikajua ndio imetoka hiyo
 
ATCL hawahusiki na mchakato wa manunuzi...wanakabidhiwa ndege zilizonunuliwa na Serikali kupitia wakala wa ndege za Serikali na Wizara yake.
 
Waafrika huwa hatuna aibu wala hiyo hofu ya kujiuzulu haipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…