Kwa aliyoyasema Rais Samia kuhusu ATCL, ni vyema Mkurugenzi akajiuzulu mapema kabla hajatumbuliwa

Sijui waliompa ph wanajionaje maana sioni content ya ph kabisa
 
Muombeee pekee yako hivi unahabari kila mradi wa alioucha magufuli umekuwa na variation za maana maana wanamjua hata wakifanya hivyo amna wa kuwagusa
 
Afanye kazi, usinifundishe malezi yule anaongoza nchi ana madaraka afanye kazi.usiniletee siasa hapa.
 
Tena kasema stupid mara ya kwanza then mara ya pili kasema Pumbavu
Anasema mawaziri wasaidie kwenye kupambana na haya, hapo ndio nilichoka. Anaona mawaziri ni wasafi sana?
 
SIO KUJIUZULU NO, NI VYEMA WAKAZIRUDISHA FEDHA ZA ZIADA MAPEMA SANA, NADHANI NDIO HATUA SAHIHI HII KUJIUZULU TU HUWA HAITOSHI NA HAINA MAANA YOYOTE.
 
Kwa Tz hii kujiuzulu ni ngumu mtu anatetea ugali wake
 
Naona wezi wa hiyo pesa saa hizi kama alikuwa anakunywa vidonge viwili vya pressure leo anakunywa vinne,wizi sio mzuri....
 
Ndio kazi aliyokuwa amejipa Magufuli kunyoosha vichwa ngumu wote Serikalini. Matokeo yake alijijengea maadui ambao mpaka leo hawataki kusikia jina lake. Tutamkumbuka kama Rais pekee "Jiwe" asiyetishwa na kutishika.
Huyo unayetaka kumpa sifa hapa muache tu apumzike.

Katika kipindi chake CAG aliripoti upotevu wa 1.5 trillion, na makando kando mengine mengi. Baada ya hapo alianza harakati za kupambana na kumnyanyasa CAG mzalendo kabisa.

Angekuwa mwema hivyo huyo JPM angempenda sana CAG Assad. Angekuwa na nia unayotaka tuiamini hapa huyo JPM, asingehakikisha nchi inakuwa na bunge la chama kimoja, bunge kibogoyo na dhaifu.
 
Mkuu mbona sifa aliishajizolea tu kabla ya umauti kumkuta? Punguza makasiriko bro, hayupo ndio lakini alama kaacha nyingi tu zitakazokukera.....Relax!.
 
Ngojeni Atakayewabembeleza
Your browser is not able to display this video.
 
Sisi ATCL. ATCL haiuhusiki na ununuzi wa ndege.

Huyo atakuwa ni Mwigulu na yule wa Wizara ya ujenzi, ndio wanaohusika na manunuzi.

Wewe unafikri hizo Yutong 200 zinazonunuliwa kwa mara moja, pesa yake inapatikana kwa njia gani kama siyo wizi wa namna hii?

Alipoondolewa uwaziri, unajua Singida United ilikuwa kwenye hali gani?
 
Stupid na pumbavu sio tusi!.
P
Siyo tusi kama kweli wewe ni stupid au mpumbavu.

Mtu akikuambia wewe ni jizi wakati hujawahi kuiba chochote, hapo amekutukana. Lakini kama ukiambiwa wewe ni jizi, na kweli ukawa jizi, hujatukanwa, umeelezwa jinsi ulivyo.

Tena Mama angefanya vizuri angeyataja haya mapumbavu stupid kwa majina ili sote tuyajue. Na mitaani yafahamike kwa haya majina yanayoelezea namna yalivyo.

Angefanya tu kama alivyofanya JPM. Yeye alisema wazi kabisa kuwa Kabudi na Mpango ni wapumbavu, na Kabudi aliinuka na kumwinamia kuonesha kukubali kuwa yeye ni mpumbavu.

Hata leo tukimwita Mpumbavu, siyo tusi, maana aliambiwa hivyo, na yeye alikiri.
 
atcl ipunguze wafanyakazi, iongeze miruko, ishushe bei ili ndege zijae
Iwe kama fastjet, kama mabasi yanatoza 58-120,000 iweje ndege isitoze bei angalau 100k kwa mruko ili watu wajae?
Ikipata abiria 2000 kwa siku kutoka Dar, Mbeya, Kilimanjaro kuna ubaya gani
Ambayo ni sawa na bilioni 2 kila siku kwa mwaka ni bilioni 700

Wakitoa gharama hata iwe bilioni 699 bado watabaki na faida hata ya milioni 10
 
Hao watu mpaka sasa kumbe hawajakamatwa na TAKUKURU?
Au hao nao wanasubiri mpaka watumwe na Rais?

Ndio maana nasema kilasiku TAKUKURU nao nijipu
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…