INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

kama we kweli una stock ya kutosha me nahitaji bongo movies za kina shumileta, chiteukae, mzimu wa pesa, mzee wa busara and the like.. weka dau tufanye kazi
Siuzi BONGO MOVIE boss wala hakuna ofisi yangu yenye BONGO MOVIE ukitaka hasara Bila kutegemea basi jipendekeze kwenye Bongo Movies.

Na uza Movie hizo nilizotaja mkuu za kizungu kutafsiriwa na za mataifa mengine sio BONGO MOVIE.
 
Hiyo 20TB inagharimu shingapi?
 
Sikubishii, ila nakuhakikishia sina movie ninayokosa.. nina collection mpaka movies za miaka 60 huko, James Bond ninazo toka ya kwanza mpaka no time to die.. naelewa biashara, na wala sikubishii na biashara ni mipango ya mtu na target zake, ndio maana nikasema siwezi kukupangia concern yangu ilikuwa uliposema movies hizi hazipatikaniki mkuu, vinginevyo kila la heri chief na mapambano yaendelee.
 
inategemea na Umenunua wapi au nani anaekuagizia Bidhaa yako ila kwa upande wangu niliponunulia imenigharimu 1.7M mpaka Mzigo unanifikia Nilipo ofisini kwangu,sijigusi kwenda popote Hapo nmelipia kila Kitu.
Ukiniagizia Itachukua siku ngp kufika bongo?
 
Ukiniagizia Itachukua siku ngp kufika bongo?
Mwl.RCT nahisi kuna mteja hapa

pitia hii thread hapa chini nadhani utaona vitu kadhaa vitakavyokusaidia kumwamini huyo nilie mtag hapo mwanzo.


Ukisharidhika na review na shuhuda kadhaa kuhusu kuagiza vitu mbele wasiliana direct na huyo teacher,Atakusaidia.

Sio kwamba mimi siwezi ila kuepuka lawama za hapa na pale nimependa umtumie huyo mwl. maana wana JF kasoro ndogo tu hawachelewi kukuita tapeli/mwizi.

Uzi wangu wa Movie ukapeperuka kama pumba za mpunga,haya kazi ni kwako mkuu Mugah, ukishapata 20TB unipe tenda ya kukujazia yani kufumba na kufumbua utakuta yote nishaigeuza rangi to RED.
 
itoshe tu kusema bwana Movies Store una hela.hongera[emoji3][emoji3]

usiache kutupa ushauri sisi vijana wenye mitaji midogo

nawasilisha
kingkongtz Mimi ni wa kawaida sana wala sina pesa za kushikika kama pesa sema pesa nimewekeza zote kwenye biashara.

Movie Store ni biashara nzuri sana, ukipata pesa baadae usiache fungua hii biashara bwana Kong.

Nipo siku zote na wakati wote kwenye hii thread watakao hitaji ushauri kuhusu hii biashara wote tutakutana humu kwenye comment.

Ukipata hela uje nikupe mzigo wa Kufanyia kazi bwanaaaa...
 
shukran boss ,kuna vitu naendelea kujifunza hapa
 
Biashara ya kurusha movie nimeifanya tangu mwaka 2011 mpaka 2014, baada ya hapo ikanipa connection ya kazi serikalini JPM alipo ingia madarakai msako wa vyeti feki ukaniondoa huko nikarudi kuifanya ndipo nikapata connectio kwenye kampuni ya wahindi , anay way ni story ndefu, naielewa changa moto zake, maswala ya kuliprishwa memory pale inapotafunwa na wadudu, mara computer kubooma, naona kwa sasa imenoka natamani kurudi tena kwenye biashara hii, ila miaka hiyo tulianza kwa ugumu kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…