Transcend ni nzuri kwa external HDD lakini sipendelei External kwasababu nazo zina changamoto zake,sipendi movable disk mimi kwasabbu najua madhara yake.
Ukifanya biashara ya Movie (kwa upande wangu) kutumia hard disk ndogo ndogo ni Loss kwanza Mother Board za mashine ninayotumia inabeba HDD (5) Mashine yenyewe ina port 6 nyuma + 4 mbele, Port za nyuma zote nimezijaza.
Port za kazi n za mbele tu,na HDD ya storage ndogo niliyonayo ni ya 6TB, so ukipga hesabu unaweza ukaona namna ambavyo ningekua nmetumia HDD za 4TB ingenigharimu na ningekosa pakuweka HDD maana mashine ingekua imejaaa.
Hapa ninavyoandika Mwezi ujao mwishoni Naenda pokea 20TB itakua imeshawasili,nataka Ondoa hizi 10TB zote niziweke pembeni nitumie 20TB tu,ifike hatua HDD zote zinakaa ndani ya mashine TU nisiwe na HARD DISK nnje ya Mashine hata 1.
Kwa mtu anaeanza Ni sawa ushauri wako wa HDD ndogo ndogo hizo za 4TB, lakini kadri unavyo expand na ofisi kuwa kubwa utakuja dharau hizo 4TB utaona n potezaji hela TU, Leo hii uniletee HDD ya chini ya 10TB sinunui hata uwe unaiuza bei ndogo kiasi gani.
Maana nitaiwekea nini? Muhimu ni kujua Namna ya Kutunza HDD zako na kuzifanyia monitoring kila wakati. Nina mwaka wa 4 sasa sijawahi kufiwa na HDD wala computer kuzingua,kna vitu ukishavielewa Changamoto za uharibifu unaziondoa kbsa kama sio kuzipunguza.