INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

kama we kweli una stock ya kutosha me nahitaji bongo movies za kina shumileta, chiteukae, mzimu wa pesa, mzee wa busara and the like.. weka dau tufanye kazi
Siuzi BONGO MOVIE boss wala hakuna ofisi yangu yenye BONGO MOVIE ukitaka hasara Bila kutegemea basi jipendekeze kwenye Bongo Movies.

Na uza Movie hizo nilizotaja mkuu za kizungu kutafsiriwa na za mataifa mengine sio BONGO MOVIE.
 
Transcend ni nzuri kwa external HDD lakini sipendelei External kwasababu nazo zina changamoto zake,sipendi movable disk mimi kwasabbu najua madhara yake.

Ukifanya biashara ya Movie (kwa upande wangu) kutumia hard disk ndogo ndogo ni Loss kwanza Mother Board za mashine ninayotumia inabeba HDD (5) Mashine yenyewe ina port 6 nyuma + 4 mbele, Port za nyuma zote nimezijaza.

Port za kazi n za mbele tu,na HDD ya storage ndogo niliyonayo ni ya 6TB, so ukipga hesabu unaweza ukaona namna ambavyo ningekua nmetumia HDD za 4TB ingenigharimu na ningekosa pakuweka HDD maana mashine ingekua imejaaa.

Hapa ninavyoandika Mwezi ujao mwishoni Naenda pokea 20TB itakua imeshawasili,nataka Ondoa hizi 10TB zote niziweke pembeni nitumie 20TB tu,ifike hatua HDD zote zinakaa ndani ya mashine TU nisiwe na HARD DISK nnje ya Mashine hata 1.

Kwa mtu anaeanza Ni sawa ushauri wako wa HDD ndogo ndogo hizo za 4TB, lakini kadri unavyo expand na ofisi kuwa kubwa utakuja dharau hizo 4TB utaona n potezaji hela TU, Leo hii uniletee HDD ya chini ya 10TB sinunui hata uwe unaiuza bei ndogo kiasi gani.

Maana nitaiwekea nini? Muhimu ni kujua Namna ya Kutunza HDD zako na kuzifanyia monitoring kila wakati. Nina mwaka wa 4 sasa sijawahi kufiwa na HDD wala computer kuzingua,kna vitu ukishavielewa Changamoto za uharibifu unaziondoa kbsa kama sio kuzipunguza.
Hiyo 20TB inagharimu shingapi?
 
Kwakua umesema utakuja anza hii biashara,nakusubir ukianza usisahau kurudia kusoma hii comment yako nimekuifadhia hapa.

Hamna site ya movie si ijui,na still kuna movie Sina na bando ninalo,kwanini sina? hili jibu utalipata ukianza fanya hii biashara.
Sikubishii, ila nakuhakikishia sina movie ninayokosa.. nina collection mpaka movies za miaka 60 huko, James Bond ninazo toka ya kwanza mpaka no time to die.. naelewa biashara, na wala sikubishii na biashara ni mipango ya mtu na target zake, ndio maana nikasema siwezi kukupangia concern yangu ilikuwa uliposema movies hizi hazipatikaniki mkuu, vinginevyo kila la heri chief na mapambano yaendelee.
 
inategemea na Umenunua wapi au nani anaekuagizia Bidhaa yako ila kwa upande wangu niliponunulia imenigharimu 1.7M mpaka Mzigo unanifikia Nilipo ofisini kwangu,sijigusi kwenda popote Hapo nmelipia kila Kitu.
Ukiniagizia Itachukua siku ngp kufika bongo?
 
Ukiniagizia Itachukua siku ngp kufika bongo?
Mwl.RCT nahisi kuna mteja hapa

pitia hii thread hapa chini nadhani utaona vitu kadhaa vitakavyokusaidia kumwamini huyo nilie mtag hapo mwanzo.


Ukisharidhika na review na shuhuda kadhaa kuhusu kuagiza vitu mbele wasiliana direct na huyo teacher,Atakusaidia.

Sio kwamba mimi siwezi ila kuepuka lawama za hapa na pale nimependa umtumie huyo mwl. maana wana JF kasoro ndogo tu hawachelewi kukuita tapeli/mwizi.

Uzi wangu wa Movie ukapeperuka kama pumba za mpunga,haya kazi ni kwako mkuu Mugah, ukishapata 20TB unipe tenda ya kukujazia yani kufumba na kufumbua utakuta yote nishaigeuza rangi to RED.
 
itoshe tu kusema bwana Movies Store una hela.hongera[emoji3][emoji3]

usiache kutupa ushauri sisi vijana wenye mitaji midogo

nawasilisha
kingkongtz Mimi ni wa kawaida sana wala sina pesa za kushikika kama pesa sema pesa nimewekeza zote kwenye biashara.

Movie Store ni biashara nzuri sana, ukipata pesa baadae usiache fungua hii biashara bwana Kong.

Nipo siku zote na wakati wote kwenye hii thread watakao hitaji ushauri kuhusu hii biashara wote tutakutana humu kwenye comment.

Ukipata hela uje nikupe mzigo wa Kufanyia kazi bwanaaaa...
 
kingkongtz Mimi ni wa kawaida sana wala sina pesa za kushikika kama pesa sema pesa nimewekeza zote kwenye biashara.

Movie Store ni biashara nzuri sana, ukipata pesa baadae usiache fungua hii biashara bwana Kong.

Nipo siku zote na wakati wote kwenye hii thread watakao hitaji ushauri kuhusu hii biashara wote tutakutana humu kwenye comment.

Ukipata hela uje nikupe mzigo wa Kufanyia kazi bwanaaaa...
shukran boss ,kuna vitu naendelea kujifunza hapa
 
Usijali mkuu halafu ni kwamba usichokijua si kila mtu hupenda kwenda sehemu nzuri na kubwa, hujawahi shuhudia mtu ana hela anaendesha gari zuri lakini hali hotelini yeye ni wa kwa mama ntilie tu?

Si kwamba hana hela ya hotel ila ameshaptia maisha ya chini sana kayazoea na anayaishi hayo maisha hata sasa akiwa na hela (lakini ana pesa) kwahyo mkuu usiogope wewe timiza malengo yako Fungua ofisi yako bila kujali nani katangulia au nani yupo pembeni yako.

Utapata wateja wako na wao watapata wateja wao ujue tu namna ya kufanya biashara, mwisho wa siku utarudi home na pesa na wao watarudi na pesa Wateja hawaishi wapo kila mahali.
Biashara ya kurusha movie nimeifanya tangu mwaka 2011 mpaka 2014, baada ya hapo ikanipa connection ya kazi serikalini JPM alipo ingia madarakai msako wa vyeti feki ukaniondoa huko nikarudi kuifanya ndipo nikapata connectio kwenye kampuni ya wahindi , anay way ni story ndefu, naielewa changa moto zake, maswala ya kuliprishwa memory pale inapotafunwa na wadudu, mara computer kubooma, naona kwa sasa imenoka natamani kurudi tena kwenye biashara hii, ila miaka hiyo tulianza kwa ugumu kweli
 
Back
Top Bottom