Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huwa najiuliza kwann serikali inapinga vikali, na kujisahaulisha kuhusu mabadiliko ya katiba? Sisi watanzania siyo wajinga ni wazembe.
 
Hekima hii imfikie Lukas Mwashambwa na ndugu yake tlaahtlaah.Hapa hapahitaji ushabiki wa vyama!
 
Hakika...

Hivi ndivyo inavyopaswa kufanyika....

Na hawa jamaa (CHADEMA) chini ya uongozi wa Tundu Lissu, wako more than serious na wananchi tunawaelewa vizuri kuliko tunavyowaelewa CCM na Samia wao wanaoukataa ukweli huu unaowakodolea macho...

Kama vyombo vya ulinzi na usalama (JWTZ, POLISI, TISS nk) vitaendelea kusikiliza na kutii maelekezo ya wanasiasa hayawani wa CCM, wasio na hoja kiasi cha kukosa ushawishi kwa wananchi, basi wawe tayari kuua watu wengi sana kuanzia sasa...

Na wakidhani kuwa watalidhibiti vuguvugu hili kwa kuweka political sanctions zenye lengo la kuwafanya CHADEMA wasikutane na wananchi kuwaunga mkono ktk agenda yao ya NO REFORMS, NO ELECTIONS bado napo ni tatizo tu maana sababu ya kisheria na kikatiba kuwazuia wasipinge wanayopinga haipo...!

Suluhu hapa ni hii uliyopendekeza ambayo ndiyo ukweli wa uhalisia wa situation ilivyo....

There's no way, kwamba, kwa hali ilivyo tunaweza kukwepa ukweli huu na kisha tukaamua kwa dhati ya mioyo yetu kukaa chini wote kama taifa tuone tunawezaje kufanya mabadiliko fulani fulani muhimu na ya lazima ya kisheria na kikatiba ili tuweze kwenda kwenye uchaguzi wote tukiwa pamoja ili tushindanishe hoja zetu huko na wananchi waamue kwa uhuru, uwazi na kwa haki nani awe kiongozi wao kuanzia u - diwani, u - bunge na u - Rais...

Jamani tuache kudanganyana. Tuache siasa za ulaghai wa Rais Samia na CCM yake. Hizo hazina nafasi na zimepitwa na wakati. Twendeni tufanye maamuzi sahihi kwa kuangalia uhalisia wa mambo...!

Lakini kama tunataka tuvurugane kwanza ndo tukae tupatane kuweka mambo sawa, basi twendeni huko maana hakuna atakayekuwa salama; sio CCM, sio viongozi au watawala na vivyo hivyo si hata kwa wananchi wote kwa ujumla wetu...!

NI UAMUZI WETU KUCHAGUA UZIMA AU MAUTI...
 
Hekima hii imfikie Lukas Mwashambwa na ndugu yake tlaahtlaah.Hapa hapahitaji ushabiki wa vyama!
Ngoja tuwa - tag ili waje fast kutoa maoni yao..

Wewe Lucas Mwashambwa na mwenzio Tlaatlaah njooni mtie neno hapa..

Hata hivyo, kati ya hawa wawili, huyu Lucas Mwashambwa kidogo huwa na akili timamu na kabusara fulani sometimes. Huyu akiona hoja ina nguvu, hu - mute na kujichimbia ndani ya Lumumba...

Lakini mwenzake huyu Tlaatlaah, ni mbishi wa kijinga hata kama ukweli wa jambo alobishia unamkodolea macho mbele yake. Huyu hana hekima ya kuzuia vidole vyake kuandika chochote. Na hana hekima ya kujizuia kuuanika ujinga wake pale anapopaswa kufanya hivyo...🚶🏻🚶🏻🚶🏻
 
Lissu ni toothless dog. Ataongea tu na hata yasipofanyika sidhan kama ana uwezo wa kufanya Chochote.

Sababu ni kua polisi, mahakama, tume na vyote vingine viko chini ya chama tawala. Akitaka kuandamanisha watu intelijensia ya polisi kama kawaida yao itasema fujo zitatokea hivyo polisi watazuia.
 
Tatizo lipo kwa wananchi. Wengi wamesinzia na hawana mpango wa kuamka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…