Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nani kasema hivyo? Mtoa mada akikupeleka Mahakamani utajitetea?
Ndio nitajitetea vyema tu...anipeleke huko mahakamani....

Nitaiambia mahakama kuwa mtoa mada ameyachochea majeshi yetu KUIASI serikali halali.....
 
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.
Bila maridhiano ngoma ngumu
 
Kifupi vyombo vya ulinzi na usalama vimeungana na CCM kukumbatia wezi na wabadhirifu wa mali za umma ambao kimsingi ni wachache kuliko wananchi wanao pata tabu, ndio maana nchi hadi leo ni kama imepata uhuru mwaka miaka ya 2000, vitu wanavyo jivuna navyo leo vilitakiwa viwepo tangu miaka ya 90 ila ujinga ndio tatizo la chama na dola
 
Lissu ni toothless dog. Ataongea tu na hata yasipofanyika sidhan kama ana uwezo wa kufanya Chochote.

Sababu ni kua polisi, mahakama, tume na vyote vingine viko chini ya chama tawala. Akitaka kuandamanisha watu intelijensia ya polisi kama kawaida yao itasema fujo zitatokea hivyo polisi watazuia.
Swala hili siyo la Lisu wala Chadema peke yao, ni la watanzania wote wazalendo bila kujali itikadi za vyama.
 
Walipoamka wako Sudan....

Walioamka wako KIVU.....
Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri. (Kutoka 20:1)
Walipoamka wako Sudan....

Walioamka wako KIVU.....
MUNGU atawafanya maadui zako waote ndoto za kutisha! (WAAMUZI 7:9-14)

Bwana atatumia njia zote kuwapiga maadui zako (I WAFALME 20:29-30)

Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. (Isa 41:10-13)
 
Swala hili siyo la Lisu wala Chadema peke yao, ni la watanzania wote wazalendo bila kujali itikadi za vyama.
Tatizo la wananchi ndo hilo. Wengi wanadhani mapambano ya mabadiliko ni ya viongozi wa vyama vya upinzani!
 
Swala hili siyo la Lisu wala Chadema peke yao, ni la watanzania wote wazalendo bila kujali itikadi za vyama.
Mi pia naelewa hivyo,
Ila Watanzania wachache sana wataelewa hivyo.
 
CCM ni imani ya nchi....

Hivyo vyombo bado havijaiona CCM ikibagaza utulivu na amani ya taifa.....
Ccm waibagaze amani ya nchi wakati huu uoga a.k.a amani ndio unawawezesha kufaidika na mali za umma bila kuhojiwa.
 
Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri. (Kutoka 20:1)

MUNGU atawafanya maadui zako waote ndoto za kutisha! (WAAMUZI 7:9-14)

Bwana atatumia njia zote kuwapiga maadui zako (I WAFALME 20:29-30)

Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. (Isa 41:10-13)
Acha paukwa pakawa....

Usalama na utulivu wa Tanzania ndio jambo takatifu lenye kuonekana na la kuadhimishwa zaidi ya maneno yote ya vitabu vya dini yoyote iwayo.....
 
Kabla haujafika huko kwa vyombo vya usalama, bc hii ianzie kwa wananchi hasa wale vichwa maji machawa
 
Ccm waibagaze amani ya nchi wakati huu uoga a.k.a amani ndio unawawezesha kufaidika na mali za umma bila kuhojiwa.
Wewe mwenyewe unafaidika na amani inayokuwezesha kufaidi mali za umma....barabara ,masoko,vituo vya usafiri ,SGR ,madaraja ,vivuko n.k...

Unataka stahiki za ubunge?!! kagombee.....

Unataka stahiki za urais?!! gombea 2025....

Kinyume chake ni maisha ya kufikirika ,kujawa na choyo ,tamaa ,wivu na hasadi kwa hao viongozi.....

#Taifa kwanza
 
Ndo muda wa teeth kuonyesha ile six sense yao kwa kushauri TL asipuuzwe kuzuia hatar isije tokea mbeleni
 
naomba niongeze hoja na iwe namba Moja

kabla hawajaenda kumshauri RAIS ,Waite wataalam ndani ya majeshi yetu mbalimbali wachambue hotuba ya ya kitaifa ya CHADEMa iliyosomwa na LISU (kwanza) kabla hawajaingia kupeleka tathimini na ushauri
 
Tatizo la wananchi ndo hilo. Wengi wanadhani mapambano ya mabadiliko ni ya viongozi wa vyama vya upinzani!
Mapambano yapi ?!!

Mabadiliko yapi ?!!

Viongozi wa upinzani na wanasiasa wanapambania stahiki za kibunge na mengineyo....wanataka watutumie wananchi kama DARAJA tu....duniani kote ni hivyo na mifano itele.....

Watanzania wamejifunza kutoka huko Sudan ,Kenya ,Somalia ,Ethiopia na DRC.....

#Amani na utulivu ni jambo la mwanzo kabla ya hayo maslahi ya wanasiasa walio wachache!
 
Huwezi Jua labda na Vyombo pia wamejikuta mateka au wako mfukoni, hii Dunia Ina mengi unaweza kufanyiwa wema na katiba halafu wewe ukaidharau katiba, karma is a bitch ngoja tuone Mungu ataamua nini awamu ijayo
 
Mkuu,
Inasemekana huyo dogo Tlaatlaah na Lucas Mwashambwa ni mtu mmoja mwenye I'd kadhaa.

Huwa anaandika utumbo na kuunga mkono hoja zake mwenyewe
Jambo la kwanza,
kibaka wa siasa za chadema hawezi kua agenda ya Taifa,

lakini pili,
ni fedheha kumtilia maanani kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ispokua kumpuuza tu,

tatu na mwisho,
hakuna aya, nukta, wala koma kwenye sheria za uchaguzi wala katiba mpya kubadilishwa.

uchaguzi ni Oct 2025, bila kuzingatia au kuskiza mdomo wala makelele ya kibaka yeyote wa siasa wa ndani au nje ya nchi, ispokua kwa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 🐒
 
Back
Top Bottom