Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Usisahau huko kwenyewe kumejaa makada na wanachama watiifu wa ccm hakuna chochote watafanya zaidi ya kufuata maagizo ya kulinda maslahi ya chama chao
 
Jambo la kwanza,
kibaka wa siasa za chadema hawezi kua agenda ya Taifa,

lakini pili,
ni fedheha kumtilia maanani kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ispokua kumpuuza tu,

tatu na mwisho,
hakuna aya, nukta, wala koma kwenye sheria za uchaguzi wala katiba mpya kubadilishwa.

uchaguzi ni Oct 2025, bila kuzingatia au kuskiza mdomo wala makelele ya kibaka yeyote wa siasa wa ndani au nje ya nchi, ispokua kwa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 🐒
Umeandika uharo, sidhani kama haya ni maandishi yako!. Upo sawa mkuu?
 
Tanzania kwanza.
Tanzania kwanza.
Tanzania kwanza.
Watu watapita, Tanzania itaendelea kuwepo.
Mungu Ibarki Tanzania.
 
..jeshi la wananchi, sio jeshi la serikali.

..wanapaswa kuwalinda na kuwatetea wananchi.
Kimsingi ndivyo inapaswa kuwa hivyo ila kwa sasa jeshi linaongozwa na kupokea maelekezo ya wanasiasa.

Amiri jeshi mkuu ni mwenyekiti wa chama, anamteua mkuu wa majeshi CDF anampa maelekezo na amri moja tu HAKIKISHA WALIO CHINI YAKO WANAKIPIGIA KURA CHAMA TAWALA.

Hapo ni wazi jeshi litakuwa upande wa chama tawala na sio wananchi kwa sababu wanalipwa na kula kutoka kwa serikali ya CCM.

Jeshini ukiwa mtu wa kuhoji au ujuaji mwingi wanakubambikia kesi kuwa umeasi kwa kusapoti upinzani.

Vijana wengi sasa jeshini wanapenda na kutamani mabadiliko na hawafurahii upumbavu unaofanywa na wanasiasa waovu wa nchi hii.

Hakika Anguko la CCM limeanza kuonekana wazi.
 
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.
Watathubutu? Wakienda tu baada ya masaa 24 watakuwa under house arrest na hiyo Asali kupewa wanaotii amri. Wewe umezaliwa lini huwajui CCM?
 
Katika vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama nina imani na JW tu lakini TISS na Polisi ni wahalifu wenza wa CCM katika kuvuruga chaguzi za Nchi hii, wangesimama kwenye nafasi zao bila kuipa CCM mbeleko katika uhalifu wao wa wizi wa kura nchi yetu ingeheshimika sana.
Huna unalolijua nyamaza mwana walioko kwenye medani wamekaa kimya halafu lisu sio kamati ya vyombo vya uliznzi hana cha kuishauri wanafanya wanavyoona inafaa kwa msaada tu tafuta clip ya msemaji wahilo jeshi unalosema unaimani nalo kwa kumezeshwa na watu bila kuna na toungable evidences (JW) jamaa banality Ilonda alikua anahojiwa na EA radio akafafanua majukumu mama ya JW na ile dhana ya kua jeshi sio ajira halafu baada ya uchaguzi uzrudi hapa jamvini utakua umepata maana ya jeshi la wananchi mkishashiba miguu ya kuku mnambukizana ujinga
 
Kimsingi ndivyo inapaswa kuwa hivyo ila kwa sasa jeshi linaongozwa na kupokea maelekezo ya wanasiasa.

Amiri jeshi mkuu ni mwenyekiti wa chama, anamteua mkuu wa majeshi CDF anampa maelekezo na amri moja tu HAKIKISHA WALIO CHINI YAKO WANAKIPIGIA KURA CHAMA TAWALA.

Hapo ni wazi jeshi litakuwa upande wa chama tawala na sio wananchi kwa sababu wanalipwa na kula kutoka kwa serikali ya CCM.

Jeshini ukiwa mtu wa kuhoji au ujuaji mwingi wanakubambikia kesi kuwa umeasi kwa kusapoti upinzani.

Vijana wengi sasa jeshini wanapenda na kutamani mabadiliko na hawafurahii upumbavu unaofanywa na wanasiasa waovu wa nchi hii.

Hakika Anguko la CCM limeanza kuonekana wazi.
Umekubali hapo hapo umekaþaa jeshini hawakumbatii ahadi hewa wanaishi na hali joto iliopo
 
Hapa Kuna kesi nzuri ya uchochezi unaoelekea kwenye uhaini!

Vyombo vya dola viache kulinda serikali iliyopo vigeuke upinzani kudai kinachoitwa katiba! Huu ni uhaini!

BTW, katiba mpya haina faida yeyote kwa wananchi wa kawaida zaidi ya wanasiasa wanaotamani kupata madaraka na ajira kwa ndugu na marafiki zao!
 
  1. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananch
Sio tu imani kwa wananchi.

Vitakuwa vimeliokoa Taifa kutoka kwenye kuharibika na kupotea kabisa. Maana CCM wameshalinajisi hili taifa kutokana na kukithiri kwa Rushwa, Ujinga na Uchawa.
 
Amiri jeshi mkuu ni mwenyekiti wa chama, anamteua mkuu wa majeshi CDF anampa maelekezo na amri moja tu HAKIKISHA WALIO CHINI YAKO WANAKIPIGIA KURA CHAMA TAWALA.

Hapo ni wazi jeshi litakuwa upande wa chama
Chadema mna vitu vya kijinga vingi mno taja nchi moja tu duniani ambayo mkuu wa majeshi huwa hateuliwi na Raisi
 
Huna unalolijua nyamaza mwana walioko kwenye medani wamekaa kimya halafu lisu sio kamati ya vyombo vya uliznzi hana cha kuishauri wanafanya wanavyoona inafaa kwa msaada tu tafuta clip ya msemaji wahilo jeshi unalosema unaimani nalo kwa kumezeshwa na watu bila kuna na toungable evidences (JW) jamaa banality Ilonda alikua anahojiwa na EA radio akafafanua majukumu mama ya JW na ile dhana ya kua jeshi sio ajira halafu baada ya uchaguzi uzrudi hapa jamvini utakua umepata maana ya jeshi la wananchi mkishashiba miguu ya kuku mnambukizana ujinga
Mbona unaharisha badala ya kujibu hoja ? Unaonekana umechanganyikiwa wewe naamua kukupuuza kwani hoja imekuzidi kimo.
 
Mapambano yapi ?!!

Mabadiliko yapi ?!!

Viongozi wa upinzani na wanasiasa wanapambania stahiki za kibunge na mengineyo....wanataka watutumie wananchi kama DARAJA tu....duniani kote ni hivyo na mifano itele.....

Watanzania wamejifunza kutoka huko Sudan ,Kenya ,Somalia ,Ethiopia na DRC.....

#Amani na utulivu ni jambo la mwanzo kabla ya hayo maslahi ya wanasiasa walio wachache!
Hujui kuwa Mamlaka ya uongozi yanatakiwa kutoka kwa wananchi? Kwa Hali ya sasa mamlaka hayo yanatoka kwa mwenyekiti wa ccm, akiamua nani awe kiongozi anakuwa, na akiamua nani asiwe kiongozi hupati uongozi hata kama wananchi watakuchagua. Huoni hili ni tatizo?
 
Jambo la kwanza,
kibaka wa siasa za chadema hawezi kua agenda ya Taifa,

lakini pili,
ni fedheha kumtilia maanani kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ispokua kumpuuza tu,

tatu na mwisho,
hakuna aya, nukta, wala koma kwenye sheria za uchaguzi wala katiba mpya kubadilishwa.

uchaguzi ni Oct 2025, bila kuzingatia au kuskiza mdomo wala makelele ya kibaka yeyote wa siasa wa ndani au nje ya nchi, ispokua kwa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 🐒
Muda utasema.
 
Back
Top Bottom