Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapa ndipo ile sera na ujamaa na kujitegemea inapotugharimu ni sera ya kupalilia umaskini na kukufanya uwe mtumwa.. Ila wenzetu Kenya hawafagilii l.. Ndiyo maana walifanikiwa kubadili katiba yao..
 
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.
Umeandika vizuri ,nami naongezea.
Wakuu wa vyombo wascan watu wao , yoyote ilie na itikadi za siasa afutiliwe mbali , hawa ndo adui wa taifa katika vyombo vyetu
 
Kwa maoni yangu naona umenena vyema sana, tatizo ninaloliona kwa nchi za wajamaa ni kuchanganya, makada wa vyama na vyombo vya dola. Inafahamika kwamba wakuu wa mikoa na wilaya ni makada wa ccm ,hapo hapo unakuta ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa mikoa/wilaya husika. na unakuta wengine wana vyeo vya kijeshi au ni mapolisi sasa hapa panatuchanganya. uwezekano wa aliye na buyu la asali akukabidhi ulambe wewe yeye akiangalia shida inaanzia hapo.
Tupambane kubadilisha huu ujinga.
 
Hapa ndipo ile sera na ujamaa na kujitegemea inapotugharimu ni sera ya kupalilia umaskini na kukufanya uwe mtumwa.. Ila wenzetu Kenya hawafagilii l.. Ndiyo maana walifanikiwa kubadili katiba yao..
Tanzania tumekwishahama kwenye Ujamaa na Kujitegemea. Tupo kwenye Ubepari.
 
Faida yao ya "kuliamsha" ni nini ?!!

Unafikiri "kitoto sana"....

Amani inapotoweka usidhani kuwa wahanga wa machafuko huwa ni hao wanasiasa na viongozi....

Mhanga nambari moja n mimi ,wewe ,watoto wako ,wangu ,mke wako ,wangu na wazazi wako na wangu.....

Fikiri kwa mapana mzeya !!
Uhuru usingepatikana kama waliokuwepo kipindi kile wasingeliamsha. Jukumu lile lie lipo pale pale kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Lengo ni kuusaka Uhuru!
Amani kutoweka ni sehemu ya mchakato wa kuusaka Uhuru!
 
Uhuru ulishapatikana 1961...mkitafutacho ni UHAINI tu....
 
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.
Vyombo ulinzi wafanye uzalendo mchi kwanza sio chama wala Rais.....Mama Tanzania kwanza
 
Serikali ni "part" ya wananchi....kazi ya jeshi ni kuilinda dola ikiwemo na serikali....acha utoto

..kama jeshi haliko kwa ajili ya wananchi kwanini serikali mbalimbali hupinduliwa?

..kiongozi akionekana hasikilizi wananchi jeshi lina haki ya kuingilia kati.
 
Mimi BushDokta naunga mkono hoja zako na kama vyombo vinajali basi ushauri huu ni sawa

Imagine

1.Mkurugenzi Mtendaji wa NEC ni CCM
2. Wajumbe wa NEC ni ccm
3. Polisi wanaolinda Kura ni wateule wa ccm
4. Wasimamizi wa Uchaguzi ni ccm
5. Usalama wa Taifa ambai kimsingi ni wadau kwenye mambi ya kitaifa wana influence ya uccm kwa kiasi flani.

6. Mifumo ya kukusanya na kuhesabu kura ni ya ccm
7. Wajumbe na wagombea wakidai haki wakati wa zoezi wanadhulika na kushambuliwa wengine hadi kufa.

Ktk Mazingira kama haya unaposema unashriki uchaguzi ili iweje?
Unless una maslahi huo uchaguzi zaidi ya ushindi ndipo utashiriki.

Hoja za Lissu ziko Valid for 100%.

Anayezipinga sio Mzalendo
Anayepinga anaahirisha kufikiri kizalendo, a.k.a kujizima data
 
Mkoloni alifanya makubwa lakini hakuwahi kuimbwa na kuabudiwa kama mtawala wa sasa

Emancipate yourselves from mental slavery - Bob Marley
Liko wapi jengo la kiibada la kumuabudu mh.Rais Samia?!!

Kuimbwa ni lazima aimbwe kwani klabu ya Yanga tu iliimbwa na marehemu Pepe Kale wa DRC......
 
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.

MAPINDUZI
 
Umeongea pointi,vyombo vya ulinzi visimamie taifa na siyo chama kimoja
Sasa hapo inategemea uzalendo wa taasisi husika,wengine wanadhani uzalendo ni kuibeba ccm milele na wengine wana mawazo kwamba bila ccm hakuna maisha.
Kuna mambo mengine ni ya msingi sana;lakini utasikia watu kama viongozi wa dini wanahimizwa kuombea amani,lakini viongozi hao hao wa dini wanashindwa kuiambia serikali kuweka misingi ya amani kwa taifa ili amani iendelee kudumu. tuna kazi kubwa sana wadanganyika
 
Acha kuviingiza vyombo vyetu wa ulinzi na usalama katika TREASON....

Mkuu wangu huo uufanyao ni UHAINI......
Jamani muwe mnawaonea huruma ndugu zenu siyo matumbo yenu tu. Sasa hivi ni nchi nzima inataka mabadiriko huwezi kua unalazimisha kila kitu kwa nguvu. Hii nchi ikisambaratika itamhusu kila mtu.

Acheni ubinafsi. Kwa nini hamtaki haki?
 
Back
Top Bottom