Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.
Mkuu,

Kwanza kabisa, nakuelewa sana. Lissu anasimamia mengi ya msingi yanayohitaji kusimamiwa. Kwa hiyo siko hapa kumpinga Lissu.

Lakini. Strategy yako ina maswali mengi kuliko majibu.

Item 1 ni violation ya kanuni muhimu ya civilian control of the military. Katika nchi ya kidemokrasia, uongozi wa jeshi hauna mamlaka ya kuwapangia viongozi wa kiraia nini cha kufanya. Viongizi wa kiraia ndio wanalipangia jeshi nini cha kufanya.

Item 2 ina contradict item 1. Ukishaanza kwa kusema wanajeshi waingilie siasa (item 1), halafu ukaifuatia point hiyo kwa kusema wanajeshi wasiingilie siasa (item 2) hapo kuna contradiction. Unataka wanajeshi waingilie siasa au wasiingilie siasa? Unajichanganya.

Item 3 nayo ina contradict kanuni ya msingi ya wanajeshi kutojiingiza katika siasa.

Kimsingi hapo points zako zimekaa hivi.

1. Wanajeshi wajiingize katika siasa.
2. Wanajeshi wasijiingize katika siasa.
3. Wanajeshi wajingize katika siasa.

This is nit only a contradiction.

It is a contradiction within another contradiction.
 
Jamani muwe mnawaonea huruma ndugu zenu siyo matumbo yenu tu. Sasa hivi ni nchi nzima inataka mabadiriko huwezi kua unalazimisha kila kitu kwa nguvu. Hii nchi ikisambaratika itamhusu kila mtu.

Acheni ubinafsi. Kwa nini hamtaki haki?
Haki ya nchi ni nini ?!!

Haki ya taifa ni nini ?!!

Sikiliza mkuu wangu ,haki za hivyo viwili hapo juu ni ;

1)Utulivu wa nchi ,
2)Amani ya taifa ,

Gharama za kuibadilisha "status quo" yoyote ni kubwa ila huwa gharama MARADUFU kuibadilisha "status quo" ya DOLA-NCHI-TAIFA......

Gharama hizo wa kuzilipia ni watanzania wote ,pumzi na damu zao......

Acheni maskhara ya hoja koko za baadhi ya wanasiasa....

#Taifa kwanza kwa njia yoyote iwayo!!
 
Hivi na wewe ni Expert Member: Mkuu kazi ya Jeshi sio kulinda dola, bali kazi yao KUU ni kulinda Nchi na Wananchi, ndio maana linajulikana kama 'Jeshi la Wananchi Tanzani - JWT"
Hivi mkuu umesahau kuwa wanajeshi kule TMA kozi wanavikwa NYOTA ya uluteni na mh.Rais wa JMT ?!!

Hebu waulize kuhusu KIAPO wanachomuahidi AMIRI JESHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA......

Unachanganywa wapi hau ?!!
 
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.
Tanzania sio Nchi ya kuchezewa na wapuuzi Wala Haina raia wa kuwa kafara Kwa maslahi ya vibaraka.
 
Kushiriki uchaguzi kwa mazingira haya ni kupaka rangi upepo
 
Liko wapi jengo la kiibada la kumuabudu mh.Rais Samia?!!

Kuimbwa ni lazima aimbwe kwani klabu ya Yanga tu iliimbwa na marehemu Pepe Kale wa DRC......
Wewe nawe kilaza... Kwani ibada ni lazima ifanyikie ndani ya jengo?
 
Tufanye mzimuni ,ni wapi huko tunakofanyia ibada ya kumuabudu mh.Rais Samia ?!!
Kuanzia bungeni, kwenye media zote, halmashauri hadi kwako nyumbani - kote huko mnaabudu na kuimba mapambio as if bila Rais hamuwezi kuishi na kufanya kazi!
Yaani kwenu chura kiziwi anakuja kabla ya MUNGU!
Ovyo sana!
 
Habari Ndugu zanguni,

Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.

Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

  1. Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
  2. Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
  3. Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikifanya haya, vitajenga imani kwa wananchi kwamba vipo kwa maslahi ya Taifa, si kwa chama fulani cha siasa.
Wakuu wa usalama hawahusiki na mambo ya siasa, mkishindwa siasa nendeni mkalime
 
Mungu aliugeuza Moyo wa Farao kua mgumu hata asielewe nyakati na matukuo yake .

Dola ikijiuliza , Vyama vingapi Afrika vya ukombozi, vimeanguka na vimeangukaje?.

Sio lazima Nchi iwe kama Nchi zingine .

Hata Dola itumie nguvu Kwa Upinzani, Nyakati zinataka Mabadiliko .

Ikubali, Mabadiliko ya Sheria za uchaguzi na Tume huru.
Unaijua China? Tangu 1949 mpk leo inatawaliwa na CPC, CCM inafanya vizuri hatutaki hao vibaraka
 
Acha kuviingiza vyombo vyetu wa ulinzi na usalama katika TREASON....

Mkuu wangu huo uufanyao ni UHAINI......
Vyombo vya ulinzi na usalama vinajua katiba na sheria za nchi? Wafanye kazi yao ya kutoa huduma ya ulinzi na usalama, sio kukimbizana na wanasiasa, wa upinzani tu, na kukumbatia wa chama tawala.
 
Katika vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama nina imani na JW tu lakini TISS na Polisi ni wahalifu wenza wa CCM katika kuvuruga chaguzi za Nchi hii, wangesimama kwenye nafasi zao bila kuipa CCM mbeleko katika uhalifu wao wa wizi wa kura nchi yetu ingeheshimika sana.
TPDF ndio wanaohakikisha wapinzani hawashiki dola Zanzibar since 1995. Vyombo vyote vya usalama Tz ni "lao moja".

Ikikaribia uchaguzi wanashika bandari zote, airport zote, vyombo vya habari vya serikali, wanaweka vizuizi barabarani kila baada ya kilometer kadhaa, wanazingira ikulu....

Zanzibar kila miaka mitano literally JW wanaongoza mapinduzi mapya kwa kushirikiana na taasisi nyengine za serikali.

Upinzani Tz bado una safari ndefu.
 
Define Treason for the sake of majority understanding! Au unadhani ukisema treason itatishia zaidi! Je vyombo vya usalama vinapofanya alliance na CCM hadharani kama hapa huoni ukandamizaji usiopaswa kufanyiwa?

View: https://youtu.be/_m1RFcDeTVY?si=_i0Ys2B2NENeOquS au nchi hii ni Mali ya watu Fulani tu na watu wanapaswa kutawaliwa Kwa lazima na ghiliba na kundi fulani
Acha kuviingiza vyombo vyetu wa ulinzi na usalama katika TREASON....

Mkuu wangu huo uufanyao ni UHAINI......
 
Back
Top Bottom