Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyo jamaa anautaka uraisi kwa nguvu sana.
 
H
Hizo sio kazi za vyombo vya Ulinzi na usalama
 
Sawa mkuu wangu, kakini sijasema naviamini vyote, TISS na Polisi ni wahalifu wenza wa CCM.
TISS na POLICE wakiamua wayafate haya mnayoyataka basi patatokea machafuko hapa nchini ambayo hao JW watashindwa kuyazuia
 
Hivi mkuu umesahau kuwa wanajeshi kule TMA kozi wanavikwa NYOTA ya uluteni na mh.Rais wa JMT ?!!

Hebu waulize kuhusu KIAPO wanachomuahidi AMIRI JESHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA......

Unachanganywa wapi hau ?!!
Mkuu, kuapa kwao kwa Rais ni kwa sababu yeye ndie Mkuu wao wa kazi (Amiri Jeshi Mkuu), ambaye amepewa Mamlaka na Wananchi. Aidha katika kiapo hicho, wanaapa kwa Rais kwaba "watawalinda Wananchi wa Jamhuri ya Muungano 🇹🇿 na Mipaka yake. Nadhani sasa utaelewa.
 
Ha ha ha ha mkuu wangu unazunguuukaaa.....

JMT ,Rais , Watanzania ni KITU KIMOJA..... falsafa pana hiyo mkuu wangu !

#JMT kwanza !
 
Vyombo vya ulinzi na usalama vinajua katiba na sheria za nchi? Wafanye kazi yao ya kutoa huduma ya ulinzi na usalama, sio kukimbizana na wanasiasa, wa upinzani tu, na kukumbatia wa chama tawala.
Huduma yao ya ulinzi na usalama haina mipaka ya kutowafikia hao WANASIASA.....
 
Kuanzia bungeni, kwenye media zote, halmashauri hadi kwako nyumbani - kote huko mnaabudu na kuimba mapambio as if bila Rais hamuwezi kuishi na kufanya kazi!
Yaani kwenu chura kiziwi anakuja kabla ya MUNGU!
Ovyo sana!
Umeweka AVATAR ya mwenye heri EL Commandante JKN nikadhani nawe una fikra pana sana...

Mkuu ni kweli bila RAIS mambo yetu watanzania hayaendi.....

Haina maana tunamuabudu Rais bali TUNAUADHIMISHA urais....hata ingekuwa wewe ndiye Rais hakika ningekuadhimisha vyema tu.....


Kumuadhimisha Rais ndiko kunakoleta UTULIVU NA AMANI ambayo akina Aziz Ki wanaamua KULOWEA hapa JMT.... wakongomani walioko hapa wanajua wanachopitia kwa M 23.....
 
 

Attachments

  • UDIKTETA MWALIM NYERERE.jpg
    100.1 KB · Views: 1
TISS na POLICE wakiamua wayafate haya mnayoyataka basi patatokea machafuko hapa nchini ambayo hao JW watashindwa kuyazuia
Una maana ukifanyika uchaguzi huru na haki bila wizi unaratibiwa na TISS na Polisi patatokea vurugu? Mbona sikuelewi, yaani kuwa watu hawataki uchaguzi huru na haki?
 
Ha ha ha ha mkuu wangu unazunguuukaaa.....

JMT ,Rais , Watanzania ni KITU KIMOJA..... falsafa pana hiyo mkuu wangu !

#JMT kwanza !
Mkuu, hivi haujui kwamba Rais ni mwajiriwa, na mwajiri wake ni Mwananchi, ndio maana wanachukuaga fomu za kuomba kazi hiyo. JMT ndio makazi ya hao wote wawili
 
Maboresho ya katiba yatasaidia pia vyombo vya ulinzi kuboreshwa na kuwa vya kisasa zaidi.
 
JKN nilimuelewa mapema sana hasa alipoanza kupingana na mamlaka za ccm.
Angekuwepo hadi leo angeshawaamsha wengi kutoka usingizini!
 
TISS na POLICE wakiamua wayafate haya mnayoyataka basi patatokea machafuko hapa nchini ambayo hao JW watashindwa kuyazuia
Yaaani machafuko yatokee kwa mafisadi CCM kutolewa madarakani?

Kawatishe wajinga wenzako huko Lumumba.
 
Mkuu. Mimi sijazungumzia Jeshi. Nimezungumzia Vyombo vya ulinzi na usalama, ambavuo ni vingi tu katika nchi hii. Vyombo hivi vinajukumu la kunusa hali ya hatari na kumshauri Raisi nini cha kufanya kuepukana na hatari hiyo. Watakuwa wazembe kama wataona hatari mbele yetu halafu wakashindwa kumshauri Raisi nini cha kufanya kihofia kuonekana wanajiingiza kwenye siasa.
Kumbuka Nchi nyingi za Afrika zimeingia kwenye machafuko mara tu baada ya uchaguzi. Sababu ni haya haya mambo ya mifumo ya uchaguzi kupendelea chama Fulani.
 
Kitu pekee ambacho wanapaswa kufanya kama vyombo vya ulinzi na usalama ni kumshughulikia Lissu endapo atavuka mipaka ya uchochezi.
 
JKN nilimuelewa mapema sana hasa alipoanza kupingana na mamlaka za ccm.
Angekuwepo hadi leo angeshawaamsha wengi kutoka usingizini!
CCM ni IMANI na si mali binafsi ya hayati baba wa taifa.....

Kamwe asingeikana IMANI hii tukufu.....
 
Kitu pekee ambacho wanapaswa kufanya kama vyombo vya ulinzi na usalama ni kumshughulikia Lissu endapo atavuka mipaka ya uchochezi.
Hata Gadafi, Asad na Sadam walitumia vyombo vya ulinzi na usalama vya Nchi zao kushughulikia wapinzani, Leo wapo wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…