Kwa asilimia kubwa sana dunia inaendeshwa na mawazo ya kike

Kwa asilimia kubwa sana dunia inaendeshwa na mawazo ya kike

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Kama dunia imekwama mahali fulani au imefanikiwa sana basi yote hayo mawili yamesababishwa na mwanamke.

Wanaume wote kabisa kwa 90% ni wanawake kwa mawazo yao (ambayo ndiyo yanayotengeneza tabia zao na mifumo ya maisha yao), pia wanaishi mfumo ambao siyo dume bali jike (feminism) kasoro maumbile tu.

Ni mwanamke ndiye anayemshape mtu tangia kwenye hatua ya ujauzito, kuzaliwa, kukuwa hadi kuwa mtu mzima. Ni mwanamke ndiye anayemfundisha mtoto (mtu) kufanya yafuatayo:-

1. Kuvaa.

2. Kula.

3. Kuongea.

4. Kuoga.

5. Kutambaa na kutembea.

6. Kucheza kwa jinsi isiyo hatari.

7. Kumkemea.

8. Kulala.

9. Kusimamia homeworks.

10. Neno la kwanza kutamkwa na mtoto ni “mama” la pili ni “dada”, kaka na baba vinafuata mwisho kutamkwa.


NB. Kwa asilimia kubwa sana dunia inaendeshwa na mawazo ya kike.
 
Kuna kaukweli fulani hiv ila ngoja nifikirie kwanza vizuri
Kwenye Msaafu wa Biblia ambao ndiyo ninaujuwa, nimegundua kuwa role ya Mwanamke ilifungwa katika kuokoa maangamizi ili maisha yaendelee/dunia iendelee.

Adamu alipata akili kubwa baada ya kumpewa Hawa.

Kwa theory hii, ninaamini Rais Samia ataipeleka Tz pakubwa kuliko Marais waliopita. Ellen Johnson Sirleaf ndiye aliyeondoa vita kongwe Liberia iliyoshinda wanaume zikiwemo jumuiya za kimataifa hadi akazawadiwa Nishani ya Nobel.
 
Ni manii ya baba na Yai la mama ndiyo inayomform mtoto na kwenda kutunzwa kwenye tumbo la uzazi yaani placenta (kwa miezi tisa). Mtoto anatengenezwa na kudevelop tabia kutokana na details zilizobebwa kwenye manii ya baba pamoja na details zilipo kwenye Yai la mama full stop.

Always Mwanaume ni Vision na Mwanamke ni Mission kwa pamoja wanaform kitu kinachoitwa Mwanadamu.

Jaribu kuchimba vizuri utugundua hakuna mawazo ya kike na hakuna mawazo ya kiume bali ni mawazo ya mwanadamu. Kwa sababu kila mmoja ni sehemu ya mwili wa mwenzake.
 
Ni ukweli..watu watajifanya kukataa tu. Lakin wengi wanapelekeshwa na wake zao, mwanamke akisema sitaki hiki mtu anaufyata. Watu wanapokea maelekezo kutoka kwa mama zao mpaka sasa
Hahahahaaa mkuu, Kama wake za Marais wangetembelewa na pepo mmoja wa uasi akawaambia ueni waume zenu leo Marais hao waliofanya makubwa kwa dunia wasingelikuwepo. Hivi unaamini ni kweli kwamba ni RAHISI KWA SERA, KANUNI, SHERIA, NA HATA KATIBA VISIMSHAWISHI CDF AU HATA BOSI WAKE kwenye jambo fulani lakini wake zao wakaweza kuwashawishi kwa 100% na kwa dkk 0?
 
Ni manii ya baba na Yai la mama ndiyo inayomform mtoto na kwenda kutunzwa kwenye tumbo la uzazi yaani placenta (kwa miezi tisa). Mtoto anatengenezwa na kudevelop tabia kutokana na details zilizobebwa kwenye manii ya baba pamoja na details zilipo kwenye Yai la mama full stop.

Always Mwanaume ni Vision na Mwanamke ni Mission kwa pamoja wanaform kitu kinachoitwa Mwanadamu.

Jaribu kuchimba vizuri utugundua hakuna mawazo ya kike na hakuna mawazo ya kiume bali ni mawazo ya mwanadamu. Kwa sababu kila mmoja ni sehemu ya mwili wa mwenzake.
Mkuu usiweke full stop,
Huku duniani nani anamshape mwanadamu kati ya baba na mama?
 
Ni manii ya baba na Yai la mama ndiyo inayomform mtoto na kwenda kutunzwa kwenye tumbo la uzazi yaani placenta (kwa miezi tisa). Mtoto anatengenezwa na kudevelop tabia kutokana na details zilizobebwa kwenye manii ya baba pamoja na details zilipo kwenye Yai la mama full stop...
Lakini ni wanadamu wenye jinsia, so ni jinsia ipi hiyo zaidi inamshape mwanadamu?
 
Ebu oneni hiki kisa huenda kikasaidia kukubali mada.

Mgeni Bi. Anna Mukuta Tibakwendera ameenda nyumbani kwa jamaa zake Bw. & Bi. Kabalimu Mutahanamilwa, akiwa anabarizi sebuleni na mwenyeji wake aliyemkuta (mama mwenye nyumba) mara mtoto akaamka usingizini na kuvamia sebuleni na kuingilia na kumiliki mazungumzo ya mamake na mgeni yule, ikawa hivi:-
  • Mtoto – wewe mgeni naomba jero nikacheze gemu.
  • Mgeni – wewe unatakiwa usome siyo kucheza gemu.
  • Mtoto – wewe ulivyosoma umefika wapi mbona mchovu tu kama Ticha wangu kila siku anataka tukanunuwe ubuyu wake.
  • Mgeni – dah! Huyu mtoto vipi huyu?!
  • Mzazi – mwanangu mpenzi unakuwaaaje lakini? Usifanye hivyo kwa mgeni! Mgeni mpuuze huyu bado mtoto akikuwa ataacha.
  • Mgeni – akaduwaa.
  • Mtoto – naomba basi buku.
  • Mgeni – sina hata hiyo. Wewe kafanye homuweki (homework) zako.
  • Mtoto – maweee hata mia ya kugongea geti pia huna? Kwahiyo umeruka geti letu kama dady?
  • Mzazi – jamani mwanangu mzuri kacheze basi nje na wenzako baadaye nitakuita babangu nikukaangie chips.
  • Mtoto – mimi sichezi na watoto wasiojuwa maisha.
  • Mzazi – basi kaangalie katuni mwanangu mzuri.
  • Mtoto – kwa ukali: sitaki sitaki sitaki. Anti (mgeni) mwenyewe huyu katuni tosha.
  • Mtoto – hata hamsini ya kukwangulia vocha pia huna? Anamuuliza mgeni.
  • Mgeni – kimyaaa...
  • Mtoto – si nilikwambia umesoma lakini mchovu tu.
  • Mzazi – mwanangu mzuri njoo basi nikupakate ulale, umwache mgeni aongee na mimi.
  • Mtoto – anti (mgeni) naomba basi simu yako niangalie Tiktok.
  • Dada wa kazi – kafungua jokofu harufu mbaya ikafika sebuleni bila mtoto kujuwa ni jokofu.
  • Mtoto – mmm… (anafuta pua kwa kidole…) mama nani kapuu? Ebu acha nimtafute, akaanza kuimba kwa kuhesabu mamake, yeye na mgeni kwa kutumia kidole kwamba yeye ambaye wimbo na kidole vitaishia kwake basi huyo ndiyo kapuu: “ana ana ana doo, kaja ka plasto, kajamba, ushuzi unanuka, tena sana, sana kabisa” Kidole kilivyotaka kuishia kwa mamake akakilazimisha kikaishia kwa mgeni.
  • Mzazi – wewe… babako akija nakusemea una tabia mbaya!
  • Mtoto – sema tu, baba mwenyewe mlevi yule, kila siku anarudi tumeishalala na naondoka shule bado amelala, saa ngapi atanichapa.
  • Mgeni – shoga mimi naondoka, tutawasiliana.
  • Mzazi – jamani… sasa unaondoka hata hatujaongea shoga yangu?!
  • Mgeni – hapana shoga ahsante, acha tu niwahi, tutaongea siku nyingine, uwe na amani ya kutosha kabisa.
  • Mzazi – haya shoga, wasalimie, karibu tena siku nyingine tuongee vizuri.
  • Mgeni – nikipata nafasi.
  • Mgeni – (nje ya geti anaondoka anajisemesha mwenyewe) mmm… nimekishiba hicho kitoto! mimi nirudi tena hapa! Labda hicho kitoto kiwe “kilemavu 3G yaani bubu, kiziwi na kipofu nitarudi”

Maswali
1. Wewe msomaji, angekuwa mwanao ungemfanyaje? Ungekuwa mgeni ungefanyaje?
2. Je, hapa baba anaweza kipi na nini kumbadilisha mtoto kama huyu mwenye viashiria vya kuwa mtukutu?
3. Unadhani mama akiamua kwa dhati hawezi kumbadilisha mwanaye huyu?
4. Huyu mtoto awapo nyumbani nani kati ya baba na mama anashinda naye kwa muda mrefu?
5. Je, unakubali au unakanusha kwamba kwa asilimia kubwa sana dunia inaendeshwa na mawazo ya kike?
 
Hahahahaaa mkuu, Kama wake za Marais wangetembelewa na pepo mmoja wa uasi akawaambia ueni waume zenu leo Marais hao waliofanya makubwa kwa dunia wasingelikuwepo. Hivi unaamini ni kweli kwamba ni RAHISI KWA SERA, KANUNI, SHERIA, NA HATA KATIBA VINAWEZA VISIMSHAWISHI CDF AU HATA BOSI WAKE kwenye jambo fulani lakini wake zao wakaweza kuwashawishi kwa 100% na kwa dkk 0?
Hakika.. unaweza kuta hata mkuu wa majeshi huko kazini wanamuhanya balaa!! Lakin akifika kwa mke wake anamuhanya balaa! Yan unaweza kuta mke hamtaki hata mama wa mume wake, na jamaa anaufyata mama mzazi hakanyagi nyumbani.
 
Hakika.. unaweza kuta hata mkuu wa majeshi huko kazini wanamuhanya balaa!! Lakin akifika kwa mke wake anamuhanya balaa! Yan unaweza kuta mke hamtaki hata mama wa mume wake, na jamaa anaufyata mama mzazi hakanyagi nyumbani.
Mwanamke akiolewa anakuwa anabeba viwili pamoja naye kwenda kwenye ukoo wa mumewe: Amani na Mafarakano (Mashirikiano na Matengano), kimojawapo anakwenda kukipandikiza. Hivyo anaweza kuvitumia kushape ukoo wa mumewe ama positively au negatively na AKABADILI MAISHA COMPLETELY ya ukoo wa mumewe.
 
Kama nihivyo basi wanaime ndo tungedai haki sawa. Kama wanawake ndo wanashep mtu basi wangetushepu tu kuwaogopa na kuwaachia madaraka yote. Yaani mwanaume kawa raisi ila tumsifu mke wake kwa kumshawishi ila huyo mke wa raisi alishindwa kuushawishi uma umfanye ye ndo rais. Hapo tutasemaje wanashep watu
 
Ni manii ya baba na Yai la mama ndiyo inayomform mtoto na kwenda kutunzwa kwenye tumbo la uzazi yaani placenta (kwa miezi tisa). Mtoto anatengenezwa na kudevelop tabia kutokana na details zilizobebwa kwenye manii ya baba pamoja na details zilipo kwenye Yai la mama full stop...
Ila mwanamke ana uwezo mkubwa wa ushawishi kwa kutumia lugha ya maumbile kuliko lugha ya kinywa. Mwanaume hana uwezo huo, uwezo wake uko kwenye lugha ya waleti, ndiyo maana mwanaume asiyejaliwa lugha ya waleti hawezi kulishawishi hata jibwa lake , jibwa litahama nyumbani kutafuta mji ambao watu wana kawaida ya kwenda buchani, hata mwanamke naye anawezakumtaliki mwanaume kwasababu haongei lugha ya waleti.
 
Back
Top Bottom