Kwa asilimia kubwa sana dunia inaendeshwa na mawazo ya kike

Kwa Simba, jike ndiye ana impact (tija), dume ni bazazi tu.
Kwa Tembo, jike ndiye mkuu wa familia na jike mkongwe ndiye mkuu wa ukoo.
Kwa kuku mlinzi wa vifaranga ni mtetea, jogoo anajuwa kufunga tai tu 12/7/24/365.
 
Mkuu,
Adamu alishepiwa na nani?
When you want to discuss something or judge anything...don't pick a side my friend.

Adam and Eve wote kwa pamoja kwa ukamilifu wao. Kila kitu kwenye maisha kinaimpact yake as longer as kipo ndani ya nature.

Formally stated, Newton's third law is: For every action, there is an equal and opposite reaction. The statement means that in every interaction, there is a pair of forces acting on the two interacting objects. The size of the forces on the first object equals the size of the force on the second object.
 
Msahafu unatuambia "ishini nao kwa akili"1Pet.3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili.

Mwanamke (siyo lazima wa ndoa) akikushawishi vunja Katiba utakataa kwa asilimia ngapi na utakubali kwa asilimia ngapi? Vivyo hivyo akikushurutisha kwamba toa talaka utakataa kwa asilimia ngapi na utakubali kwa asilimia ngapi?
 
Isaac Newton mwenyewe alimpiga mawe babake wa kambo kwa kumpiga mamake, na Isaac akatoroka nyumbani na kuwa chanzo cha yeye kuwa school dropout. Japokuwa huyu babake wa kambo alikuwa akimhudumia ikiwemo kumsomesha lakini inadhihirika kwamba Isaac alimbeba mamake moyoni zaidi kwasababu ndiye aliyemshape!
 
Ulichosema ni kweli. Wengi wanaangalia upande wa nguvu na mamlaka aliyonayo mwanaume pasipo kukumbuka kuwa wengi wetu tumelelewa na mama zetu tukiambiwa mwanaume lazma uwe jasiri na mwenyewe mamlaka na wanawake kupandikiziwa mitazamo ya wao ni dhaifu kwa mwanaume na niwajibu wao kuwatumia wanaume, lakin ukwel ni kuwa ujasir na mamlaka tuliyonayo tumeyapata toka kwa hao hao wanawake na kama ikitokea leo hii(siombi iwe hvyo) wanawake wakabadirika na kuanza kuwakuza watoto wa kiume kama wakike na wakike kama wakiume bas ndan ya miongo 2 au 3 mwanaume atapoteza authority aliyonayo sasa .

NB: nimeangalia upande wa malezi
 
Katu! labda mtoto wa chupa (aliyezaliwa maabara), kwasababu baba amegoma kuoa hivyo anatoa mbegu zake atengenezewe mtoto wa chupa (maabara).
Hujawai kulea kwaio kausha uliza aliewai kulea mtoto yeyote yule neno baba ndio lakwanza hatakama baba hajawai kukuona
 
Wanaume walio wengi wakitalikiana na wake zao huwa wanawatamania kifo cha mapema au hata kuwaua watalaka wao hao lakini mwanamke siyo rahisi kuwaza kumuua mtalaka wake.
 
Hujawai kulea kwaio kausha uliza aliewai kulea mtoto yeyote yule neno baba ndio lakwanza hatakama baba hajawai kukuona
Kwanini mtoto kwa mkubwa wakipata dharura wanatamka neno "mamaaaaa" badala ya "babaaaaaa"?
 
Hujawai kulea kwaio kausha uliza aliewai kulea mtoto yeyote yule neno baba ndio lakwanza hatakama baba hajawai kukuona
Kwanini mama akifa familia inakosa mwelekeo hata kama baba ana uchumi mzuri? Kwanini baba akifa hata kama mama hana uchumi mzuri familia inatoboza?
 
Kwanini mtoto kwa mkubwa akipata dharura anatamka neno "mamaaaaa" badala ya "babaaaaaa"?
Hio nikwamba mama ndio neno lakaribu kweny maisha yake nandio yuko karibu ila mtoto akizaliwa neno baba ndio lakwanza kulitamka bila kufundishwa kama kuna mmama hapo aliewai kulea muulize
 
Kwanini mama akifa familia inakosa mwelekeo hata kama baba ana uchumi mzuri? Kwanini baba akifa hata kama mama hana uchumi mzuri familia inatoboza?
Kaz yamama kulea nakaz yababa kutunza yan baba hata akiishi ulaya yeye akituma pesa tu inatosha ila mama yeye ndio mleaji kwaio kama baba kaacha pesa mama anateleza tu
 
Mtoto wangu tu hawezi kuwa na tabia mbovu vile

Lkn ni mtoto mzuri sana yule anahitaji kupewa mafunzo na kumshepu anaakili sana

Believe or not wa hivi nakaa naye kabisa

Mpaka ataingia line tu

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa asilimia kubwa sana dunia inaendeshwa na mawazo ya kike.

 
Kuna binadamu watakuja kusema ni mwanamke huyo huyo aliyemfundisha binadamu wa kwanza matumisi...
 
Kwa kuwa kwenye maafa hasa vita wahanga wakubwa ni wanawake na watoto, hivyo basi kama Marais wote duniani wangekuwa wanawake (Maamiri Jeshi Wakuu wanawake) unadhani kungekuwa na vita duniani? Siyo kwamba wasingeamuru majeshi kwenda vitani ili wahanga ambao ni wanawake na watoto wasiathirike na kwamba huenda dunia isingekuwa na uadui?
 
Kuna binadamu watakuja kusema ni mwanamke huyo huyo aliyemfundisha binadamu wa kwanza matumisi...
Ukimwachia mwanamke 2000/- kwamba ajibane wanywe uji hadi ukirudi jioni yeye atabajeti hiyo ela hadi familia itakula chakula badala ya uji. Mwanamke (breadwinner) akimwachia baba wa nyumbani 2000/- kwamba wanywee angalau chai hadi akirudi jioni ndiyo wale chakula nakwambia hiyo ela haitatosha chai. Kumbe mwanamke mawazo yake yanatembea kwenye mawanda mapana sana zaidi ya mawazo ya mwanaume.

Mwandishi wa kitabu hicho chini anasema akili ya mwanamke inaweza kubeba mambo/mawazo mengi kwa wakati mmoja na kuyachakata yote kwa wakati huo mmoja na kuyatolea ufumbuzi jadidi, huku mwanaume anao uwezo wa kubeba jambo moja tu kwa wakati mmoja. Anasema mwanamke ana uwezo wa kuona harakaharaka mambo kadhaa yaliyo nje ya agenda; ambayo mwanaume hawezi na akiweza basi ni jambo moja tu.

NB. Hii inanifanya niamini kwamba Tz kumpata Rais SSH ni sawa na kuokota dodo kwenye mwarobaini. Aidha, huenda JPM angeishi na kuongezwa muda bado hasingeweza kukamilisha miradi yote, lkn kwa nguvu za mwanamke za kuhandle mambo mengi kwa wakati mmoja (ambayo mwanaume hana) nasukumwa na busara ya Mwandishi kuamini kwamba Rais SSH anaweza kukamilisha miradi yote ndani ya muda bila kuomba nyongeza ya muda wa kukaa Ikulu.


Taswira kwa hisani ya google.

Kwa asilimia kubwa sana dunia inaendeshwa kwa mawazo ya kike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…