Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Yaan hapo naitaman ya mwenye pik pik huyo
Sema picha hazifunguku
 
Ya kakobe muachieni kakobe, kwani mmeona waliofunga hizo ndoa wanalalamika? kila watu wana utaratibu wao, kama wao wanaona ni sahihi kufanya hivo and wanafuraha, basi wacha wafurahie.

Na sisi ambao bila sherehe tunaona mambo hayaendi basi na tufanye sherehe. Tusilazimishe kila mtu awe kaa sisi
 
Mkuu unajaribu kupotosha uma!,hii inaitwa kubariki ndoa na wala sio ndio,hii ni kwa wale wanaoishi uchumba sugu na wanapika na kupakua,utakuwa hauelewi vizuri ndoa ni nini na kubariki ndoa ni nini !
amini usiamini, hata mtoto wake wa kumzaa alifunga ndoa namna hiyohiyo mwezi huu wa pili, na ilifungwa ndoa moja tu siku hiyo. huo ndio umekuwa msimamo wa kakobe tangu naanza kumjua. sisali pale, ila huwa namfuatilia, na msimamo huo ni wa kweli, ya kwamba, mke anakuwa ashakuwa mkeo pale tu wazazi wa pande mbili wakikubaliana kuwa muoane, cha kwanza au any of them kinaweza kuanza ni ninyi kukubaliana, halafu wazazi wenu pia wakubaliana, na wewe ukatoe mahali, kwisha habari. hizo mbwembwe zingine ni mapambo tu. alikuwa anatofautiana na wenzake wwenye msimamo kwamba, mfano, mimi nimetoa posa, nimetoa mahali, ninaishi na mwanamke tumeshazaa watoto lakini hatujabarikiwa kanisani, yapo makanisa hadi leo yanasema hapo ndoa hakuna. lakini kwenye Bible yeye anasema hizo kubariki hazikuwepo, wazazi wakukubaliana kukupatia mke mkayamaliza kule home tayari amekuwa mkeo. huku church mnakuja tu kubarikiwa. ndio maana hata serikali inatambua ndoa zote kuwa ni sawa, ziwe za kikristo, za kiislam, za boman mbele ya serikali ni sawa tu, huko kubarikiwa au kutobarikiwa serikalii haitambui, kwasababu hata wale wa bomani huwa hawabarikiwi kiislam wala kikristo. yapo makanisa yametengenisha familia nyingie tu, mtu ameishi na mwanamke miaka kadhaa wamezaa watoto rundo, wameamua kwenda kwenye hilo kanisa, wanaambiwa mnaishi bila ndoa mnazini, achaneni.
 
Funzo kubwa kwa vijana; kumbe inawezekana kuoa kwa bei poa kabisa na maisha yakendelea vizuri tu; humuelemei mtu wala hubaki na madeni.
 
nina ndugu aliolewa hapo mwaka juzi style ni hio hio ingawa baadhi walikodi magari, tulifanya sherehe ndogo baada ya kutoka kanisani. nashangaa za mwaka huu zimetrend hivi duuh.
 
Shughuli ya wazazi inaishia kwenye posa.

Ikishapokelewa unaweza hata usiende chachi maana ndoa tayari hapo
 
Mzee hayo madubwasha ya kukariri ndo madeni yenyewe.

Nshamwambia mama chanja wangu tutengane kwa muda kisha tuibukie kwa Kakobe tufunge upya
 
Nimewapenda bure nitafanya mchakato wa kuamia hapo. Kwanini utumie mamillion kwa shughuri ya siku moja[emoji1787]
Mbali ni kwamba imepunguza gharama, kwanza naona wamependeza sana kwa mavazi waliyovaa.

Pia kila anayeonekana kwenye picha ni mwenye furaha usoni. Kikubwa ni amani ya moyo na upendo wa dhati, haya mengine ni matokeo tu.
 
Naomba number ya fundi aloshona hayo magauni
 
Mbali ni kwamba imepunguza gharama, kwanza naona wamependeza sana kwa mavazi waliyovaa.

Pia kila anayeonekana kwenye picha ni mwenye furaha usoni. Kikubwa ni amani ya moyo na upendo wa dhati, haya mengine ni matokeo tu.
Sana wamependeza sana,siyo makitu yasiyo na ulazima.
 
Nimewapenda bure nitafanya mchakato wa kuamia hapo. Kwanini utumie mamillion kwa shughuri ya siku moja[emoji1787]
Sio siku moja ni masaa 60 tu. Haina haha ya kuhama pale unaposali unaweza kufunga watu wanne tu.
 
Wabongo wanafik jinsi wanavyopenda msosi na bia afu uwaambie ndo kanisan tu !!!mmmh
 

Halafu wewe jamaa siyo muelewa kabisa,watu wameshaamua kufanya hivyo wewe unakomaa siyo sawa,wewe kama nani? Acha kupangia watu maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…