Tatizo heshima niliyoijenga katika jamii, naheshimika mno, sipo tayari kuikabili aibu hii
Unajua sikuelewi? Mtu umeoa halafu unawaza utaonekanaje?
Huyo si mkeo? Kwani kwenye ndoa mnaenda kulima bamia?
Hayo ni matunda ya ndoa na mnapaswa muwe grateful. Kuna watu wanahangaika hawapati watoto.
Wengine mtoto wa kwanza anapata vizuri then miaka inapita mtoto wa pili wanatafuta milele daima hawapati. Especially kwa lifestyle diseases za siku hizi kwa wanawake. Karibu kila mwanamke ana fibroid au changamoto ingine ya uzazi.
Be grateful una mtoto mwingine anakuja. Lakini pia ujifunze na mkubaliane na mkeo kupanga uzazi going forward.
Btw: Nimeongea kwasababu imenigusa binafsi pia. Mke wangu alibeba mimba ya mtoto wa pili wakati wa kwanza ana miezi sita na ananyonya bado. Fast forward today, mkubwa ana miaka mitano na mdogo anakaribie minne mwezi wa tatu. Nina raha sana kila nikiwaangalia. Na wametupa nafasi ya kupambana na maswala mengine kwa sasa na kusahau ulezi kwa muda. Wife amerudi pia shule sasa.