Kwa bahati mbaya mke ameshika ujauzito tena

Kwa bahati mbaya mke ameshika ujauzito tena

Hongera sana mkuu.
Kwani ujauzito wa mwisho alijifungua kwa operation? Kama jibu ni hapana. Basi hongera tena. Cha muhimu awahi clinic mapema apewe ushauri.. aanze kutumia dawa za madini chuma na folic acid sababu mwili wake bado hauna store ya kutosha..

Upande wako anza kusaka hela kwa wingi maana hao watoto wataenda shule wakati mmoja.
Ahsante
 
Yaan kumpa mkeo ujauzito ni kujidhalilisha kumbe, kama amna tatizo kwa mkeo lea mimba na hyo mtoto

Miez9 ni mingi kwa mtoto kama utasimamia lishe na matibabu kwa ukaribu.

Labda kama unaogopa mimba ikianza kuonekana itajulikana ulikula mama bila kinga.
Hamna, ni fedheha kwangu na kwa mabosi zangu!
 
Unajua sikuelewi? Mtu umeoa halafu unawaza utaonekanaje?

Huyo si mkeo? Kwani kwenye ndoa mnaenda kulima bamia?

Hayo ni matunda ya ndoa na mnapaswa muwe grateful. Kuna watu wanahangaika hawapati watoto.

Wengine mtoto wa kwanza anapata vizuri then miaka inapita mtoto wa pili wanatafuta milele daima hawapati. Especially kwa lifestyle diseases za siku hizi kwa wanawake. Karibu kila mwanamke ana fibroid au changamoto ingine ya uzazi.

Be grateful una mtoto mwingine anakuja. Lakini pia ujifunze na mkubaliane na mkeo kupanga uzazi going forward.

Btw: Nimeongea kwsbb imenigusa binafsi pia. Mke wangu alibeba mimba ya mtoto wa pili wakati wa kwanza ana miezi sita na ananyonya bado. Fast forward today, mkubwa ana miaka mitano na mdogo anakaribie minne mwezi wa tatu. Nina raha sana kila nikiwaangalia. Na wametupa nafasi ya kupambana na maswala mengine kwa sasa na kusahau ulezi kwa muda. Wife amerudi pia shule sasa.
Hongera
 
Acha upumbavu akitoa hiyo mimba akafa utajiskiaje jinga kweli yan elimu yote haijakusaidia bado unataka uishi kuangalia watu watu wanakuonaje
 
Wewe ndiye uliyeandika utoto, huyo ndugu kaomba ushauri na mimi namshauri kwamba; kama ataona uhai wa huyo mtoto upo hatarini basi njia rahisi ni kutoa hiyo mimba, kutoa mimba kwa sababu za msingi sio dhambi.--- kuna sababu nyingi husan za kiafya zinazopelekea mimba kutolewa na hilo sio dhambi.
Kutoa mimba sio rahisi na sio vizuri
 
I'm too weary, yaani tuna mtoto wa miezi karibia 9 sasa, ila mke wangu jana kapima ujauzito baada ya kuhisi uchovu, kwa masikitiko makubwa ni mjamzito. Nitaficha wapi sura yangu Mimi? Naheshimika mno inakuwaje wakijua mke wangu mjamzito tena?

Yaani nionekane primitive Mimi? Nafikiria nimuambie tutoe ila navuta muda, mke wangu ndio chanzo cha yote, ananipa show huku mzunguko kausahau, na mimi siku reason!..

Nafikiria nimuambie akaitoe, naombeni mawazo yenu Wanajamvi!! Ndo nadhalilika hivyo
Kiongozi
Usiingie kwenye hiyo dhambi ya kutoa mimba
Mimi nilipata changamoto kama hiyo na niliipokea pamoja na kuwa ilinipa wakati mgumu kidogo mwanzoni
Wala usihofu, wataongea kidogo tu na hutawasikia tena kwani changamoto kama hiyo hutokea sana kwa mtoto wa kwanza kufuatana na wa pili. Daktari kabisa wa kutibu watu anaunganisha watoto iwe wewe; nini cha ajabu?
Jitahidi tu wife apate virutubisho murua na baadae kidogo huyo dogo unamuachisha kunyonya na kumnunulia maziwa ya formula. Atakua vizuri bila shida
 
Lea mkuu usiue hicho kiumbe huenda ndio mwanao wa mwisho binafsi imenikuta hiyo Mara mbili wife kajifungua mtoto wa kwanza analea miezi 6 mimba nikataka kuitoa nikashauriwa tukaacha sasa watoto miaka mitano kwa sita baada ya miaka mitatu na point mimba mtoto kazaliwa mwaka juzi Leo kafunga mwaka na nusu mimba nyingine nimekubali kulea maisha yanaenda usiangalie watu wanasemaje muhimu tafuta maziwa mbadala mtoto atakua safi kabisa pamoja na kwamba madokta wanashauri tuwanyonyeshe hivyohivyo nilichokiexperience wanaharisha bora kuuachisha apige lactogen anakuwa hutaamini.
 
Kutoa mimba sio rahisi na sio vizuri

Madaktari wakigundua kwamba mtoto kakaa vibaya tumboni kwa mama mjamzito na kamwe hataweza kujifungua kwa njia salama, njia rahisi na nzuri ni ipi katika hali hiyo??!; (1) kuacha hiyo mimba ikue hadi miezi 9 na mama afe na mtoto afe au wote wafe, au (2) kuitoa hiyo mimba mapema ili kunusuru maisha ya mama.??!.

Kumbuka unadai; kutoa mimba sio kitu rahisi na sio vizuri.

Mimi nasema; kitu kinakuwa rahisi na kizuri baada ya ulazima na umuhimu wake.
 
Wakiingia huwa hawapigi hodi, please zingatia lishe bora mbona mtoto wa miezi tisa anakula vyakula vyote maziwa unamnunulia kwa kuongeza calcium.
Acha hizo ww 😄😄😄
Mtt wa miez 9 anaweza kula ugal tembele 😟😟😟
Ila hata ukimlisha utakua umemfanyia ukatili wa hali ya juu aisee
 
I'm too weary, yaani tuna mtoto wa miezi karibia 9 sasa, ila mke wangu jana kapima ujauzito baada ya kuhisi uchovu, kwa masikitiko makubwa ni mjamzito. Nitaficha wapi sura yangu Mimi? Naheshimika mno inakuwaje wakijua mke wangu mjamzito tena?

Yaani nionekane primitive Mimi? Nafikiria nimuambie tutoe ila navuta muda, mke wangu ndio chanzo cha yote, ananipa show huku mzunguko kausahau, na mimi siku reason!..

Nafikiria nimuambie akaitoe, naombeni mawazo yenu Wanajamvi!! Ndo nadhalilika hivyo
Kutoa mimba? Acha kuwaza huo upuuzi, fuata ushauri wa daktari wako, watakua tu hao ndugu yangu wala usiwaze kuua mtoto wako
 
Tafadhali usitoe hiyo mimba zaeni tu pengine huyo unayemtoa ndiye Rais ajaye
 
Madaktari wakigundua kwamba mtoto kakaa vibaya tumboni kwa mama mjamzito na kamwe hataweza kujifungua kwa njia salama, njia rahisi na nzuri ni ipi katika hali hiyo??!; (1) kuacha hiyo mimba ikue hadi miezi 9 na mama afe na mtoto afe au wote wafe, au (2) kuitoa hiyo mimba mapema ili kunusuru maisha ya mama.??!.

Kumbuka unadai; kutoa mimba sio kitu rahisi na sio vizuri.

Mimi nasema; kitu kinakuwa rahisi na kizuri baada ya ulazima na umuhimu wake.
Uamuzi wa kuitoa bado ni hatari upande wa mama mzee, Tuwaheshimu sana akina mama maana hata kuibeba mimba kwa miezi tisa bado kujifungua nako kunakuwa na changamoto kuna wanaojifungua salama wapo wanaopoteza maisha
 
Back
Top Bottom