I'm too weary, yaani tuna mtoto wa miezi karibia 9 sasa, ila mke wangu jana kapima ujauzito baada ya kuhisi uchovu, kwa masikitiko makubwa ni mjamzito. Nitaficha wapi sura yangu Mimi? Naheshimika mno inakuwaje wakijua mke wangu mjamzito tena?
Yaani nionekane primitive Mimi? Nafikiria nimuambie tutoe ila navuta muda, mke wangu ndio chanzo cha yote, ananipa show huku mzunguko kausahau, na mimi siku reason!..
Nafikiria nimuambie akaitoe, naombeni mawazo yenu Wanajamvi!! Ndo nadhalilika hivyo
Hili jambo nimewahi kutana nalo mimi. Tena kama nilijua leo mtu anakazwa mimba. Kabla hata ya bao kutoka nilimuuliza kama yuko kwenye siku zake ni withdraw. Alihesabu vidole akaruhusu mseleleko. Baada ya mwezi kitu na box.
Nilipoambiwa ndoa imejibu tena mtoto mwingine akiwa na mwaka mmoja niliitika tu sawa na sikuongelea tena kuhusu mimba hiyo kwa wiki moja. Niliwaza mengi sana. Kwanza mke wangu alikuwa amejifungua kwa operation mtoto tunayelea. Kwa ushauri inakuwa baada ya OP mtoto mwingine apatikane angalau baada ya miaka miwili au mitatu, Sasa kwangu aibu inakuja baada ya mwaka , nilijiuliza ntantembeaje nimebemenda mtoto kama watu wanavyosema, halafu kafirst born nakapenda na kukaonea huruma tumekanyima kupata haki zake. Nilikuwa na maumivu hiyo wiki yote. Kuna wakati nilitamani tuitoe ila kwa kuwa sipendi hivyo vitu nilikaa kimya.
Lakini hiyo wiki ilinipa nafasi ya kutafakari thamani ya uhai na zawadi bora ya watoto. Nilijiuliza watu wanatafuta watoto siku wakipata wanabeba mimba mfululizo hata 4 ili kufidia , kwa nini mimi nipaniki? Najuaje baraka atakazo kuja nazo mtoto? Na je sina uwezo wa kulea. Jibu likawa hapana naweza. Niligundua kinachonisumbua ni macho ya watu na mitazamo yao na wala sio kiumbe kijacho.
Baada ya wiki maamuzi binafsi ilikuwa tutalea mimba na tumsubiri kijacho kwa hamu. Watu wanatamani hiyo fursa ya kupata mtoto hawaipati halafu mimi naumia kijinga. Kwanza nilifikiria mtoto mwenyewe ni wa ndani ya ndoa hata waseme vipi mimi naziba masikio nasonga mbele. Sex ndani ya ndoa matunda yake ni watoto haijalishi utavuna mwaka mzima, na sisi tumebarikiwa matunda hayo mazuri ambayo ni zawadi toka kwa Mungu ZABURI 127: 3 nenda kasome.
Jambo nililofanya nikumpigia Daktari wa wife wa mambo ya uzazi ili kujua usalama wa mama kwa ujio mpya wa mtoto na ndani ya tumbo lake ukizingatia alikuwa bado hajapona vizuri kidonda kutoka na kujifungua kwa Operation. Daktari aliamuru apelekwe kwa ajili ya uchunguzi. Baada ya hapo niliambiwa nisiwe na wasiwasi wowote mama na kiumbe cha tumboni watakuwa salama hakuna shida yeyote na alinihakikishia kumfuatilia kwa karibu ukuaji wa mimba yake mpaka atakapojifungua. Pia kuna dawa alipewa wife ili huyu mtoto mwingine ambaye ni binti aendelee kunyonya kwa angalau miezi 5-6 mbele bila kudhurika kutokana na mimba.
Basi nikaziba masikio nikasonga mbele mwishowe wife alijifungua kwa OP tena mtoto wa kiume. Na cha ajabu watoto wangu hawa huwezi fikiri kuwa wametofautiana kama mwaka mmoja na miezi tisa hivi. Dada mtu ana mwili unakimbia balaa utafikiri kamuacha miaka mitatu mdogo wake.
Nipo hapa naenjoy na wanangu ninaowapenda na sijutii kupandanisha mambo kwa kuwa ni matokeo mazuri ya ndoa.
Licha ya andiko refu nafikiri utajifunza kitu hapa na kupata ujasiri wa kusonga mbele. Nakutakia malezi mema ya mimba na mtoto aliyepo. Jambo la msingi Kumbuka kila mtoto anakuja na baraka zake pamoja na ugali wake duniani.
Sent from my SM-A115F using
JamiiForums mobile app