Kwa bahati mbaya mke ameshika ujauzito tena

Ahsante
 
Hamna, ni fedheha kwangu na kwa mabosi zangu!
 
Hongera
 
Acha upumbavu akitoa hiyo mimba akafa utajiskiaje jinga kweli yan elimu yote haijakusaidia bado unataka uishi kuangalia watu watu wanakuonaje
 
Kutoa mimba sio rahisi na sio vizuri
 
Kiongozi
Usiingie kwenye hiyo dhambi ya kutoa mimba
Mimi nilipata changamoto kama hiyo na niliipokea pamoja na kuwa ilinipa wakati mgumu kidogo mwanzoni
Wala usihofu, wataongea kidogo tu na hutawasikia tena kwani changamoto kama hiyo hutokea sana kwa mtoto wa kwanza kufuatana na wa pili. Daktari kabisa wa kutibu watu anaunganisha watoto iwe wewe; nini cha ajabu?
Jitahidi tu wife apate virutubisho murua na baadae kidogo huyo dogo unamuachisha kunyonya na kumnunulia maziwa ya formula. Atakua vizuri bila shida
 
mkuu mtoto wako akija kugundua ID yako hii baada ya miaka 15 labda atakudharau sana
 
Lea mkuu usiue hicho kiumbe huenda ndio mwanao wa mwisho binafsi imenikuta hiyo Mara mbili wife kajifungua mtoto wa kwanza analea miezi 6 mimba nikataka kuitoa nikashauriwa tukaacha sasa watoto miaka mitano kwa sita baada ya miaka mitatu na point mimba mtoto kazaliwa mwaka juzi Leo kafunga mwaka na nusu mimba nyingine nimekubali kulea maisha yanaenda usiangalie watu wanasemaje muhimu tafuta maziwa mbadala mtoto atakua safi kabisa pamoja na kwamba madokta wanashauri tuwanyonyeshe hivyohivyo nilichokiexperience wanaharisha bora kuuachisha apige lactogen anakuwa hutaamini.
 
Kutoa mimba sio rahisi na sio vizuri


Madaktari wakigundua kwamba mtoto kakaa vibaya tumboni kwa mama mjamzito na kamwe hataweza kujifungua kwa njia salama, njia rahisi na nzuri ni ipi katika hali hiyo??!; (1) kuacha hiyo mimba ikue hadi miezi 9 na mama afe na mtoto afe au wote wafe, au (2) kuitoa hiyo mimba mapema ili kunusuru maisha ya mama.??!.

Kumbuka unadai; kutoa mimba sio kitu rahisi na sio vizuri.

Mimi nasema; kitu kinakuwa rahisi na kizuri baada ya ulazima na umuhimu wake.
 
Wakiingia huwa hawapigi hodi, please zingatia lishe bora mbona mtoto wa miezi tisa anakula vyakula vyote maziwa unamnunulia kwa kuongeza calcium.
Acha hizo ww πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Mtt wa miez 9 anaweza kula ugal tembele 😟😟😟
Ila hata ukimlisha utakua umemfanyia ukatili wa hali ya juu aisee
 
Kutoa mimba? Acha kuwaza huo upuuzi, fuata ushauri wa daktari wako, watakua tu hao ndugu yangu wala usiwaze kuua mtoto wako
 
Tafadhali usitoe hiyo mimba zaeni tu pengine huyo unayemtoa ndiye Rais ajaye
 
Uamuzi wa kuitoa bado ni hatari upande wa mama mzee, Tuwaheshimu sana akina mama maana hata kuibeba mimba kwa miezi tisa bado kujifungua nako kunakuwa na changamoto kuna wanaojifungua salama wapo wanaopoteza maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…