Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Wakuu habari za asubuhi.

Ni matumaini yangu mmeamka salama siku hii ya pasaka.

Nina mpango wa kununua gari kwa bajeti ya Tshs 10m - 12m. Nipo mkoani na ni mara yangu ya kwanza kumiliki gari. Nina familia ya watu 6 yani wife watoto 3 na house girl.

Matumizi yangu ni kuendea kazini, kuwapeleka watoto shule, kwenda kanisani Jumapili na familia, kwenda mjini kununua mahitaji, na mara moja kwa mwaka kwenda kuwasalimia wazee kijijini.

Kutoka mahali ninapoishi hadi kazini kuna umbali wa 2Km rafu road, kwenda shuleni 3Km (1km rafu, 2Km rami), mjini 4Km (1Km rafu, 3Km rami), kanisani 2Km rafu road na kijijini kwa wazee ni 1150Km, takribani 70 rafu road baada kutoka mkoani.

Naomba ushauri kwa bajeti tajwa hapo juu naweza kupata gari gani inayoendana na matumizi yangu? Nikipata inayotumia mafuta kati ya 10Km - 15km/1Lt inaweza kunifaa.

Natanguliza shukrani za dhati.
Kwa maelezo uliyo toa Tua hapa mkuu

Toyota CAMI
aff1a06301ea25594d223fc7775814a8.jpg

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app

Kwanza ground clearance ni kubwa kuliko gari unazoshauriwa Raum, Premio na Spacio na bado ina sifa nyingine nyiingi kuzi zidi na ni offroad vehicle achilia mbali mwonekano wake kama prado[emoji2956][emoji2960]
 
Kwa maelezo uliyo toa Tua hapa mkuu

Toyota CAMIView attachment 2581864

Ana familia ya watu 6 wengine watapakatana,
 
Kwa gari ya familia kubwa kwa brand ya Toyota, zitakazokufaa ni Wish, Spacio, Sienta, na Raum. Ila bajeti yako ipo chini. Ungeongeza angalau ifike 14mil utapata kwa kuagiza. Miaka 5 iliyopita kwa bajeti hiyo ungeweza kupata Raum nzuri tu. Ila kwa sasa angalau uwe na 14mil kwenda juu. Corona ilileta mabadiliko. Freight charges zimepanda kutoka $800 hadi $1800.

BTW, nimeangalia Beforward asubuhi hii, Sienta ya 2004 (7 seater) ni $2994 (7mil) na ushuru wake ni 5.2mil. Hapo bado charges za bandari, clearance, na service ya kuanzia.
 
Kwa maelezo uliyo toa Tua hapa mkuu

Toyota CAMIView attachment 2581864

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app

Kwanza ground clearance ni kubwa kuliko gari unazoshauriwa Raum, Premio na Spacio na bado ina sifa nyingine nyiingi kuzi zidi na ni offroad vehicle achilia mbali mwonekano wake kama prado[emoji2956][emoji2960]
Ataipata kwa hiyo budget yake ya million 10 mpaka 15 ?
 
Back
Top Bottom