Kwa gari ya familia kubwa kwa brand ya Toyota, zitakazokufaa ni Wish, Spacio, Sienta, na Raum. Ila bajeti yako ipo chini. Ungeongeza angalau ifike 14mil utapata kwa kuagiza. Miaka 5 iliyopita kwa bajeti hiyo ungeweza kupata Raum nzuri tu. Ila kwa sasa angalau uwe na 14mil kwenda juu. Corona ilileta mabadiliko. Freight charges zimepanda kutoka $800 hadi $1800.
BTW, nimeangalia Beforward asubuhi hii, Sienta ya 2004 (7 seater) ni $2994 (7mil) na ushuru wake ni 5.2mil. Hapo bado charges za bandari, clearance, na service ya kuanzia.