Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Kwa maelezo uliyo toa Tua hapa mkuu


Toyota CAMI

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app


Kwanza ground clearance ni kubwa kuliko gari unazoshauriwa Raum, Premio na Spacio na bado ina sifa nyingine nyiingi kuzi zidi na ni offroad vehicle achilia mbali mwonekano wake kama prado[emoji2956][emoji2960]
 
Ana familia ya watu 6 wengine watapakatana,
 
Kwa gari ya familia kubwa kwa brand ya Toyota, zitakazokufaa ni Wish, Spacio, Sienta, na Raum. Ila bajeti yako ipo chini. Ungeongeza angalau ifike 14mil utapata kwa kuagiza. Miaka 5 iliyopita kwa bajeti hiyo ungeweza kupata Raum nzuri tu. Ila kwa sasa angalau uwe na 14mil kwenda juu. Corona ilileta mabadiliko. Freight charges zimepanda kutoka $800 hadi $1800.

BTW, nimeangalia Beforward asubuhi hii, Sienta ya 2004 (7 seater) ni $2994 (7mil) na ushuru wake ni 5.2mil. Hapo bado charges za bandari, clearance, na service ya kuanzia.
 
Ataipata kwa hiyo budget yake ya million 10 mpaka 15 ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…