Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Shem nashukuru kwa ushauri wako! Baada ya kunishauri, nimeingia google ili nijiridhishe na hiyo gari. Ni kweli gari ni nzuri ila sasa inaonekana kwenye ulaji wa mafuta itakuwa changamato. Nyingi zina cc 2,350, 2,400, 2,000 na 1,900 ambayo naona nitashindwa kuitumia kama nilivyoeleza kwenye bandiko langu. Nimeshafanya makadirio ya matumizi ya mafuta yasizidi lita 2 kwa siku, yaani Tsh.6,000/day, ambayo ni 180,000/= kwa mwezi. Ndiyo maana nikasema gari inayotumia 1lt/10 - 15Km itanifaa zaidi.
 
Nimeendelea kufanya utafiti nimegundua zipo gari nyingi ambazo ni familly car na zina ukubwa wa engine (CC) wa kawaida tu kama vile HONDA STREAM, VOLKSWAGEN TOURAN, MAZIDA PREMACY, SUBARU EXIGA, TOYOTA SIENTA, n.k lakini upatikanaji wa spea ndiyo tatizo na zipo chini sana (ground clearance) maana matumizi yangu yanahusisha mchanganyiko wa njia za vumbi na lami. Mpaka sasa ninafikiria Spacio, Raum na Honda CR-V, bajeti zake naweza kuongezea kidogo nikapata.
 
Ongeza ongeza kidogo ununue Premio ya CC 1490 au ya CC 1790.
 
Nakazia
Mshua's
 
Ingia zenji lenga Suzuki Escudo old Kwa million 6 imenyoka sn , hutajuta. ushuru kama million 2.5 hv, chukua kuanzia namba H kushuka chini, million moja njoo piga rangi na sofa ndani, umemaliza , gari ngumu ipo juu ,ina 4WD, cc 1590. Unataka nn tena hapo ..
 
Probox muzee.
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri. Hii unamvua mtu au inauzwa showroom?
 
Probox muzee.
Nasikia Succeed ndiyo ipo vizuri kuliko Probox. Halafu, hizi gari wanasema zinasimamishwa sana njiani na matrafic ukiwa highway, wanadai zinatumika kubeba magendo na kujaza watu wengi kwenye buti. So, type ya watu wanaomiliki inaonekana wana matumizi mabaya ya haya magari. Naogopa nisije nikaharibu status yangu mtaani........
 
Poa...Allex vipi?
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri. Hii unamvua mtu au inauzwa showroom?
Unamvua mtu ,mpya befoward inarange million 25 na zaidi, lakini Zanzibar ni ndogo gari hazitembei sana, nyingi engine bado Safi
 
Hiyo hela yote Ukilimia matikiti heka 20 unapata faida million 90
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…